Sunday, April 19, 2015

WATANZANIA tusimame kupinga mauaji ya albino - Lowassa

WATANZANIA wametakiwa kulaani na kukemea mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino kwa kuwa matukio hayo yanaitia aibu nchi ya Tanzania na kupoteza sifa yake, kuwa nchi yenye amani.

Aidha Chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania (TAS) kimetakiwa kushawishi majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo kutokana na mauaji ya watu wenye ualbino kumfikia mapema Rais Jakaya Kikwete ili kutoa hakumu.

Wito huo ulitolewa Jijini Dar es salaam jana na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa wakati akihutubia mamia ya vijana walioshiriki katika matembezi ya hiyari ya kulaani na kupinga mauaji, ukataji wa viungo pamoja na ufukuaji wa makaburi ya watu wenye ualbino.

Lowassa akiwa mwenye afya njema akiwa na wabunge, madiwani pamoja na watu wenye ulemavu huo walitembea umbali wa kilometa tano kuanzia Uwanja wa Taifa na kupitia Temeke Hospitali, Chang'ombe Polisi, Shule ya Sek
ondari Kibasila na kumalizia katika viwanja vya TCC Club kwa kutumia dakika 25.

No comments:

Post a Comment