Marehemu Mawazo alivyoagwa na wana-CHADEMA Mwanza leo.. (Picha) #RIP
Taarifa iliyotolewa jana na viongozi wa
CHADEMA Mwanza ilielekeza utaratibu wa siku tatu mfululizo mpaka mazishi
ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Geita, Marehemu Alphonce Mawazo.
Leo kuanzia asubuhi taratibu zilianza kwa kuutoa mwili wa Marehemu Hospitali, wakaelekea viwanja vya Furahisha
vilivyopo katikati ya Mwanza kwa ajili ya shughuli za kumuaga marehemu
ambapo viongozi mbalimbali wa CHADEMA wamewaongoza wanaCHADEMA
waliokusanyika katika viwanja hivyo kumuaga marehemu.
Papa Francis ndiye kiongozi wa kwanza wa Kanisa katoliki kutoka mataifa ya Amerika.
Kiongozi
huyu alizaliwa mjini Buenos Aires, Argentina 17 Desemba mwaka 1936 na
kupewa jina Jorge Mario Bergoglio. Babake, Mario, alikuwa mhasibu katika
shirika la reli nchini humo. Mamake Bi Regina Sivori alikuwa tu mke
nyumbani aliyeshughulisha zaidi na kuwalewa watoto wake watano.
Ujanani
Papa Francis alipenda sana kandanda na aliwahi kufanya kazi za kawaida
kama kuwa mlinzi katika jumba la starehe. Na katika shughuli zake za
kidini kuna wakati viongozi wa kisiasa wa Argentina walimtaja kama
mpinzani wao kisiasa.
Papa Francis hupenda sana kutangamana na watu wa kawaida
Papa Francis anajiita mtu wa kawaida, msemo wake
maarufu na ambao ameutumia mara kadhaa ni kwamba, "watu wangu ni maskini
na mimi ni mmoja wao".
Si jambo la kushangaza, hivyo basi, kwamba
kiongozi huyo ya Wakatoliki bilioni 1. 4 anaishi maisha ya kawaida sana
na katika nyumba ya kawaida makao makuu Vatican. Huwa anajipikia
mwenyewe chakula chake.
Papa Francis hata kabla ya kuwatazwa kwake
na kuwa kiongozi ya Wakatoliki duniani, katika huduma zake za kidini
alionekana kama mtu wa kawaida sana, mpenda maskini na watu wa kawaida
na asiyetaka makuu.
Hata mavazi yake ya kidini sio yale yaliyo na mapambo mengi.
Hii
ni kutokana na kwamba yeye ni wa huduma ya Wa-Jesuit. Wafuasi wa huduma
hii ni makasisi waliojitilea kuishi maisha ya umaskini na kuwahudumia
zaidi maskini na wasiojiweza miongoni mwa jamii.
Kabla ya
kuingilia shughuli za kidini na hatimaye kujiunga na chuo cha mafunzo ya
kidini, kiongozi huyo aliwahi kufanya kazi katika maabara na pia kama
mlinzi katika jumba moja la starehe huko Argentina. Na baadaye akiwa na
umri wa miaka 33 alitawazwa kuwa kasisi wa Kanisa Katoliki
Hatimaye alipanda na kuwa Askofu wa jimbo la Buenos
Aires mwaka 1998 na miaka miatatu baadaye Papa John Paul II alimtawaza
kuwa Kadinali.
Alipokuwa Kadinali serikali za Rais Néstor Kirchner
na mrithi wake Cristina Fernández de Kirchner zilimuona kiongozi huo wa
kidini kama mpinzani wao kisiasa. Tangu enzi hizo hadi wa leo Papa
Francis msimamo wake ni kwamba "Ukimfuata Kristo lazima ufahamu kuwa
kuwanyanyasa watu au kuwanyima haki zao ni dhambi kubwa sana.”
Viongozi
kadhaa wa dini na madhehebu mengine wamemtaja Papa Francis kama
kiongozi mwenye kupenda uhusiano bora miongoni mwa dini na madhehebu
tofauti. Kwa mfano mwezi Novemba mwaka 2012 katika Kanisa kuu la
Kikatoliki mjini Buenos Aires, Papa Francis aliwaleta pamoja viongozi wa
Kiyahudi, Waislamu na madhehebu ya kiinjilisti katika ibada maalum ya
pamoja ya kuombea amani na suluhu ya machafuko Mashariki ya Kati.
Na ndio pengine tarehe 13 Machi, 2013 alipochaguliwa
kuwa kiongozi wa Wakatoliki wote duniani viongozi wa Kiislamu mjini
Buenos Aires walisifu uteuzi wake na kumtaja kama " rafiki wa Waislamu
na mtu anayependa kushauriana na watu wa dini zote".
chanzo BBC
Ziara ya Papa Francis!! Hivi ndivyo Wakenya walivyomkaribisha ....
Papa Francis wa kanisa katoliki duniani ameanza ziara yake katika nchi za Afrika na leo alikuwa Kenya.
Papa Francis alilakiwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika uwanja
wa ndege uliopo Nairobi na kuwashukuru Wakenya kwa kumkaribisha vizuri
huku akiwatakiwa baraka tele za Mwenyezi Mungu.
Nchi nyingine za Afrika ambazo Papa Francis atatembelea ni pamoja na Uganda pamoja na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
a ya kuagwa na
maziko ya marehemu Alphonce Mawazo wa Chadema hii hapa, Lowassa, Sumaye
na Mbowe kuongoza maombolezo Ratiba ya shughuli ya utoaji heshima za
mwisho na mazishi ya Kamanda Mawazo Leo Siku ya Ijumaa, Novemba 27 saa 2
asubuhi, mwili wa Mpiganaji na Kiongozi wetu Alphonce Mawazo
utachukuliwa Hospitali ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba yake mdogo,
eneo la Nyegezi-Swea kwa ajili heshima za familia kabla ya kuelekea
Viwanja vya Furahisha ambapo Viongozi waandamizi wa UKAWA, wakiongozwa
wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, Mgombea Urais Edward
Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, wabunge wa UKAWA,
wataongoza maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake kutoa
heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mawazo. Baada ya Viwanja vya
Furahisha, mwili wa Mpiganaji Mawazo utasafirishwa kuelekea Geita kwa
ajili ya kuwapatia nafasi wakazi wa Mkoa wa Geita kumuaga Kiongozi wao
siku ya Jumamosi, Novemba 28 kuanzia asubuhi mapema ambapo baadae mchana
mwili huo utapelekwa Mji Mdogo wa Katoro, mkoani Geita, ambapo pia
wananchi watapata fursa ya kumpatia heshima za mwisho na kumuaga Mawazo
ambaye alikuwa ni Mgombea wao wa Ubunge wa Jimbo la Busanda. Baada ya
wakazi wa Katoro kushiriki tukio hilo, mwili wa Kamanda Mawazo
utapelekwa nyumbani kwao kijijini Chikobe tayari kumhifadhi kwenye
nyumba ya milele shambani kwake, siku a Jumapili, Novemba 29, baada ya
familia, ndugu, jamaa na wakazi wa kijiji hicho kutoa heshima zao za
mwisho. Tumaini Makene Msemaji Mkuu Chadema
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Sentensi 7 za Mbowe nje ya Mahakama baada ya kuruhusiwa kuaga mwili wa marehemu Mawazo Mwanza.
Ishu ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kuzuiwa kuaga mwili wa MarehemuAlphonce Mawazo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Geita imekuwa ikiripotiwa na kuandikwa kwenye vyombo vya habari huku ikisubiriwa kutolewa majibu na Mahakama Kuu Mwanza kuhusu hatma ya zuio hilo.
Leo maamuzi ya Mahakama Kuu Mwanza
yametoka na majibu kwamba wanaCHADEMA na viongozi wao wamepata kibali
cha Mahakama hiyo kuendelea na shughuli za kuaga pamoja na mazishi ya
kiongozi huyo.
Marehemu Alphonce Mawazo kwenye Jukwaa la Kampeni enzi za uhai wake.
Nje ya Mahakama Kuu Mwanza, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe alipata dakika chache kuongea na wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa wakisubiri kusikia maamuzi ya Mahakama >>>> “Ni
lazima tukae vikao kupanga ratiba ya kumuaga Kamanda Mawazo, Jaji
ametoa maelekezo kwamba viongozi wa CHADEMA, familia ya marehemu na
Jeshi la Polisi wakae pamoja kupanga ratiba kamili.”
“Tutaheshimu
maelekezo ya Jaji lakini hatutakubali kuonewa, muwe na imani kwamba
haki itatendeka… tunakwenda kwenye vikao lakini tunahitaji kumaliza
jambo hili kuanzia kesho, tutamuaga Mawazo kwa heshima anayostahili
katika eneo ambalo tutawatangazia.” >>> Freeman Mbowe.
Ezekiel Wenjena Salum Mwalimu wakiwa ndani ya Mahakama Mwanza.
Watu wa usalama nje ya Mahakama Kuu Mwanza.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wanaCHADEMA
Wakili wa CHADEMA, John Mallya.
Kwa hisani ya Millart Ayo.com
Ratiba ya kuagwa na
maziko ya marehemu Alphonce Mawazo wa Chadema hii hapa, Lowassa, Sumaye
na Mbowe kuongoza maombolezo Ratiba ya shughuli ya utoaji heshima za
mwisho na mazishi ya Kamanda Mawazo Leo Siku ya Ijumaa, Novemba 27 saa 2
asubuhi, mwili wa Mpiganaji na Kiongozi wetu Alphonce Mawazo
utachukuliwa Hospitali ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba yake mdogo,
eneo la Nyegezi-Swea kwa ajili heshima za familia kabla ya kuelekea
Viwanja vya Furahisha ambapo Viongozi waandamizi wa UKAWA, wakiongozwa
wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, Mgombea Urais Edward
Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, wabunge wa UKAWA,
wataongoza maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake kutoa
heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mawazo. Baada ya Viwanja vya
Furahisha, mwili wa Mpiganaji Mawazo utasafirishwa kuelekea Geita kwa
ajili ya kuwapatia nafasi wakazi wa Mkoa wa Geita kumuaga Kiongozi wao
siku ya Jumamosi, Novemba 28 kuanzia asubuhi mapema ambapo baadae mchana
mwili huo utapelekwa Mji Mdogo wa Katoro, mkoani Geita, ambapo pia
wananchi watapata fursa ya kumpatia heshima za mwisho na kumuaga Mawazo
ambaye alikuwa ni Mgombea wao wa Ubunge wa Jimbo la Busanda. Baada ya
wakazi wa Katoro kushiriki tukio hilo, mwili wa Kamanda Mawazo
utapelekwa nyumbani kwao kijijini Chikobe tayari kumhifadhi kwenye
nyumba ya milele shambani kwake, siku a Jumapili, Novemba 29, baada ya
familia, ndugu, jamaa na wakazi wa kijiji hicho kutoa heshima zao za
mwisho. Tumaini Makene
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu