Friday, August 23, 2013

ANGELLAH KAIRUKI ALIPOTOA BAISKELI KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA VIUNGO



Angella Kairuki akiwa na watoto wake Kemy pamoja na Esta muda mfupi baada ya kukabidhi baiskeli hizo.
Mama kairuki akiongea na mtoto Halima ambaye naye pia alipata baiskeli hiyo.
Wazazi wakiwa na watoto wao baada ya kukabidhiwa baiskeli zao

..........

...............

mtoto mmojawapo wa Mama Kairuki akimuendesha mtoto mmoja wapo aliyekabidhiwa baikeli

Mama Kairuki akiwa na familia yake pamoja na mtoto Halima
Mama Kairuki akisisitiza jambo

Mama Kairukia akimuendesha mtoto Halima





Mheshimiwa akikabidhi  baadhi ya zawadi zingine kwa mzazi kwa niaba ya watoto

Mama yake na Zitto Kabwe ambaye pia ni kiongozi wa SHIVYAWATA akishukuru kwa niaba ya uongozi mzima wa chama hicho
Mtoto akifurahia zawadi zake


WAZIRI KAIRUKI ATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU

NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki ambaye pia ni Mlezi Mkuu wa kikundi cha waandishi wa habari wajasiriamali (HABARI GROUP), ametoa msaada wa basikeli maalum kwa watoto wenye ulemavu kupitia shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu nchini (SHIVYAWATA).

Angellah alikabidhi viti hivyo jana, vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 12, kwa baadhi ya watoto hao, na baadaye kuwafikia watoto wote wenye mahitaji.

Akizungumza wakati wa kukabidhi, alisema viti hivyo ni maalum kwa watoto wenye miaka kuanzia sifuri hadi tisa, na ametoa kutokana na kuguswa na matatizo ya wenye ulemavu na pale anapopata nafasi anawakumbuka.

"Nimekuwa nikifanya kazi zaidi na watoto wenye ulemavu wa kusikia (Viziwi), lakini pia nikaona kuna kundi lina mahitaji zaidi, hivyo kwa kidogo nilichopata  nikawambuka, nafanya kazi kwa kushirikisha familia yangu,  sitaishia hapa nitawasaidia zaidi kwa kadri nitakavyojaaliwa,"aliongeza kiongozi huyo aliyekuwa ameambatana na wanaye wawili.

Akishukuru kwa msaada huo, Katibu wa SHIVYAWATA, Felician Mkudem alisema kuwa  wanafarijika sana kuona watu muhimu kama Angellah, wanakumbuka na kuwajali.

"Kiongozi wa serikali ndiye jicho na sauti za watu wenye ulemavu, hivyo kwa kutusaidia vifaa saidizi kwa wtaoto wenye ulemavu ni faraja kubwa sana, kwani mambo hayo ni miongoni mwa tunayoyapigania,"alisema.

Mkude alitumia fursa hiyi kukamabidhi nyaraka mbalimbali, ikiwemo mpango mkakati wa ukondaishaji wa watu wenye ulemavu na sheria mbalimbali zinazowahusu.
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ulemavu wa Viungo, (CHAWATA), Shida Salum aliishukuru serikali ya Rais Kikwete kuwakumbuka watu wenye ulemavu na kuwafanyia mengi kwa ajili ya ustawi wao.

Wazazi wa watoto hao walishukuru kwa msaada huo na kwamba utawasaidia  watoto wanaosoma waliokuwa wanabebwa kwenda na kurudi shule, na wengine waliokuwa hawajaanza masomo kutokana na hali ngumu ya kuwafikisha shuleni.

Viti hivyo vipatavyo 29, viligawiwa kwa watoto watano, wengine wawili wakiwa wanapata huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na vingine vilivyobaki watatafutwa wenye mahitaji na kukabidhiwa.