Tuesday, October 30, 2012

Picha zilizobamba dunianiii.....



Hawa wanapendezana ile mbayaaaa... kila eneo pamokoooo.....

Justin Bieber na Selena Gomez!

Kuna mwenye swaliiiiiiiiiiii......

SUMA LEE AIBIWA GARI

Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri haina shaka kuwa utakuwa unakumbuka stori iliyochukua nafasi kwenye kipindi cha XXL siku chache zilizopita juu ya nyota wa songi la 'Hakunaga' Suma Lee kupata ajali wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya kupiga shoo.
Taarifa kutoka Coco Beach zinasomeka kuwa nyota huyo mzaliwa wa mkoa wa Tanga ameibiwa ndinga yake hiyo aina ya Land Cruiser VX mwishoni mwa wiki iliyopita wakati alipokuwa kwenye mapumziko ya wikiend katika ufukwe wa bahari ya hindi.
"Haikuwa siku nzuri kwangu, nimeibiwa gari na watu ambao nahisi walikuwa wanaifuatilia kwa siku nyingi maana hata wakati wanaiba watu walikuwa karibu waliniambia kuwa watu hao hawakuvunja wala kuharibu chochote walichokifanya ni kufungua mlango kama ambavyo mimi huwa nafanya na kuwasha gari kisha kuondoka…"
Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri haina shaka kuwa utakuwa unakumbuka stori iliyochukua nafasi kwenye kipindi cha XXL siku chache zilizopita juu ya nyota wa songi la 'Hakunaga' Suma Lee kupata jari wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya kupiga shoo.
Hii ni gari ambayo inayofanana na gari aliyoibiwa Sumalee.

Taarifa kutoka Coco Beach zinasomeka kuwa nyota huyo mzaliwa wa mkoa wa Tanga ameibiwa ndinga yake hiyo aina ya Land Cruiser VX mwishoni mwa wiki iliyopita wakati alipokuwa kwenye mapumziko ya wikiend katika ufukwe wa bahari ya hindi.
"Haikuwa siku nzuri kwangu, nimeibiwa gari na watu ambao nahisi walikuwa wanaifuatilia kwa siku nyingi maana hata wakati wanaiba watu walikuwa karibu waliniambia kuwa watu hao hawakuvunja wala kuharibu chochote walichokifanya ni kufungua mlango kama ambavyo mimi huwa nafanya na kuwasha gari kisha kuondoka nalo kama la kwao," alisema Suma
Akiendelea zaidi Suma alisema kuwa kwa kuwa suala liko polisi hawezi kuzungumza sana ila ana uhakika gari yake ataipata tu kwani anafahamu watu wengi wanouza vifa avya magari Kariakoo labda kama watu hao wakiamua kulifugia kuku...alimaliza.

Friday, October 26, 2012

TV ZENYE MIGONGO NA MATUMBO MAKUBWA PIA ZITAPOKEA MATANGAZO YA DIGITAL






Imeelezwa kuwa TV zote zikiwemo zile zenye migongo, matumbo na viuno virefu zote zina uwezo sawa wa kupokea matangano ya digitali na Watanzania waepuke uvumi wa watu wachache wanaodai kuwa TV  za zamani hazitapokea zitafutwa mara Tanzania itakapoingia kwenye mfumo wa Digitali.
Wito huo umetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano hapa nchini TCRA ambaye pia na Mratibu wa Ofisi za Kanda, Bw. Victor Nkya, wakati wa mkutano wa Wataalamu wa Mawasiliano ya Habari kwa njia ya digitali kutoka nchi za SADC unaojadili umuhimu wa mfumo wa Digitali.
Bw. Nkya amesema kuwa wananchi hawana haja ya kuwa na hofu juu ya TV walizonazo zikiwemo zenye matumdo na migongo mikubwa kuwa hazitaweza kupokea matangazo ya televishen katika mfumo mpya wa digitali.
Amesema kutokana na watu wengi kutumia televishen za Analojia, ni lazima kila mmoja wetu awe na kingamuzi na kazi ya Mamlaka ya mawasiliano ni kuwajengea wananchi matumaini na kuepuka kudanganywa.
Kwa siku za hivi karibuni baada ya Tanzania kuridhia mabadiliko ya mfumo wa Digitali, wananchi wamekubwa na wasiwasi wakidhani kuwa huo ndio mwisho wa tv za zamani.
Awali akifungua Mkutano huo wa siku tatu hapa mjini Zanzibar, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mh. Rashid Suleiman, amewataka wananchi kukabiliana na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa mabadiliko ya kutoka katika mfumo wa analojia na kuingia katika digitali.
Amesema ni vema wananchi wakahama mapema kutoka katika mfumo huo wa zamani ili kuepuka usumbufu wakati yatakapotokea mabadiliko hayo kwani hakutakuwa na muda wa nyongeza kama Watanzania walivyozoea.
Na kuna umuhimu wa wananchi pia kusikiliza maelekezo ya wataalamu badala ya kusikiliza propaganda za watu wasio na ujuzi juu ya teknolojia hiyo.
"Watanzania hawana haja ya kuogopa na badala yake wajiandae kujipatia vingamuzi na kinyume cha hivyo watashindwa kupata matangazo ya televishen kama wanavyotarajia." Alisema Waziri.
Amesema kila mabadiliko yana hasara na faida zake, lakini kwa mabadiliko ya kutoka katika mfumo wa analojia kwenda digitali, kuna faida kubwa na moja ya faida hizo ni kuwawezesha watu wote kupokea matangaza sawa na yenye ubora unaofanana na kwa wakati muafaka.
Mkutano huo wa siku tatu unazishirikisha nchi zote za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC ikiwemo  Angola, Afrika ya Kusini, Malawi, Namibia, Botswana, Swazlland, Lesotho, Msumbiji na wenyeji Tanzania.

Wednesday, October 24, 2012

BIN ZUBEIRY YASHINDA TUZO YA COPA COCA COLA 2012


Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma ya Coca Cola Kwanza, Evans Mlelwa (kulia), akimkabidhi Mahmoud Zubeiry aka BIN ZUBEIRY wa bongostaz.blogspot.com (kushoto) mfano wa Hundi ya Sh. Milioni 2, baada ya kushinda tuzo ya Mwandishi bora wa blogs wa mashindano ya Copa Coca Cola. Wengine katikati ni Meneja wa Sprite, Warda Kimaro na Katibu wa TASWA, Amir Mhando.
Jimmy Tara naye alipokea kitu chake...

 KAMPUNI ya Coca Cola Kwanza, leo imewapa tuzo Waandishi watano wa Habari nchini, baada ya kuibuka vinara katika tuzo za Waandishi Bora wa mashindano ya soka ya vijana kwa umri chini ya miaka 17, Copa Coca Cola yaliyofanyika Julai mwaka huu.
Upande wa Blogs, bongostaz.blogspot.com ya BIN ZUBEIRY imeibuka kinara na kuzawadiwa Sh, Milioni 2 sawa na washindi wengine, upande wa Televisheni, Jimmy Tara wa ITV, Radio, Amry Masare wa Radio One, Magazeti, Japhet Kazenga wa Daily News na Mpiga Picha, Mohamed Mambo wa Habari Leo.
Tuzo hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa Coca Cola Kwanza, Evans Mlelwa, makao makuu wa kampuni hiyo ya vinywaji baridi, Mikocheni, Dar es Salaam.
Mchakato wa kutafuta washindi uliendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ambacho leo kiliwakilishwa  na Katibu wake, Amir Mhando.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi Somoe Ng'itu mwandishi wa gazeti la Nipashe wa pili kutoka kulia akiwa bize huku mwenzie akitafakari..

story, pix from Bin Zubery..

HONGERA BIN ZUBERY.......huu ni mwanzoooo tuuuu.


Monday, October 22, 2012

MATONYA AKIRI KUWA BONGO MOVIE WANAIGIZA HADI KWENYE MAPENZI



Inadaiwa kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Matonya aka Tonya Boy,alifungiwa ndani kimapenzi na mmoja ya wasanii wa bongo movie na kulizwa shilingi za kitanzania milioni 6, sasa ameamua kuweka wazi kuwa wanawake wa tasnia hiyo ni michosho kwani wanapemnda hela na wanaleta maigizo hadi kwenye mapenzi.
MATONYA,alidai kuwa kuna mmoja wa mademu wazuri wanaovuma kwenye tasnia bongo movie ndiye aliyefanya mchezo huo mchafu kwani alijifanya anampenda sana kumbe alikuwa anamuigizia na alikuwa na ishu yake.
Alidai baada ya tukio hilo kutokeo demu huyo hakumuona tena na alikuja kusikia yupo mkoani kitu ambacho kilimfanya aishiwe nguvu kwani hakuamini kilichotokea na hapo ndipo alipoamini kuwa mademu wa tasnia hiyo ni wapigaji na ukiwaonesha kwako utajuta.
"Bongo movie hakuna demu yaani hata bure siwataki tena yani wanaleta maigizo hadi kwenye mapenzi...dah kweli hii tasnia ina laana na inahitaji kuombewa kwani wasanii wake wana tamaa ya hela na wanamapepo ya ngono yani wakimuona mwanaume ana hela basi mate yanawatoka, hata bure siwatakiiii....."alilala Matonya.
Hata hivyo alipoulizwa jina la msanii huyo wa filamu alishindwa kumtaja kwa madai kuwa hata kama aliiba kiasi hicho cha pesa lakini kwa upande wake hana bifu naye ingawa hatamani hata kumuona.
By

Saturday, October 20, 2012

Waandamanaji 53 mbaroni,baadhi wapenya na kutinga Ikulu

****JWTZ yadhibiti mitaa Kariakoo, maduka barabara zafungwa

picha zikiwaonyesha waandamanaji waliodhibitiwa.....

Magari ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) yakiwa yamepakia wanajeshi tayari kukabiliana na waandamanaji wa Kiislamu eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam jana.
Jiji la Dar es Salaam jana lililipuka hata kulazimika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuingilia kati na kuongeza nguvu kudhibiti  vurugu kubwa zilizotikisa eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, zilitokana na maandamano ya baadhi ya waumini wa Kiislamu waliokuwa wanataka kwenda Ikulu.
Magari kadhaa ya JWTZ yaliyosheheni askari  wa jeshi hilo yaliranda katika mitaa mbalimbali ya  jiji  na eneo la Wizara ya  Mambo ya Ndani  na  Ikulu  huku helkopta ya polisi ikiwa angani kufuatilia usalama wa eneo hilo.
Askari wa JWTZ waliingilia kati kusaidia jeshi la polisi lililoonekana kuzidiwa nguvu baada ya waandamanaji hao kupambana na polisi hao kwa kuwarushia mawe.
Askari hao waliokuwa na silaha, ikiwemo mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na risasi za moto, walitanda katika maeneo mbalimbali ya Jiji hilo.
Maandamano na vurugu hizo zilisababisha shughuli mbalimbali  hasa biashara na usafiri kusimama huku wafanyakazi wa maeneo ya mjini kuondoka mapema maofisini.
Waumini hao waliandamana  kuishinikiza  serikali imuachie huru  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislam Tanzania  Sheikh Issa  Ponda, aliyefunguliwa mashtaka ya uchochezi pamoja na waumini wengine kadhaa walioko mahabusu.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, pamoja na Mkuu wa Mkoa Said Meck Sadik, kwa nyakati tofauti waliwasihi waumini kutawanyika mara baada ya kumaliza ibada ya Ijumaa jambo ambalo baadhi ya Waislam hawakuliafiki.
Askari wa JWTZ  hawakujihusisha na kamata kamata  ama kupambana na waandamanaji moja kwa moja lakini walikuwa nyuma ya polisi kuhakikisha kuwa pale nguvu inapopungua wanaingilia .
Pamoja na askari wa  JWTZ, Vikosi  vya  Kutuliza Ghasia  (FFU),  vikishirikiana na  askari wa vikosi vya  mbwa pamoja na wanamgambo wa jiji walikabiliana na maandamano yaliyoanza baada ya swala ya Ijumaa.
KUPAMBANA NA WAANDAMANAJI
Katika vurumai hizo polisi walitumia virungu, mabomu ya machozi, maji ya kuwasha huku wengine wakiwa na bunduki na risasi za moto kuwatawanya waandamanaji ambao walijibu kwa kuwarushia mawe na vitu vingine.
Licha ya kuwa na vurumai hizo  gari la polisi lilitoa tangazo kwa wanausalama kufanya kazi yao kwa tahadhari na kukataza ukamataji watuhumiwa na kudhibiti vurumai usitumie risasi za moto  na mabomu ya machozi yaliyokuwa yanarushwa yasielekezwa kwa raia.
Kadhalika polisi  waliuzingira  msikiti wa Idrisa ulioko karibu na kituo cha Polisi cha Msimbazi  kufuatia idadi kubwa ya waandamanaji kukimbilia humo. Ili kuwatoa waliokuwa  mafichoni  polisi walimwaga maji ya kuwasha ili kuwatoa waandamanaji walioingia ndani kwa  kuruka ukuta.
Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji  waliokuwa wametanda barabarani hali iliyosababisha barabara  kadhaa zikiwemo za Kariakoo, Kinondoni, Kawawa na Morogoro kufungwa.
Mathalani watu walishindwa kupita kwenye barabara ya Kinondoni inayoungana na ile ya Kawawa kutokana na polisi kudhibiti maandamano hayo na kusababisha njia hiyo isipitike.
KARIAKOO YALIPUKA
Kariakoo,  ambayo kiuchumi ni  kitovu kikubwa cha biashara za Tanzania jana ilizizima  kwa moshi na kelele za mabomu na kusababisha  biashara za mabenki, maduka ya fedha, soko kuu la vyakula  na bidhaa za walaji kufungwa kwa muda wote.
Pia ofisi na vioski zinapouzwa bidhaa na huduma mbalimbali vilifungwa  kwenye  sehemu nyingine za mitaa  ya katikati ya jiji zilizohofiwa kukumbwa na  vurumai hizo.
Eneo hili halikuwa shwari kwani wananchi wakiwemo wanafunzi walijikuta katika wakati mgumu huku wangine wakipigwa na mgambo wa jiji  na kuishia mikononi mwa polisi wa FFU.
Uharibifu wa mali ulitikisa kwa kuchoma matairi katikati ya  barabara pamoja na wezi kupora kwa urahisi bidhaa zilizokuwa maeneo ya wazi.
NIPASHE iliyokuwa eneo la tukio, ilishuhudia malori ya polisi yenye namba PT 18448 , PT 2093, PT 1145 na T662 APM yakiwa yamebeba watuhumiwa na gari la  makachero wa upelelezi yakisomba watu kadhaa waliokamatwa kwenye vurumai hizo na kuwapeleka  kituo cha Msimbazi .
Walioshikiliwa watabakia rumande hadi Novemba Mosi wakisubiri maamuzi ya hatua zitakazochukuliwa. Kadhalika polisi walifanya msako wa nyumba kwa nyumba ili kuwakamata waliokuwa  wanapambana nao wakiwa majumbani.
TISHIO LA MAISHA
Wakati huo huo  vurugu hizo zimesababisha mwanamke  mmoja ambaye hakufahamika kuzirai na kupoteza fahamu kufuatia milipuko ya mabomu ya kutoa machozi iliyorindima Kariakoo.
WANANCHI WALAANI
Watu mbalimbali  wamelaani tukio hilo na kuitaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wanaosababisha vurumai  kwani zinahatarisha amani ya nchi
Kwa upande wake, Skeikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhadi Salum aliwaomba Waislamu kuacha kuandamana na kwamba waliache sheria ichukue mkondo wake  na suala la dhamana   ni haki ya kila mmoja, hivyo watapatiwa.
Viongozi wa dini walitoa wito wa kutafuta suluhu kwa kuaa pamoja ili kufikiana muafaka.
KOVA ALONGA
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleimani Kova, akizungumzia vurumai za jana  alisema hakuna polisi wala raia aliyepoteza maisha jana.
Kova aliongeza kuwa waliokamatwa ni  kutokana na vurugu hizo ni 53 na kwamba walitiwa mbaroni baada ya kukaidi amri ya serikali ya kuwataka wasiandamane . Katika hatua nyingine alisema waliojeruhiwa ni wale waliokimbia ovyo.
Alisema hakuna risasi zilizotumika mbali na mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kudhibiti vurugu hizo.
NCHIMBI ATETA NA VIONGOZI WA ULINZI
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi, jana alikutana na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wa wizara  hiyo. Habari  tulizozipata kabla ya kwenda mitamboni zilisema.
JK ATOA POLE
Rais  Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema kuomboleza kifo cha askari polisi  Said Abdulrahman  aliyuawa  kikatili visiwani  Zanzibar.
Abdulrahman wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), aliuawa kinyama kwa kupigwa mapanga kichwani na mikononi usiku wa Jumatano wiki hii  katika eneo la Bububu  wakati akirejea nyumbani baada ya kazi kazi.
 “Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na taarifa za kuuawa kikatili kwa askari wetu Said Abdulrahman wa kikosi cha Kutuliza  Ghasia usiku wa tarehe 17 Oktoba wakati  akirejea nyumbani kwake, baada ya kukamilisha zamu yake ya kulinda usalama wa raia na mali zao kwa siku hiyo,” alisema Rais Kikwete.
“Kitendo hiki cha mauaji ni kitendo kiovu, ni cha kikatili na kinachostahili kulaaniwa na kufanyiwa kila aina ya uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria haraka iwezekanavyo,” alisema Rais Kikwete katika salamu hizo.
Alisema anaungana  na familia hiyo kumwomba Mwenyezi Mungu, ailaze roho yake mahala pema peponi .

HOSPITALI YA AMANA
Majeruhi tisa wa vurumai hizo walifikishwa katika hospitali ya Amana ambapo nane kati yao walitibiwa na kuruhusiwa wakati mmoja Neema Samson (26) amelazwa.

CHANZO: NIPASHE

KILICHOSABABISHA MAUWAJI YA KAMANDA BARLOW CHABAINIKA.

Marehemu Barlow....

MWELEKEO wa upelelezi wa mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow umebadilika na sasa tukio hilo linahusishwa na kisasi cha mapenzi na tayari mtu mmoja anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi Mwalimu Dorothy Moses kutiwa mbaroni na polisi.Awali, ilidaiwa kwamba Kamanda Barlow ambaye aliuawa kwa risasi usiku wa kuamkia Jumamosi muda mfupi baada ya kumfikisha mwalimu huyo nyumbani kwake, alivamiwa na majambazi.
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI, Robert Manumba alithibitisha jana kukamatwa kwa mtu huyo (jina tulihifadhi) akisema: “Ni kweli mtu mmoja amekamatwa, lakini kwa sasa siwezi kuzungumzia kwa kina kuhusu suala hilo kwa sababu bado tunamhoji na tunaendelea na uchunguzi. Tutakapokamilisha, tutatoa taarifa.”
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lily Matola pia alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo. Hata hivyo, alisema amesikia habari hizo kwa kuwa yuko safarini kwenda mkoani Kilimanjaro kwenye mazishi ya kamanda huyo... “Hayo nimesikia, lakini kwa sasa sipo Mwanza hivyo siwezi kuzungumzia lolote.”
Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, zinaeleza kwamba upelelezi wa mauaji hayo umefanikiwa kwa hatua kubwa na kwamba mtu huyo alikamatwa Dar es Salaam baada ya kuwekewa mtego na makachero waliopo katika timu ya uchunguzi na alisafirishwa hadi Mwanza ambako anashikiliwa na jeshi hilo.

Ilielezwa kuwa mtu huyo alikamatwa kutokana na kuwapo kwa taarifa za siri za kiitelejensia kutoka kwa watu mbalimbali.

"Kuna hali imefunguka na imesaidia sana. Inaonyesha kwamba Dorothy alikuwa na uhusiano na mtu huyu ambaye alikuwa akifika nyumbani kwake, kama mumewe na watu wanajua jambo hili,” alieleza mmoja wa askari polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini
.
Alisema kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba uamuzi wa mwalimu huyo kusitisha uhusiano wa mapenzi na mtu huyo huenda ndicho chanzo cha mauaji hayo lengo likiwa ni kumshawishi Dorothy kurejesha uhusiano
.
"Mimi natambua kwamba huyu jamaa na Dorothy walikuwa na uhusiano na inajulikana mjini kuwa hata mke wa mtuhumiwa anatambua jambo hilo kwani walishagombana siku moja mjini na hata katika msiba nyumbani kwao na mtuhumiwa,” alisema mama mmoja (jina tunalo), aliyejitambulisha kama mmoja wa marafiki wa karibu wa Dorothy
.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitangiri (jina tunalo), anasema amekuwa akimfahamu mtuhumiwa aliyekamatwa kama baba mwenye nyumba hiyo na kila mara amekuwa akimkuta hapo nyumbani wakati wa kujisomea na wanafunzi wenzake.

"Mimi ninamfahamu kama baba wa rafiki yangu na nimewahi kumkuta wakati wa kujisomea hapo nyumbani na watoto wa nyumba hiyo.”

Dorothy ambaye ametajwa kuwa mjane, ni Mwalimu katika Shule ya Msingi Nyamagana na tangu kufariki kwa mumewe Ofisa wa zamani wa TRA, Modest Lyimo mwaka 1997.

“Watu wote wanajua kwamba mtuhumiwa alikuwa akitembea na huyo mwalimu, wameonekana mara nyingi wakiwa muziki,” alieleza mmoja wa ndugu wa karibu wa mke wa mtuhumiwa.

Hili ni tukio la tatu mkoani Mwanza kutokea kwa ofisa wa polisi kuuawa. Katika tukio la awali lililotokea mwaka 1987, askari aliyetambulika kwa jina la Inspekta Gamba aliuawa kwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Nyakato na katika tukio la pili mwaka 1997, aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Kati ASP Mahende aliuawa kwa kupigwa risasi eneo la Bugando saa nne usiku alipokuwa akifuatilia majambazi waliokuwa wakijitayarisha kuvamia


Dar wamuaga Kamanda Barlow

Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal aliongoza waombolezaji waliofika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Barlow nyumbani kwake, Ukonga Dar es Salaam jana
.
Mwili wa Kamanda Barlow ambao unasafirishwa leo kwenda mkoani Kilimanjaro kwa mazishi, uliwasili nyumbani kwake saa 6.45 kabla ya kupelekwa katika Kanisa la Mtakatifu Agustino, Ukonga kwa ajili ya ibada na kutoa heshima za mwisho.
A
kitoa salamu za Serikali, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima alisema kifo cha Kamanda Barlow ni pengo kwa taifa... “Tutahakikisha watuhumiwa wanapatikana kwa mikono yote miwili na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao.”
M
kuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema alisema juhudi za kuwasaka watuhumiwa zinaendelea kwa ushirikianao wa wananchi.
“Kifo cha Kamanda Barlow kimeacha pengo kwani hivi sasa askari mmoja analinda watu 1,300 hivyo kwa kifo chake unaweza kuona ni pengo la aina gani na ukilinganisha yeye alikuwa kamanda wa mkoa mzima,” alisema IGP Mwema.

Alisema jeshi lake litaendelea kulinda amani ya wananchi na kifo cha Kamanda Barlow kinalifanya liongeze nguvu.

Akitoa mahubiri, Padri Veri Urio alisema kila jambo hutokea kwa wakati na kifo cha Kamanda Barlow kimesababishwa na watu. Alisema mwenye mamlaka ya kuondoa uhai wa mtu ni Mungu pekee hivyo waliosababisha kifo chake siku ikifika, watajibu kwa nini walifanya hivyo
.
IGP Mstaafu, Omary Mahita alisema atamkumbuka Kamanda Barlow kwa uchapaji wake kazi tangu akiwa polisi Interpol (polisi kimataifa)alifanya kazi kwa weledi uliotukuka
.
“Daima nitamkumbuka kwani nimefanya naye kazi sehemu tofauti na askari waliobaki waige mfano wake wa uwajibikaji” alisema Mahita.

Mbali ya Dk Bilal, viongozi wengine walioshiriki katika ibada hiyo jana ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), makamanda wa polisi, viongozi wa Serikali na vyama vya siasa na wananchi.

Imeandikwa na Frederick Katulanda, Mwanza na Ibrahim Yamola, Dar.
CHANZO CHA HABARI HII NI "GAZETI LA MWANANCHI".

Thursday, October 18, 2012

Mr II, Sugu, Baba Sasha ama Joseph Mbilinyi aibuka na hiki...


Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu huku akiwa bize na shughuli za kumlea mtoto wake mpya, Sasha Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ameibuka na status katika page yake ya facebook ya kulaani vikali kauli za Naibu Waziri bw Malima....sitaki kuongeza chumvi cheki jinsi Mbunge wetu Mbilinyi alivyokisanua....full kujiamini.....kinegaaaaaaaaa.
 Sasha ameshakua.....
Baba Sasha akiwajibika....bizeee tuuuu kumlea Sasha..jamaa kamkologa weeeeee......Chezea Baba Sasha wewee!

Dk. Ulimboka aibuka, atoa ya moyoni

Ulimboka alipokewa kwa shangwe baada ya kutua uwanja wa ndege alikuwa akitokea nje ya nchi  kutibiwa.....

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka, ameibuka na kusema yupo tayari kueleza yaliyompata ikiwa serikali itaunda chombo huru kwa ajili ya kuchunguza sakata hilo.
Kwa mara ya kwanza jana, Dk. Ulimboka alitoa tamko lilisosainiwa na wakili wake, Rugemeleza Albert Nshala na kusomwa na wakili Nyaronyo Kicheere, jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari.
Dk. Ulimboka mwishoni mwa Juni, mwaka huu, alitekwa na watu wasiofahamika katika barabara ya Tunisia, wilayani Kinondoni na kupigwa, kung’olewa meno na kutupwa katika msitu wa Mabwepande, nje ya Jiji la Dar es Salaam.
Hata hivyo, jana waandishi wa habari walishikwa na butwaa baada ya kuona tamko hilo zito likisomwa na Wakili Kicheere badala ya Dk. Ulimboka mwenyewe kama watu wengi walivyotarajia.
Wakili Kicheere aliwaambia waandishi wa habari kwamba Dk. Ulimboka, alishindwa kufika mbele yao na kusoma tamko hilo kwa kuwa yupo nje ya nchi kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Hata hivyo, Kicheere hakutaja nchi ambayo Dk. Ulimboka amekwenda kuchunguzwa afya wala siku aliyoondoka.
Katika tamko hilo, Dk. Ulimboka alisema yupo tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo huru na makini vitakavyoundwa na serikali ili aeleze ukweli wa kilichompata.
Katika tamko lake hilo, Dk. Ulimboka alisema ametafakari sana na kuona kwamba kama hatatoa tamko hilo, atakuwa hajawatendea haki Watanzania wenzake kwa kuwa walihusika katika kumuombea kwa Mwenyezi Mungu alipokuwa anaumwa.
Alisema kuwa mambo mengi yaliyoelezwa na vyombo vingi vya habari hasa magazeti, yalikuwa yana ukweli ndani yake likiwamo lile la MwanaHalisi lililofungiwa na Serikali Julai 30, mwaka huu.
Aliongeza kuwa kabla ya kutoa tamko hilo, alijiuliza maswali mengi ambayo yalikosa majibu na kati ya mambo aliyojiuliza, ni jukumu la nani atakayehakikisha haki inatendeka katika nchi ya Tanzania.
“Ni jukumu la asasi za kiraia ama mhusika mwenyewe, kuelezea kinagaubaga kilichompata na baada ya kukosa majibu nikaona ni vyema niwaeleze Watanzania hali halisi,” alisema.
Alieleza kuwa kabla ya kutekwa, kupigwa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande, alikuwa na kikao na ofisa aliyetambulishwa kwake kwamba anatokea Ikulu.
Alimtaja mtu huyo kuwa ni Ramadhan Abeid Ighondu, ambaye  alitambulishwa kwake kama ofisa anayetoka Ikulu kwa kuwa alikuwa anakutana naye mara kwa mara kabla ya tukio hilo la kutekwa na kupigwa.
Sehemu ya tamko hilo lilisema Ighondu alitambulishwa kwake na kigogo mmoja ambaye hakumtaja jina akiwa na wenzake ambao ni madaktari.
Dk. Ulimboka alisema walijulishwa kwamba hoja na madai mbalimbali ya madaktari, yatakuwa yanachukuliwa na Ighondu na kuyapeleka serikalini kwa ajili ya kutafuta mwafaka wa kupandishiwa nyongeza za mishahara na madai mengine.
Alisema siku hiyo aliyotekwa, alipigiwa simu na Ighondu kupitia simu ya mkononi namba 0713 760473 na kwamba anamtambua Ighondu kwa sura.
Aliongeza kuwa katika mawasiliano hayo, yeye (Dk. Ulimboka), alikuwa akitumia simu namba 0713 731610 na kwamba anaamini ofisa huyo wa Ikulu yupo hai na yupo tayari na wenzake kutoa ushahidi.
Aidha, Dk. Ulimboka alisema kwa nyakati tofauti, ofisa huyo alitumwa kwake na kumtaka ampatie nyaraka mbalimbali vikiwamo vyeti vya elimu kwa ajili ya uthibitisho wa taaluma yake.
“Mimi Dk. Ulimboka nina haki ya kuishi kwa mujibu wa ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania wenzangu wana haki ya kuulinda uhai wangu,” alisema.
“Je; uhai na maisha yangu vina thamani ndogo kama ya mnyama anayekwenda machinjioni? Je, serikali itakubali lini kuunda tume huru kuchunguza tukio hili?,” Alihoji.
 Aliwataka madaktari kutovunjika moyo katika kudai haki zao za msingi na kwamba yupo pamoja nao katika harakati hizo.
Juni 26, mwaka huu, Dk. Ulimboka alitekwa, akapigwa, akang'olewa kucha kabla ya kuokotwa msitu wa Mabwepande na kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) kwa matibabu.
Hata hivyo, baadaye alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Dk. Ulimboka alirejea nchini Agosti 12, mwaka huu.
Tangu hapo, hajawahi kuzungumza na vyombo vya habari kuhusiana na sakata zima la kutekwa kwake hadi alipotoa tamko hilo jana.




CHANZO: NIPASHE

DIAMOND ATAMANI KUIRUDIA SHULE


WAKATI wasomi wengi wakisisitiza kuhusu vijana kutambua umuhimu wa elimu, msanii wa muziki wa muziki wa kizazi kipya, Nasseb Abdul ‘Diamond’, amedai kuwa anatamani kurudi shule kuendelea na masomo lakini kutokana na shughuli zake za muziki anakosa nafasi.

Akiongea na mwandishi wetu 
alidai kuwa anaamini elimu yake ya kidato cha nne ni ndogo sana na ana changamoto nyingi ili kufikia level za kimataifa, hivyo ana mipango ya kurudi shule lakini akifikilia mambo mengi muziki na ratiba za show huwa anakata tamaa kabisa lakini anaamini atafanya hivyo siku moja ili kutimiza ndoto yake ya kufika mbali zaidi kielimu.

Diamond
alisema kuwa kuna umuhimu wa yeye kwenda shule lakini kwa sasa hafikirii kama anaweza kukaa tena darasani na kumsikiliza mwalimu pengine aende nje kwa ajili ya kusomea muziki huku akiendelea na kazi hiyo hata huko atakapokuwa akisoma.

“Naweza kurudi shule lakini pengine nikasomee muziki na mambo mengine yanayohusu muziki,”
alidai.

Wednesday, October 17, 2012

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda ashikiriwa na polisi

hapa akisisitiza jamboo...!!
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo, imemtia mbaroni Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda Issa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi kanda maalum,Suleiman Kova, alisema kuwa Ponda amekamatwa kutokana na kukabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi dhidi ya Serikali iliyoko madarakani.
Makosa mengine ni uchochezi wa udini kati ya waislamu na wakristo na ndani ya waislamu wenyewe,kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani jijini.
Tuhuma nyingine ni kulazimisha watu kufanya maandamano hasa wanawake na watoto,kumtisha kumuua sheikh Mkuu Mufti Issa Shaaban bin Simba, kujisifia kuingia Makao Makuu ya Jeshi la Polisi bila ruhusa na uvamizi wa kiwanja.
Tuhuma nyingine ni kuingilia uhuru wa Mahakama, umwagaji wa damu, uchomaji wa makanisa zaidi ya nane, uharibifu wa magari, wizi, upotevu wa vifaa vya makanisa. “Sheikh ponda amekuwa mstari wa mbele kupambana na vyombo vya dola na kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kudai watuhumiwa waliokamatwa kwa uvunjaji wa makanisa na kufikishwa Mahakamani waachiwe mara moja kabla ya siku saba”alisema.
Ponda alikamatwa juzi majira ya saa 4:30 usiku akiwa kwenye pikipiki kuelekea katika maficho yake maeneo ya Temeke.
“Juzi usiku sijalala kabisa kuhakikisha oparesheni ya kumkamata inakwenda salama, Ponda ni mjanja sana ila Serikali ina mkono mrefu kabla ajaingia katika maficho yake Temeke,alijaribu kukimbia ili atoroke lakini akakamatwa”alisema.
Kova pia alisema kuwa mnamo Oktoba 12,mwaka huu Ponda aliwaongoza wafuasi wake na kuvamia kiwanja namba 311/2/4 block T chang’ombe mali ya kampuni ya Agritanza kwa madai ya kulikomboa.
“Ponda akiwa na wafuasi wake walivamia kiwanja hicho cha agritanza na kudai kuwa wanakomboa mali za waislamu zilizouzwa na Bakwata,uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kiwanja hicho kina hati miliki namba 93773 iliyotolewa na Wizara ya Ardhi pamoja na mikataba mbalimbali ya kuuziana”alisema
Aidha Kova alisema kuwa uongozi wa Bakwata ulipeleka mashahidi kuthibitisha uhalali wa kiwanja hicho na kusema kuwa watu waliovamia wanakabiliwa na shitaka la kuingia kwa jinai pamoja na uharibifu wa mali.
"Kati ya watu 38 tuliowakamta wanawake ni saba na wanaume ni 31 na tuliwakuta na silaha mbalimbali kama visu,mapanga,sururu na vifaa vya kuvunjia na vya ujenzi,jenereta na kujenga jengo la haraka”alisema Kova.
Aidha Jeshi la Polisi limesema kuwa limemvumilia Ponda kwa muda mrefu na kuwataka watu wanaoandamana kinyume cha taratib kuacha. “Nawasifu sana wakristo ni wavumilivu,wanabusara kwa tukio la mbagala la kuchoma makanisa la sivyo hali ingekuwa ya hatari na hata hivyo Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu haijasajiliwa kisheria”alisema.
Kova amewataka wafuasi wengine wajisalimishe kwani opareheni inaendelea na watawachukulia hatua za kisheria. Pia amewaasa wananchi kutumia akili zao binafsi na kuacha kufuata mkumbo watashughulikiwa.Jeshi la Polisi linatarajia kumfikisha Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika. 

chanzo issamichuzi blog

Tuesday, October 16, 2012

Mintanga aachiwa huru


Akiingia mahakama Kuu....hongera mzeee
hapa akitoka mahakamani......


 Na Hellen Mwango wa Nipashe
Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, jana imemuachia huru aliyekuwa rais wa zamani wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) Alhaji Shabani Mintanga baada upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha ushahidi dhidi ya tuhuma za kula njama na kusafirisha dawa za kulevya kilo 4.8 aina ya heroin ya Sh. milioni 120.
Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Dk. Fauz Twaib baada ya upande wa Jamhuri kuita mashahidi wanne dhidi ya Alhaji Mintanga lakini hata hivyo ushahidi wao umeshindwa kuishawishi mahakama kumuona mshtakiwa kuwa ana kesi ya kujibu.
Jaji Dk. Twaib alisema kuna sababu sita zilizoifanya mahakama bila kuacha shaka imuone mshtakiwa hana kesi ya kujibu.
Alisema sababu ya kwanza; upande wa Jamhuri umeshindwa kupeleka mahakamani kielelezo cha dawa au picha anazodaiwa kusafirisha Alhaji Mintanga kutoka nchini kwenda Mauritius.
Sababu ya pili; katika ushahidi wa Jamhuri na hati ya mashtaka iliyopo mahakamani, hakuna uwiano wa uzito wa dawa za kulevya ambapo hati hiyo inaonyesha ni kilo 4.8 wakati kule nchini Mauritius inaonyesha kilo 6.
Katika sababu ya tatu, jaji alisema ushahidi wa upande wa Jamhuri uliotolewa mahakamani hapo kwa nyakati tofauti ulikuwa unajichanganya kwa sababu shahaidi wa nne Charles Ulaya aliyekuwa mpelelezi wa kesi hiyo, aliiambia mahakama kuwa aliyekuwa anatafutwa ni Mika na sio Alhaji Mintanga.
“Shahidi Ulaya katika ushahidi wake alisema hamjui Alhaji Mintanga na kwamba katika upelelezi wake aliyekuwa anatafutwa kwenye kesi hiyo ni Mika,” alisema Jaji Dk. Twaib wakati akisoma sababu ya nne.
Sababu ya tano, alisema Jamhuri ingeweza kumshtaki Alhaji Mintanga kwa kosa la kula njama hata hivyo imeshindwa kuthibisha kama walikaa mahali gani kula hizo njama.
Katika sababu ya sita, Jaji Dk. Twaib alisema Kamishna wa Dawa za kulevya Kamanda Christopher Shekiondo hakwenda mahakamani kutoa ushahidi na kwamba hata taarifa za uzito wa dawa zilizodaiwa kusafirishwa kwenda Mauritiaus alizipata kwa njia ya simu.
Vielelezo pekee vilivyowasilishwa na upande wa Jamhuri ni simu ya mshtakiwa pamoja na tiketi zilizoonyesha kwamba mshtakiwa alisafiri kwenda nchini Mauritius ambavyo haviwezi kuishawishi kwamba alihusika na biashara hiyo ya dawa za kulevya.
“Kutokana na sababu hizo mahakama bila kuacha shaka imeona kwa hoja zilitolewa, mshtakiwa hakuhusika na suala hilo bali ni Mika na upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake hivyo hana kesi ya kujibu na yuko huru,” alisema Jaji Dk. Twaib.
Katika kesi ya msingi, Mintanga alikuwa anadaiwa kuwa Juni 3, mwaka 2008 eneo lisilofahamika akiwa na wengine sita ambao hawajakamatwa, walikula njama ya kutenda kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin kutoka nchini kwenda Mauritius.
Katika shitaka la pili, Mintanga alidaiwa kuwa Juni 10, mwaka 2008 akiwa na wengine sita ambao hawajakamatwa walisafirisha dawa za kulevya kilogramu 4.8 kutoka nchini kwenda Mauritius.
Alhaji Mintanga aliyekuwa amevalia suti ya 'Kaunda' ya rangi nyeusi na makubadhi ya rangi ya kahawia, baada ya kuambiwa kuwa hana kesi ya kujibu na yuko huru alionekana kama aliyepigwa ganzi pale kizimbani alipokuwa amesimama na baada ya muda mfupi aliachia tabasamu huku wanaodaiwa kuwa wanafamilia yake walionekana wakilipuka kwa furaha.
Watu wake wakiwamo watoto wake, walimkumbatia Mintanga kabla ya kuondoka naye katika viunga vya mahakama hiyo.
Mawakili wa utetezi, Jerome Msemwa na Yassin Membea, walizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti.
Msemwa alisema mahakama imeona kwamba Mintanga hakuhusika na tuhuma zilizokuwa zinamkabili na kwamba imetoa haki kwa pande zote mbili.
Wakili Membea alisema haki imetendeka kwa mteja wake pamoja na kusota mahabusu kwa zaidi ya miaka minne lakini mwisho mahakama imeona ukweli.
Mapema mwaka 2008, Mintanga alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akikabiliwa na kesi hiyo ambapo kutokana na mashtaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana kisheria alikuwa mahabusu hadi jana mahakama ilipomuona hana kesi ya kujibu.



CHANZO: NIPASHE

Wema Sepetu na Aunt Ezekiel waomba radhi kwa kukaa uchi


Hapa ni Idara ya Habari (MAELEZO) ambapo Wema na mwenzake Aunt Ezekiel walijitokeza mbele ya waaandishi wa habari na kuomba msamaha kufuatia mavazi yao ya kuwaacha nusu uchi.

Na Dina Ismail
LICHA ya kuomba radhi kutokana na kuvaa nusu uchi katika matamasha ya Fiesta mwaka huu, wasanii wa filamu nchini, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wamesema wataendelea kuvaa nguo hizo.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam jana, wasanii hao walielezea kujutia tukio hilo ambalo hawakulitarajia kutokea.
Walisema wao kama wasanii wa filamu, wanalazimika kuvaa mavazi kulingana na wakati na tukio husika, ndiyo maana walivaa mavazi yale, lakini tatizo lilikuwa ni urefu wa jukwaa.
Mmoja ya wasanii hao, Aunt Ezekiel alisema kwamba kilichotokea ni bahati mbaya kwani hawana uzoefu na majukwaa ya muziki na matokeo yake kuwa hivyo.
“Yale mavazi huwa tunayavaa kila mara, lakini kwa bahati mbaya jukwaa lilikuwa refu na ndiyo maana tulionekana hivyo…tunaomba msamaha na tumeshajifunza.
Tunapenda kuchukua fursa hii kuiomba radhi jamii yote, ndugu jamaa na marafiki kwa tukio hili ambalo hatukulitarajia,” alisema Aunt Ezekiel.
Akizungumzia tabia yake ya kupiga picha za utupu, Aunt alikana na kudai kwamba; “Hizo picha wanazodai ni za utupu si kweli, bali nilipigwa mgongo kwa ajili ya jalada la filamu ya Young Millionea.
Hizo nguo fupi sijaanza kuvaa jana wala juzi, hivyo kwa tukio lile ilitokea bahati mbaya na kuanzia sasa nitakuwa makini na vitu kama hivyo,” alisema Aunt Ezekiel.
Naye Wema, pamoja nakuomba radhi aliitaka jamii kutowachukulia vibaya kutokana na mavazi hayo, kwani mara nyingi wanavaa kulingana na wakati na mahali.
Alisema baada ya dosari hizo kujitokeza, aliamua kuanza kuvaa suruali za jeans au kaptula ili kuepukana na kitendo hicho.Kwa upande wake Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Wilson Makubi alisema baada ya tukio la wasanii hao, waliwaita na kuzungumza nao na mwisho wa siku walikiri makosa na wakaomba radhi.
HIZI NDIZO PICHA ZILIZOWAPONZA:








huyu ni Wema Sepetu

Sunday, October 14, 2012

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKANISA YALIYOHARIBIWA KATIKA VURUGU ZA WAISLAMU MBAGALA.....

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es salaam....
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Askofu Msaidizi wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Dayosisi ya Dar es salaam na Pwani Mkosimonga  uharibifu mkubwa uliofanywa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Bw. M Mkosimonga uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa baadhi ya waumini wa  Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam kufuatia uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia uharibifu mkubwa uliofanywa katika kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye magari yaliyokuwa yameegeshwa ndani ya kanisa la Pentekoste la Mbagala.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Bw. Mkosimonga  uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo.

WINGU ZITO:Utata wagubika kifo cha RPC Barlow

Marehemu Kamanda Barlow enzi za uhai wake.


 Mwanamke aliyekuwa naye ashikiliwa na polisi
Utata umegubika mauaji ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi usiku wa kuamkia jana.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa Barlow, aliuawa maeneo ya Kitangiri katika barabara inayoelekea Bwiru, jirani na hoteli ya Tai Five jijini hapa. Alisema mauaji hayo yalifanyika kati ya saa 7 na saa 8 usiku, wakati Barlow akimsindikiza mwanamke aliyejulikana kama Doroth Moses. Inasemekana kuwa wote wawili, walikuwa wametoka kuhudhuria kikao cha maandalizi ya harusi ya mtoto wa dada wa Barlow, kilichofanyika hoteli ya Florida.
Hata hivyo, taarifa zisizo rasmi kutoka mitandao ya kijamii kuhusu utata wa mauaji hayo, zinaeleza kuwa Barlow na mwanamke huyo walikuwa wanatoka katika hoteli inayotajwa kwa jina la La-Kairo. Akifafanua, Ndikilo alisema Barlow alikuwa akiendesha gari yake binafsi aina ya Toyota Hilux- double cabin na kwamba alikuwa akimsindikiza mwanamke huyo kwenda nyumbani kwake.
Mwanamke huyo ambaye anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi, ni mwalimu katika Shule ya Msingi Nyamagana. Alisema wakati wakikaribia eneo la Kitangiri anakoishi mwanamke huyo, waliwaona watu wawili wakiwa wamevaa mavazi maalum (jackets) yanayovaliwa na wananchi wanaoshiriki ulinzi shirikishi unaofahamika pia kama polisi jamii. Kwa mujibu wa Ndikilo, baada ya kuwaona watu hao ambao waliwamulika kwa tochi, Doroth alimuuliza Barlow iwapo anawafahamu, naye alimjibu kuwa watakuwa ni polisi jamii.
Hata hivyo, Ndikilo alisema baada ya Barlow kusimamisha gari pembeni, mkabala na nyumba anayoishi mwanamke huyo, watu hao wawili waliwasogelea huku wakionyesha kukerwa na mwanga wa taa za gari. Alisema watu hao walimhoji Barlow kwa nini anawamulika kwa taa za gari, lakini wakati akijaribu kutoa ufafanuzi kwamba yeye ni RPC, ghafla walitokea watu wengine wapatao watatu, walisimama kuzunguka gari la Kamanda huyo.
Baada ya kuona hali hiyo, huku akijaribu kuwauliza iwapo hawamfahamu kuwa yeye ndiye RPC na kutoa radio call (simu ya upepo) ili kufanya mawasiliano na polisi wa doria. “Ghafla mmoja wa watu hao alitoa bastola na kumfyatulia risasi ambayo iliingilia shingoni na kutokea upande wa pili wa bega,” alisema Ndikilo.
Alisema baada ya tukio hilo, watu hao walichukua vitu kadhaa ikiwemo bastola, simu na radio call alivyokuwa navyo Barlow na kutoweka kusikojulikana. “Kimsingi mazingira ya mauaji yenyewe bado yana utata, lakini Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi tunafanya kazi ya kuchunguza ili kuujua ukweli,”alisema.
Kwa mujibu wa Ndikilo, baada ya kufyatuliwa risasi inaaminika Barlow alikufa papo hapo kutokana na kuvuja damu nyingi na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando ukisubiri taratibu za mazishi. Alisema kutokana na mazingira hayo ya utata ya mauaji, Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamke aliyekuwa naye kwa mahoajiano zaidi. Taarifa za awali zilidai kwamba mwanamke huyo anayesadikiwa kuwa ni mjane, ni dada yake Barlow.
Lakini baadaye jana, Mkuu wa mkoa wa Mwanza alikanusha taarifa hizo na kusisitiza kuwa ni mtu ambaye alikuwa amempa lifti wakati wakitoka katika kikao cha harusi. Kufuatia mauaji hayo Ndikilo alisema kuwa Polisi Makao Makuu, limemtuma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba kuongeza nguvu ya uchunguzi wa tukio hilo.
Nyumbani kwa Doroth, kijana Kenrogers Edwin aliyejitambulisha kama mtoto wa kaka yake wa mwanamke huyo, alisema kabla ya tukio hilo, shangazi yake (Doroth) alipiga simu ili wamfungulie geti. Alisema kwamba wakati akifungua geti, aliona gari likiwa limeegesha huku watu wawili wakiwa upande wa abiria na wengine watatu wakiwa upande wa dereva na kisha alisikia mlio wa risasi na baadaye watu hao walitimua mbio baada ya kuona pikipiki inakuja nyuma yao.
Baadhi ya wananchi waliozungumzia mauaji hayo walielezea kushangazwa kwao na hatua ya Barlow kutembea usiku bila mlinzi wake (bodyguard) ambaye kwa kiwango kikubwa angeweza kusaidia kumuepusha na kifo.
IGP MWEMA AMTUMA DCI KWA UPEPELEZI
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Said Mwema, katika taarifa aliyoitoa jana jijini Dar es Salaam, alisema ameshamtuma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Robert Manumba, mkoani humo kuimarisha ulinzi na upepelezi wa tukio hilo.
Aidha, Mwema amewaomba wananchi kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo, utakaowezesha kuwabaini wahalifu hao. Akielezea kuhusu mauaji hayo, Mwema alisema, wakati huo Barlow alikuwa akitokea kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake eneo la Florida hoteli Mwanza mjini. Alisema alikuwa ameongozana na ndugu yake wakitoka kwenye kikao hicho. Alisema tukio hilo limewashtua na kuwahuzunisha na kwamba wakati uchunguzi ukiendelea, wataendelea kutoa taarifa kadri wanakavyozipata. ….
MAKAMANDA WA MIKOA WATOA KILIO
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa mbalimbali nchini, wamesema kuwa wamempoteza kiongozi mwenye uzoefu wa muda mrefu kazini na aliyekuwa mchapakazi katika jeshi hilo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema ukomavu wa kazi ndio uliosababisha kamanda huyo kupelekwa katika mkoa ambao ni miongoni mwa mikoa migumu nchini.
Alisema enzi za uhai wake, alikuwa akiwaelimisha wenzake ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kwamba alikuwa mwepesi kuwarekebisha wale wanaoenda kinyume na kazi. Kenyela alisema kwa upande wake atamkumbuka kwa sababu ndiye aliyempokea wakati akianza kazi hiyo na alikuwa akiishi naye kwenye kambi za maofisa huko Tabata.
“Wito wangu kwa wananchi walaani vitendo vya mauaji ya viongozi kwa sababu kumpoteza kiongozi ni gharama kubwa katika nchi hasa ukiangalia muda uliotumika kumuandaa hadi amefikia hatua hii,” alisema. MOROGORO Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema kuwa, ameguswa na msiba huo wa ghafla na kueleza kuwa, atamkumbuka daima kwa kuwa alikuwa akifanya kazi yake kwa kujiamini.
“Tumempoteza jembe kwa sababu alikuwa mzoefu kwenye kazi na asiye mchoyo pindi umwombapo ushauri, kwa wale wachanga kwenye kazi walikuwa wakimtumia sana ili waweze kuifanya kazi yao kwa ufanisi,” alisema. MTWARA Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Maria Nzuki amewataka wenzake, kuyaenzi na kuyaendeleza yale mazuri aliyokuwa akiyafanya Barlow enzi za uhai wake.
TANGA
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Constantine Massawe, ameeleza kusitikitishwa na mauaji ya Barlow na kuwataka watumishi wa jeshi hilo kuwa wavumilivu wakati wakisubiri uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea ili hatua madhubuti ziweze kuchukuliwa.
“Kwa sababu kuna kikosi maalum ambacho kimeenda kufanya uchunguzi wa mauaji hayo basi nawasihi wenzangu tuendelee kuwa wavumilivu mpaka hapo upelelezi utakapokamilika na kujua hatma yake au hatua gani za kuchukua, “alisema. Alimwelezea marehemu alikuwa mtu mchapa kazi, mvumilivu na aliyeipenda kazi yake na kwamba ameacha pengo kubwa katika nafasi hiyo.
KILIMANJARO
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, amesema kifo cha Barlow ni cha kawaida ambacho kinaweza kumkuta mtu yeyote na haipaswi kujiuliza maswali mengi. Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Boaz alisema kifo hicho kinaweza kikamkuta hata rais wa nchi yoyote ambaye analindwa na walinzi chungu nzima.
“Kifo chake kinatupa majonzi sisi makamanda wenzake,lakini kikubwa kilichobaki ni kumuombea kwa Mungu na kuacha uchunguzi kufanyika,” alisema. Aliongeza, “kwa sasa ni mapema mno kuzungumza chochote,lakini ninachoweza kusema ni kuwa kifo chake kimenistua na ni kifo ambacho kinaweza kikamtokea mtu yeyote.”
Aidha kwa upande wao baadhi ya wananchi mkoani Kilimanjaro wameeleza kushangazwa na kiongozi mkubwa wa Polisi kuuawa na majambazi. Bariki Sanga mkazi wa Kilimanjaro aliliambia NIPASHE Jumapili kuwa,ni jambo la kujifunza kwa kila kiongozi na kila raia kuwa mlinzi wa mali zake mwenyewe.
MBEYA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko kifo hicho. Alisema ingawa hapaswi kulitolea tamko kwa kuwa linashugulikiwa na Polisi Makao Makuu, kifo hicho ni changamoto kubwa kwa jeshi hilo ambalo sasa linatakiwa kujipanga na kufanya kazi kwa bidii. Alisema kuwa yeye binafsi anamfahamu vizuri Barlow kwa kuwa alimpokea vizuri wakati yeye (Diwani) alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kuwa Kamanda wa Polisi wa mkoani Shinyanga.
Alisema Barlow pia alikuwa ni mwenyekiti wa Makamanda wa Polisi wa Kanda ya Ziwa ambaye alikuwa akiwaunganisha vizuri na kupunguza kabisa matukio ya uhalifu kwenye kanda hiyo. Aliongeza kuwa kwa vyovyote ambavyo uchunguzi utakavyobaini, kifo cha Barlow ni pigo kwa Polisi, kwa kuwa mchano wake ulikuwa bado unahitajika sana ndani ya jeshi hilo.
DODOMA
Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Stephen Zelothe, ambaye Barlow alikuwa mwanafunzi wake kikazi, alisema ni masikitiko makubwa kutokea kwa tukio hilo. “Ni masikitiko makubwa kutokea kwa jambo hili…siwezi kusema lolote tuache kwanza mambo ya kidunia (mazishi) yapite,”alisema Zelothe kwa masikitiko makubwa alipoulizwa nini kifanyike

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Thursday, October 11, 2012

RUDI yapata tuzo ya ubora kimataifa


Mkurugenzi Mtendaji wa RUDI, Abel Lyimo kulia akiwa na mwenyekiti wa bodi ya RUDI wakiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) tuzo hizo.

 Viongozi wa RUDI waliokuwa wakiongea na waandishi wa habari leo.

Na Carren-Flora Mgonja
TAASISI ya Maendeleo Mijini na Vijijini (RUDI) imepata tuzo ya ubora wa kazi za kuhamasisha
kilimo na mafanikio katika mapinduzi ya kijani kwa wakulima wadogo nchini.
RUDI ilipokea tuzo hiyo hivi karibuni kutoka kwa aliyekua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Koffi Annani mjini Arusha wakati wa mkutano wa kimataifa wa
Akizungumzia tuzo hiyo Mwenyekiti Mtendaji wa RUDI Abel Lyimo alisema tuzo hiyo imetolewa na
Shirika la Ubia wa Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA) na kutambuliwa kuwa taasisi binafsi
lililohamasisha mapinduzi ya kijani Tanzania .
 “Tinashughulika zaidi na wakulima wadogo tukiwahamasisha walime mazao ya nafaka hasa
mpunga… lengo ni kuwainua wakulima na kukifanya kilimo kiwe kweli uti wa mgongo wa uchumi wa
Tanzania .
“…Ilikua furaha kwetu kwa sababu ni RUDI pekee ndiyo iliyopokea tuzo hii kutoka Tanzania
mbele ya rais Jakaya Kikwete, tukaona kwamba mchango wetu unatambuliwa ndiyo maana leo
tumeamua kuzungumza na waandishi wa habari ili taifa litufahamu zaidi,” alisema Lyimo.
Alisema kazi kubwa inatofanywa na taasisi hiyo iliyoanza mwaka 2007 ni kuanzisha na
kuimarisha vikundi vya wakulima kisha kuviunganisha na asasi za fedha na masoko.
Kwa mujibu wa Lyimo tangu kuanzishwa kwa RUDI iliyowezeshwa na Asasi NORGES yenye maskani
yake nchini Norway wamewafikia wakulima zaidi ya 60,000 katika mikoa nane ya Tanzania Bara.
Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Mbeya, Morogoro, Iringa, Dodoma , Singida, Shinyanga, Geita na
Njombe huku akisisitiza kwamba kabla ya kuwafikia wakulima huzungumza na serikali ya wilaya
husika kufahamu vipaumbele vyao.
“Wakulima tunaofanyakazi nao tumewaunganisha na makampuni ya wauza pembejeo binfasi pia
wamefaidika na mfumo wa uhifadhi wa mazao kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani…zaidi ya sh
bilioni moja zimetumika,” alisema na kuongeza kwamba lengo ni kuwafikia wakuliam 100,000
baada ya miaka mitano.

Wednesday, October 10, 2012

Jokate Mwegelo 'anatisha' azindua Kampuni yake ya Kidoti




 full kujiamini...safi mama...umethubutu na umeweza...


katika wadada wanaojiamini mjini si mwingine ni Sinta....daaa..namkubali ile mbayaaa alipoingia yeye tuuuu shughuli ilinogajeee...coz alichelewa alisema alikuwa kwenye kikao, ila alijitahidi kadiri ya uwezo wake na kuwakilisha...upoo juu mama, hapa akiwa na warembo wa Kidoti waliovaa baadhi ya nywele zake.


Carren Mgonja
MWANAMITINDO anayetamba kwa sasa hapa nchini Jokate Mwegelo ‘Jokete’ jana amefungua rasmi kampuni yake yenye Chapa ya Kidoti inayojihusisha na masuala mbalimbali ya Urembo.
Akizungumza na jijini Dar es Salaam Jokate alisema, ameamua kuanzisha kampuni hiyo ambayo kwa sasa imeanza na uuzaji wa Nywele na baadae ataendelea na mambo mengine mbalimbali ya urembo ikiwemo nguo na vifuasi vya urembo na vipodozi.
Alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 2011 na kuzinduliwa rasmi jana, kwa nia ya kubadilisha mtazamo mzima wa tasnia ya mitindo na kusema kuwa Chapa hii itasheheni bidhaa mbalimbali zikiwemo nywele za sanisi.


Katika nywele hizi tuna staili nane tofauti kwa kuanzia ambazo tumezipa majina ya reysa, dessy, fania, Whitney curls, jokate, Myra, Selita na nayomi.
Napenda kusema what is fashion without hair? Hizi nywele mabibi na mabwana zimefanyiwa utafiti kwa takribani mwaka mzima ili kuhakikisha tunasaidia kuboresha mitazamo ya nywele za kuongezea kwa wasichana, wadada mpaka akina mama. Ni nywele safi zenye ubora wa hali ya juu, hazifungamani, ziko katika mawimbi, rangi na style za kisasa, ni nyepesi, rahisi kusukia, zinadumu kwa muda mrefu na muhimu kuliko yote zinapatikana kwa bei nafuu sana. Sasa mwanamke anaweza kupendeza kichwani kwa style tofauti bila ya kuharibu sana bajeti yake ya mwezi ama mwaka na kila paketi ina ujazo wa kutosha kichwa kizima. Ni bidhaa inayomfaa mwanamke wa kisasa.


Utengenezwaji wa nywele hizi nimezisimamia mwenyewe nikiongozwa na watengenezaji wangu, kama binti ninayejiamini na kupenda kupendeza, ninayetazamwa na watanzania kwa uwigni wao na wengi kuulizia style mbalimbali ninazofanya ni nimepata faraja kubwa sana kuweza kutengeza nywele hizi kwa ajili ya kina dada wenzangu, wasichana na akina mama.


Nywele hizi zinakuhamasisha wewe u-ainishe urembo wako, ujitambue kupitia nywele hizi hizi vile vile tunasema katika packeti ya nywele mmoja unaweza kupata staili kibao yaani nywele mmoja staili kibao. Tumezoa kuona weaving kwa mfano zikitumiwa kusukiwa tu lakini Leo hii tunakwambia kupitia hio nywele unaweza pia ukapata staili za kubana na hivyo kubadilisha muonekano wako Mara nyingi uwezavyo. Mambo ya Kidoti hayo

“Nywele hizi zinamfaa mtu yoyote,na ninaimani kubwa wadau wangu watazipenda kwa kuwa nywele moja mitindo tofauti na leo zinaanza kutoka na katika saluni mbalimbali zitakuwepo”alisema Jokate na kuongeza kuwa nguo za Kidoti zitatambulishwa rasmi katika soko mwakani zikifuatiwa na vifuasi vya urembo pamoja na vipodozi.
“Msingi wa ubunifu wangu ni mchanganyiko wa kipekee wa kiini cha utamaduni wa Kiafrika pamoja na mitindo ya kisasa ulimwenguni kwa ajili ya wanawake na wanaume wa kisasa. Nachukua muda kusoma mienendo ya soko na kujua wateja wangu wanataka nini katika maisha yao na hivyo kutumia ubunifu wangu katika mitindo kuwasaidia kuyafikia malengo yao,” alimalizia Jokate.
Aliongeza kuwa harakati ya Kidoti inaendeshwa na timu ya vijana wabunifu na pamoja na kwamba shughuli za Kidoti zinaendeshwa kutoka Dar es Salaam, chapa hii ni ya kiulimwengu zaidi na kuwaomba wadau mbalimbali kumpa sapoti juu ya bidhaa hiyo.