Monday, January 14, 2013

KAMANDA KOVA AKUTANA NA WANAFUNZI WA VYUO VYA IFM NA MWALIMU NYERERE KUZUNGUMZIA MATATIZO YAO

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya hatua zitakazochukuuliwa baada ya kupata taarifa hizo ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wote kwapamoja kwenda Kigamboni kufuatilia tukio hilo kwa pamoja.

Tunaimba! Tunavuka bure Tunavuka bure kwenye Pantoni.

Pamoja na kutakiwa kupungua hapa wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho. Picha zote na Raha za Pwani, hii ni sehemu ya kwanza tutawaletea sehemu ya pili ya tukio hili ambalo hadi hivi sasa filamu inaendelea hapa feli na ikielekea Kigamboni.
Wanafunzi wa Chuop Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia leo majira ya saa nne nanusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na kubakwa hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.
Ulinzi uliimarishwa nnje ya jengo la Wizara ya Mambo ya ndani kufuatia kadhia hiyo ya wanafunzi. Tembelea Mtaa kwa Mtaa Blog kwa picha zaidi

TAMASHA LA WASANII KUFANYIKA DAR LIVE JANUARI 26

 
Mwakilishi kutoka kampuni ya Vannedrick Tanzania Ltd, ambao ni moja ya waandaaji wa tamasha hilo, Dino Debwe, akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
 
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, naye akiongea machache wakati wa mkutano huo na wanahabari.
 
Baadhi ya wasanii wa filamu nchini kutoka kushoto ni Dk Cheni, Snura, Shamsa Ford na Shilole wakifuatilia mkutano huo.
 
 Sehemu ya wanahabari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Lamada Ilala jijini Dar leo.
Kitalima Gerald na Khatimu Naheka
SHIRIKISHO la Filamu Tanzania (TAFF), limeandaa Tamasha la Wasanii litakalofanyika Januari 26, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, rais wa shirikisho hilo, Simon Mwakifwamba, alisema tamasha hilo wamelipa jina la Siku ya Ma-Star wa Filamu Tanzania, likiwa na lengo la kupata fedha za kujiendesha.
Mwakifwamba alisema wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kukosa ofisi na vitendea kazi muhimu ndani ya ofisi kulingana na hadhi, hivyo wanakadiria kupata shilingi milioni 60 katika tamasha hilo.
Alisema kwa kutambua hilo wameliandaa tamasha hilo wakiamini kupata wadau wengi wapenzi wa kazi zao.
Kiingilio kwa watoto kitakuwa Sh 2,000, wakubwa 7,000 na VIP 15,000. Tamasha litaanza saa 4:00 asubuhi.
“TAFF tumeandaa Tamasha la Wasanii tulilolipa jina la Siku ya Ma-Star wa Filamu Tanzania, litakalofanyika Januari 26, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Dar Live.
“Lengo ni kupata fedha kwa ajili ya kukabiliana na changamoto zinazotukabili, ikiwemo kuwa na ofisi kulingana na hadhi yetu na vitendea kazi muhimu ndani ya ofisi, tumekadiria kupata shilingi milioni 60 katika tamasha hilo linalotarajiwa kuanza saa nne asubuhi,” alisema Mwakifwamba.
by mrisho's blog

Thursday, January 10, 2013

MH TEMBA:WAMENILIZA TENA VIFAA VYA GARI YANGU


 Baada ya kukemea uwizi wa vifaa vya magari na kufanikiwa kukamata baadhi ya wezi wanaohusika na matukio hayo ya uibaji wa vifaa vya magari,sasa leo Mh.Temba ameibiwa tena vifaa vya gari yake na vifaa hivyo ni Power Window,Dashbody,Side mirrow na vitu vingine vyenye gharama kubwa.

Baada ya kuibiwa vifaa hivyo aliweza kutangaza ila hakufanikiwa kupata hata kimoja ila amesharipoti katika kituo cha Polisi,sasa
 Kupitia katika mtandao wa twitter wasanii wanafunguka juu ya uibaji wa vifaa hivyo vya magari wamechoshwa.


http://djfetty.blogspot.com

Tuesday, January 8, 2013

Dk. Slaa: Gesi ni mali ya wananchi


Dk Salaa
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema suala la gesi asili linaleta mvutano kwa sababu ya maslahi ya watu wachache.
Watu wanaoendekeza mgogoro katika sakata hilo ni wale waliofilisika kifikra, hawajui Katiba na hawajui kuwa wananchi ndio walinzi wa kwanza wa rasilimali zao.
Alisema kuwa wanaokuja na hoja ya kusema ni siasa, wanakurupuka kwani wao kama wanasiasa ni lazima kupiga kelele kupinga dhuluma inayotaka kufanywa na serikali dhidi ya wananchi hao.
Akizungumza na Tanzania Daima juzi, Dk. Slaa, alisema Katiba ya nchi pamoja na udhaifu iliyonao, imeainisha vema misingi ya kusimamia rasilimali za taifa kwa usawa bila ubaguzi wala dhuluma.
Alisema kuwa katika suala hilo hawatafuti umaarufu wowote wa kisiasa, na hivyo kuhoji ni nani anaweza kutafuta umaarufu katika shida za watu?
Dk. Slaa aliongeza kuwa Mtwara ni sehemu tu ya Tanzania, hivyo wananchi wa huko na Lindi wana haki ya kunufaika na rasilimali iliyopatikana kwao.
“Serikali inasisitiza kujenga mitambo Kinyerezi kwa kuwa wanataka kuleta gesi hiyo Dar es Salaam ili kunufaika wao kwanza, jambo ambalo ni la kiubaguzi,” alisema.
Kwa mujibu wa katibu huyo, serikali ingekuwa wazi kwa kuwaambia wananchi inalinda Katiba ipi; maana iliyopo inawapa wananchi haki ya kulinda rasilimali zao na kunufaika nazo.
Alifafanua kuwa mkazo unaopaswa kuwepo kwa maendeleo ya taifa, unazungumzia kuondoa maadui watatu yaani ujinga, maradhi na umaskini.
“Wananchi wa Mtwara ni maskini, mkoa wao umetelekezwa muda mrefu, wamekopwa korosho yao, sasa wamepata gesi na wanayo haki ya kudai wanufaike nayo ili nao wapate viwanda, shule na hospitali nzuri,” alisema.
Dk. Slaa alisema mikoa hiyo haijawahi kuwa na hospitali ya rufaa, hivyo wanaionya serikali isiendeshe shughuli za uchumi kwa maslahi ya watu wachache.
Alisisitiza kuwa hakuna sababu za kutokuwekeza mitambo ya gesi Mtwara na Lindi ili isaidie ukuaji wa maeneo hayo kiuchumi na kwamba jambo hilo wala halina siasa.
Alisema ni jukumu la kila mwananchi kulinda utajiri wa taifa lake kwani wao ndio wamiliki, hivyo hawapaswi kutegemea hisani ya serikali na badala yake serikali inapaswa kuwajibuka kwao.
Kauli hiyo ya Dk. Slaa inakuja siku chache baada ya Waziri wa Nishati na Madini kuwabeza wananchi wa Mtwara walioandamana wakiongozana na baadhi ya wanasiasa kupinga usafirishwaji wa gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
Desemba 27, wananchi wa Mtwara waliandamana kupinga hatua ya serikali kutaka wasafirishe gesi hadi Dar es Salam na kuwaacha wao wakiwa hawana kitu.
Januari 2, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, akizungumza na waandishi wa habari alipinga hatua hiyo ya wananchi na kusema jambo hilo limevamiwa na wanasiasa.
“Hiyo gesi inayowafanya wanasiasa wawashawishi wakazi wa Mtwara kuandamana haiko Mtwara wala Lindi, bali iko katika mipaka ya Tanzania ndani ya kina kirefu cha bahari na kwa hilo kila Mtanzania ana haki ya kutumia,” alisema.
Waziri Muhongo alisema ni jambo la kusikitisha kuona wakazi wa Mtwara wakiandamana kwa ajili ya gesi wakati walipa kodi wa Tanzania hawajaandamana kwa ajili ya rasilimali zinazotoka maeneo mengine kwenda kutumika Mtwara.
Alikwenda mbali na kulaumu kile alichokiita wanasiasa kujiingiza katika sakata hilo na kuwahimiza wananchi waandamane.

Monday, January 7, 2013

SIJATAPELI MOMBASA - PROFESA JAY

Prof Jay amethibitisha kuwa taarifa zinazo samba kwamba ametapeli Promoter Mombasa sio za kweli. Jay amesema alikubaliana na Promoter Eljah wa mjini Mombasa kuhusu show 2 ambazo zilikuwa tarehe 24 December iliyofanyika Jambori na Tarehe 25 Iliyofanyika Kwetu Beach. Show zote  Prof Jay alizifanya kama ilivyo pangwa ila Ilipofika muda wa kulipwa sasa hapo ndio tatizo lilipoanza.
Prof Jay


Prof Jay amekaririwa na sammisago.com akisema Promoter huyo alishindwa kumlipa pesa alizo takiwa kumlipa na kwa sasa Bado promoter huyo anadaiwa na Prof Jay Shilingi laki moja na Elfu Ishirini za Kenya [120,000] ambazo ni 2.201,215  Za Tz. Kila akipigiwa simu alikuwa anasema Jay nitakulipa baadae na halipi. Prof Jay amesema Promoter huyo hakulipa hata nauli yake ya kurudi Tanzania na Ilibidi Prof Jay aingie mfukoni na kulipia watu wake nauli na mambo mengine. Hizi ndio sababu zilizo mfanya jay asifanye show ya Tarehe 31 December iliyopangwa kufanyika  Jamboree.

Fahamu kuwa Mkataba wa makubaliano yao upo na promoter huyo aliandika pesa zote na makubaliano yao.Jay amesema anashangazwa sana na taarifa hizi kwani yeye ndiye anadai na sio kudaiwa chochote ndio maana promoter huyo ameongea hivyo kwenye vyombo vya habari ili kulinda jina lake. Pia alimaliza kwa kusema kabla taarifa kama hizi kusamba lazima waandishi wafanye uchunguzi kwani wanaweza kufanya watu kufikiriwa vibaya na jamii inayo wazunguka.




Hii Ndio Ilikuwa Post Ya Profesa Jay Kabla Ya Show Jamboree Mombasa.
Kwa hisani ya http://www.sammisago.com




"NAWAPENDA MARAFIKI WA KIUME MAANA HAWANA MAJUNGU KAMA WANAWAKE".....QUEEN DARLEEN


STAA anayefanya poa na ngoma ‘Kokoro’, Queen Darleen, ameuambia mtandao huu  kuwa anajisikia raha kuwa na marafiki wengi wa kiume kuliko wanawake, huku akiamini kuwa tabia za baadhi ya wanawake ndizo zinazomfanya awe hivyo.

Msanii huyo ni mmoja ya wanawake wenye staili za kipekee kabisa kwenye game ingawa ndani ya mwaka huu amekuja kivingine kabisa baada ya kuwa kimya kwa muda na kuteka mashabiki kupitia kibao cha ‘Maneno Maneno’.


Kauli ya msanii huyo imekuja baada ya kuzungumza na mwandishi wetu alietaka kujua ni kundi gani la watu ambao hupenda kuwa nao karibu sana na kubandilishana mawazo ndipo yenye maana, ndipo alipofunguka kuwa mara nyingi huwa karibu na wanaume na si wanawake.


Alisema kuwa karibu na wanaume haimanishi kwamba ni mabwana zake hapana bali anaona ni watu ambao anaendana nao ingawa tabia zake si za kiume kama baadhi ya watu wanavyopenda kudhani kutoka na staili zake au aina ya kazi anazofanya.


“Kuna watu wanajua mimi nina tabia za kiume hiyo inawezekana kwa sababu wao ndo wanaosema, napenda sana kuwa na watu ambao tutafanya mambo ya maendeleo na si kuzungumza mapenzi na upuuzi muda wote hiyo ndo sababu kubwa inayonifanya nijiweke sana kwa wanaume,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa anahisi akijiweka karibu sana na wanawake hakuna kitu kikubwa watakachokuwa wanazungumza zaidi ya majungu na mapenzi, ingawa hata wanaume baadhi yao wako hivyo ila si kama wanawake ambao hupoteza mda mwingi kujadili ujinga.

Friday, January 4, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAMIA KUZIMA MWILI WA SAJUKI


 
.

.

.

Hawa ni miongoni mwa waliokua wanasubiri kuupokea mwili, kwa mbali anaonekana Profesa Jay.

.

Mchekeshaji Masanja Mkandamizaji na Mwimbaji Linex ni miogoni mwa wasanii waliohudhuria, wengine ni pamoja na Mwana Fa, Profesa J, Mzee Kitime na King Kikii.

.

Mwana Fa na Profesa J.

King Kikii Mwana Fa na Profesa J.

Msanii Z Anto akiswali juu ya kaburi la Marehemu Sajuki.

Hapa ndipo alipozikwa Marehemu Sajuki.

Zola D kwa mbali.

Hili gazeti walilokua wanasoma kulikua na habari kuhusu kifo cha Sajuki.

.

.

Mwili ulipokua unaingizwa.

picha za juu kwa hisani ya millardayo.com

Rais Jakaya Kkwete akiendelea na shughuli za mazishi (picha kwa hisani ya issamichuzi.blogspot.com)

mwili wa marehemu SAJUKI ukiingizwa eneo la makaburi(picha kwa hisani ya issamichuzi.blogspot.com)
Rai

SAJUKI ALISEMA HAWEZI KUISHI TENA DUNIANI

Millard na Dinno.
Mwigizaji Dinno alikua rafiki mkubwa sana wa Marehemu Sajuki na ndio alikua analala hospitali na Sajuki pale Muhimbili.
Ameongea Exclusive na AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kutoa maneno ya mwisho ambayo aliyasikia kutoka kwa Sajuki akimzungumzia mke wake ambae ni Wastara.
Kwa haraka haraka mwigizaji Wastara amesifiwa sana na watu mbalimbali kwa moyo wake wa ushujaa wa ukweli wa upendo kwa Sajuki japo walipitia matatizo makubwa na mengi kwenye maisha yao.
Masanja Mkandamizaji na Arnold Kayanda ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania waliopaza sauti zao kupitia mitandao ya kijamii kumsifia Wastara kwa moyo wa upendo.
Tukirudi kwa Dinno, namkariri akisema “tulipokuwa Arusha sisi watatu tu Sajuki alionyesha ishara ya kukata tamaa, siku moja tulikua hotelini usiku kama saa tisa hivi Wastara alikuja kuniamsha kwenye chumba changu nikaenda kwa Sajuki, alikua anaumwa sana akamwambia Wastara naomba mpigie mama niongee nae, Sajuki akamwambia mama yake mzazi kwamba Wastara nampenda sana, kanizalia mtoto mzuri anaitwa Farhini, naomba msimsumbue naomba msimpe shida yoyote amenisaidia sana, naomba mumwachie Farhini amlee amtunze mtamuona, yalikua maneno mazito sana mpaka machozi yakawa yananitoka”
Kwenye mstari mwingine Dinno amesema jambo jingine ambalo Sajuki aliliongea mwishoni ni kuhusu upendo miongoni mwa wasanii wa movie Tanzania, namkariri akisema “alikua ananiambia hebu jitahidi kuwa unakaa na wasanii, unajua sisi hatupendani Dinno ila mimi iko siku nitakuja kuropoka nikae na watu niwazungumzie tuweke upendo pamoja, tukishapendana tutafanya kitu Dinno”

by millardayo.com