Pichani
kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mh James Mbatia,
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe, Waziri mkuu mstaafu Mh Edward
Lowassa na Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Lipumba
Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa leo amejiunga na Ukawa kupitia
chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema katika hafla iliyohudhuriwa na
waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.
Hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na Viongozi wote wanaunda umoja wa
Katiba ya Wananchi Ukawa akiwemo mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba,
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mh
James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD Mh Emmanuel Makaidi.
Mh Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya Kujiunga na CHADEMA mama Regina Lowassa
Waziri
Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa na Mkewe mama Regina Lowassa wakionyesha
kadi zao za Uanachama wa CHADEAMA mara baada ya kujiunga na CHADEMA
katika hafla iliyofanyika Bahari Beach Hotel
Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa akiwa na Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Lipumba
Mwenyekiti
wa Baraza la wanawake CHADEMA na Mbunge wa Kawe Mh Halima Mdee
akisikiliza kwa makini yaliyokuwa yakijili katika hafla ya kujiunga na
Chadema kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh Edward Lowassa
Lowassa ambaye aliambatana na mkewe Mama Regina Lowassa wote
walikabidhiwa kadi ya kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) na Mh Freeman Mbowe.
No comments:
Post a Comment