Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM).MBUNGE
wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), ameingia katika matata.
Katika kujaribu kudhibiti mtoto wa shule ambaye anadai alibakwa naye na
kuambukiwa virusi vya ukimwi, mbunge huyo ametoa vitisho vya kuua mtoto
huyo na kujiua kama njia ya kuepuka dhahama inayoelekea kumkabili.
Siku
moja baada ya gazeti hili kuripoti habari za mbunge mmoja (bila kumtaja
jina), jana asubuhi Profesa Kapuya ameibuka na kumtisha mwanafunzi huyo
mwenye miaka 16 anayesoma Shule ya Sekondari Turiani iliyoko Magomeni
jijini Dar es Salaam.
Baada ya kujua kuwa mtoto huyo ndiye alitoa
habari za masahibu hayo, ambayo mbunge hakutaka yajulikane, alimpigia
simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.
Jana Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Profesa Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.
Alfajiri
saa 11:21 kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0784993930, Profesa
Kapuya alituma ujumbe ufuatao kwa mtoto huyo: “chagueni kunisubiri tuje
tuongee au mnataka kufa?”
Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma
ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema:
“Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake
kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu.
“Mwambieni
Mbowe mwenye hilo gazeti awape nyumba ya kuishi. Si mmemuingizia hela
leo? Mnatumika bure watu wanaingiza hela nyingi, mmenitibua lazima
niwauwe wiki hiii haitaisha, nitapanga kambi popote.
“Jana si
wamekuficha? Tuone kama utalindwa milele. Kazi ya kulindwa imeisha,
maana wameshatengeneza hela. Lazima mvae sanda. Hilo sio ombi, ni wajibu
wenu. Mnajitia mafia watoto sio? Watoto wetu wanauza unga, nani
anawakamata? Nani atapigana nasi?”
Hata hivyo, baada ya kuhisi
kuwa watoto hao wamedhamiria kumchukulia hatua, na wamewasiliana na
taasisi mbalimbali za kiraia na serikali zenye uwezo wa kumtia adabu,
mbunge huyo alimtumia mtoto huyo ujumbe wa kuonyesha alikuwa anafikiria
kunywa sumu..
Ujumbe huo uliotumwa kwa mtoto huyo saa 11:2 3
ulisema: “nimwakosea sana, acha nife mie nakunywa sumu nijiue, na nyie
mje mnizike.”
Hasira za Profesa Kapuya dhidi ya mtoto hao
zilitokana na hatua ya mtoto huyo na dada yake kufichua unyama wanaodai
kutendewa na mbunge huyo, ambaye amewahi kushika nyadhifa kadhaa za
uwaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.
Tangu alipogundua kuwa
mtoto huyo alizungumza na gazeti hili juzi, saa 5:17 usiku wa kuamkia
jana alituma ujumbe usemao: “Si mpo Bilz? Sasa tupo pamoja na nyie mpaka
usiku.”
Baadaye saa 5:31 alituma ujumbe huu: “Hivi hamkubali kushindwa? Leo ulifuata nini ofisi ya CCM?”
Ujumbe
huo ulitokana na ukweli kwamba dada wa mtoto anayedaiwa kubakwa alifika
Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) juzi asubuhi kuonana na Katibu
Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, ili kuomba chama kimsaidie
kumbana Profesa Kapuya, ambaye alikuwa ameanza kuwatisha yeye na mdogo
wake.
Hata hivyo, kwa mujibu wa mtoto huyo, Kinana alisema suala hilo si la chama bali la Profesa Kapuya binafsi.
Mtoto
huyo alikataa ushauri wa kupeleka shauri hilo mbele ya vyombo vya
sheria, akidai kuwa jitihada zake zimekuwa zinazimwa na mbunge huyo
anayedai serikali haiwezi kumfanya lolote.
Alisisitiza kuwa hana
imani na serikali, lakini akasema yupo tayari kuchukua hatua kali dhidi
ya Profesa Kapuya iwapo atasimamiwa na watetezi wa haki za binadamu.
Baadhi
ya mashirika yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha Sheria na
Haki za BInadamu (LHRC) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP)
yalijitokeza kumsaidia watoto hao, ambao ni yatima.
Mtoto huyo na
dada yake, wakizungumza na gazeti hili kwa hofu mafichoni, walisema kwa
sasa hawana imani tena kama kuna serikali nchini Tanzania kwa kuwa
wamedhalilishwa, wametembezwa hadi Bungeni na wabunge bila hatua
kuchukuliwa, licha ya kutoa taarifa katika kituo cha polisi Oysterbay
tangu mwaka jana.
Hata hivyo, kabla ya tukio la watoto hao
kuripoti, ofisi za gazeti hili juzi usiku kulikuwa na watu waliokuja
wakiwatafuta watoto hao, huku wakiwatisha kwa simu na kuwatolea maneno
ya kejeli, wakidai watawamwagia tindikali.
Mmoja wa watoto hao,
alidai kuwa miongoni mwa vijana waliokuwa wanawatisha juzi walikuwa
katika gari T170 BGY, Benz, Cream Metalic, ambayo inamilikiwa na mbaya
wao.
Jana gazeti hili lilichapisha habari kuwa mwanafunzi huyo
aliyesema kuwa waziri huyo alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii
iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho
katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012
alipoitwa kwenda kuchua ada kwa mara ya pili.
Akizungumza kwa uchungu, alisema mbunge huyo alifanya kitendo hicho kwenye Hoteli ya Giraffe, Jijini Dar es Salaam mwaka 2011.
Alisema
kuwa yeye alikuwa na urafiki na mwanafunzi mwenzake Zuhura
Mwaking’inda. Mwaking’inda amewahi kuwa Diwani wa Kata ya Sinza Jimbo la
Ubungo, Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo,
rafiki yake (mtoto wa Mwaking’ida) alikuwa amepooza hivyo alikuwa
analazimika kumhudumia hali iliyowaunganisha hadi huyo mtoto alipochukua
jukumu la kumtambulisha kwa baba yake ambaye naye alimtambulisha kwa
Kapuya ili aweze kumsaidia fedha kwa jili ada.
Mwanafunzi huyo
alisema baada ya kutambulishwa aliitwa katika hoteli moja jijini Dar
ambapo baada ya kufika mapokezi wafanyakazi wa hoteli hiyo walimkataza
kuingia chumbani katika maana kwamba umri wake alikuwa mdogo (mwaka 2011
alikuwa na miaka 14), lakini Kapuya aliamrisha aje chumbani pamoja na
dereva na kumwingiza kwa nguvu.
Akiwa chumbani alimlazimisha
kulala naye kisha kumpa sh laki saba, badala ya sh elfu sitini na saba
kiasi ambacho kilikuwa ndio mahitaji halisi ya ada.
Mwanafunzi
huyo amesema baada ya muhula mmoja aliitwa tena na mbunge huyo katika
Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala tarehe 3 June 2012,
ambapo pia alimlazimisha kulala naye kwenye zulia la ofisi yake, kisha
kumpa sh 350,000/.
Alisimulia kwamba wakati anatoka kwa huzuni
ofisini kwa mbunge huyo, mmoja wa wahudumu wa hapo alimuuliza kwanini
anatoka kwa huzuni, alimweleza kisa hicho, na huyo mama aliangua kilio
kwa kumwambia “mwanangu umekufa pole tu, huyu baba ni muathirika wa
ukimwi”.
Aliongeza kuwa baada ya kuambiwa vile alilia na kufanya
fujo hapo mapokezi hadi alipokamatwa na walinzi wa kisha kupelekwa kituo
cha polisi kufunguliwa mashtaka, lakini akiwa polisi alipoeleza mkasa
wote, Polisi walilazimika kumwita Kapuya na wakawasuluhisha kwa
makubaliano kwamba Kapuya atakuwa anamlipia ada, na kumpa pesa za
matumizi sh. laki tatu kila mwezi, jambo ambalo amekuwa akilitekeleza
kupitia simu yake ya mkononi 0755993930.
Kwa mujibu wa mwanafunzi
huyo, 24 Januari 2013, alifika mtu nyumbani kwao mtu mmoja (jina
tunalihifadhi) na kujitambulisha kuwa yeye ni jambazi na kuwa alitumwa
kwenda kuwaua kwa malipo ya sh. milioni 50, lakini alipokuta ni watoto
wadogo aliwasamehe, na kusema yeye ni jambazi sugu hawezi kupoteza nguvu
zake kuua vitoto.
Alienda akiwa na bastola, maji kwenye chupa
yanayodhaniwa kuwa ni tindikali na bomba la sindano. Kwa mujibu wa mtoto
huyo, jambazi huyo anasema kuwa tayari alilipwa milioni 15 za awali.
Mtoto
huyo alisema jambazi huyo aliwambia kuwa yeye ni rafiki wa mtoto wa
Kapuya na wanamfahamu vizuri, lakini hataweza kuaua baada ya kubaini
kuwa wao ni yatima tu.
Hata hivyo kufikia mwezi Februari mwaka
huu, mtu asiyefahamika alienda nyumbani na kutelekeza gari aina ya T.199
BGY Mercedes Benzi ya Blue wakati wanafunzi hao wakiwa shuleni, kisha
kuacha ufunguo kwa jirani yao kwa maelekezo kuwa wakifika awapatie.
Na
Kapuya aliwapigia simu kuwaarifu kuwa amempa zawadi ya gari kwa ajili
ya matumizi ila yeye na dada yake wanaruhusiwa kuuza ili wapate pesa kwa
ajili ya mahitaji yake siku zilizosalia, kwani muda sio mrefu baada ya
uchguzi mkuu 2015, Kapuya atakuwa Waziri Mkuu, hivyo itakuwa ngumu yeye
kumtumia huyo binti pesa kama alivyoelekezwa na jeshi la polisi kituo
cha Oysterbay.
Baada ya mwanafunzi huyo na dada yake ambaye ana
umri wa miaka 20, kupewa gari walishindwa kulitumia hivyo kutoa taarifa
polisi kwani kwa kupokea gari hilo ilikuwa ni kuwatelekeza kwani yeye
hana hata hela ya kuweka mafuta ya gari, hivyo walienda polisi ili kesi
ipelekwe mahakamani kumshtaki kapuya.
Polisi wa Oysterbay
walikubali kulipeleka tatizo hilo kwa Katibu wa Bunge, ambaye alimwita
mwanafunzi huyo na mdogo wake waende Dodoma kukutana na Kamati ya Haki,
Maadili na Madaraka ya Bunge ingawa walipofika Dodoma walikaa na kamati
ya hiyo kwa maelezo kuwa Kapuya hakuwepo hadi Bunge lilipoisha
walirejeshwa Dar es Salaam.
Mtoto huyo na dada yake alitoka ofisi
za CCM lakini akiwa anaelekea kituo cha basi alithadharishwa na
mwanafunzi mwingine kwa haraka kuwa akimbie kwa kuwa atamwagiwa
tindikali na watu waliokuwa wanamfuata nyuma, alikimbilia katika mtaa wa
Hoteli ya Star light kisha aliomba msaada baada ya kupotea njia na
hivyo alisaidiwa na mama mmoja kufikishwa chumba cha habari cha Channel
Ten.
Ni katika chumba hicho ndio mwandishi wa habari hizi alienda
na kuwakuta watu wawili hao waliokuwa wanamhitaji binti huyo lakini
walikatazwa kumchukua.
-TANZANIA DAIMA