a ya kuagwa na
maziko ya marehemu Alphonce Mawazo wa Chadema hii hapa, Lowassa, Sumaye
na Mbowe kuongoza maombolezo Ratiba ya shughuli ya utoaji heshima za
mwisho na mazishi ya Kamanda Mawazo Leo Siku ya Ijumaa, Novemba 27 saa 2
asubuhi, mwili wa Mpiganaji na Kiongozi wetu Alphonce Mawazo
utachukuliwa Hospitali ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba yake mdogo,
eneo la Nyegezi-Swea kwa ajili heshima za familia kabla ya kuelekea
Viwanja vya Furahisha ambapo Viongozi waandamizi wa UKAWA, wakiongozwa
wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, Mgombea Urais Edward
Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, wabunge wa UKAWA,
wataongoza maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake kutoa
heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mawazo. Baada ya Viwanja vya
Furahisha, mwili wa Mpiganaji Mawazo utasafirishwa kuelekea Geita kwa
ajili ya kuwapatia nafasi wakazi wa Mkoa wa Geita kumuaga Kiongozi wao
siku ya Jumamosi, Novemba 28 kuanzia asubuhi mapema ambapo baadae mchana
mwili huo utapelekwa Mji Mdogo wa Katoro, mkoani Geita, ambapo pia
wananchi watapata fursa ya kumpatia heshima za mwisho na kumuaga Mawazo
ambaye alikuwa ni Mgombea wao wa Ubunge wa Jimbo la Busanda. Baada ya
wakazi wa Katoro kushiriki tukio hilo, mwili wa Kamanda Mawazo
utapelekwa nyumbani kwao kijijini Chikobe tayari kumhifadhi kwenye
nyumba ya milele shambani kwake, siku a Jumapili, Novemba 29, baada ya
familia, ndugu, jamaa na wakazi wa kijiji hicho kutoa heshima zao za
mwisho. Tumaini Makene Msemaji Mkuu Chadema
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu

Sentensi 7 za Mbowe nje ya Mahakama baada ya kuruhusiwa kuaga mwili wa marehemu Mawazo Mwanza.
Ishu ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kuzuiwa kuaga mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Geita imekuwa ikiripotiwa na kuandikwa kwenye vyombo vya habari huku ikisubiriwa kutolewa majibu na Mahakama Kuu Mwanza kuhusu hatma ya zuio hilo.
Leo maamuzi ya Mahakama Kuu Mwanza
yametoka na majibu kwamba wanaCHADEMA na viongozi wao wamepata kibali
cha Mahakama hiyo kuendelea na shughuli za kuaga pamoja na mazishi ya
kiongozi huyo.
Nje ya Mahakama Kuu Mwanza, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe alipata dakika chache kuongea na wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa wakisubiri kusikia maamuzi ya Mahakama >>>> “Ni
lazima tukae vikao kupanga ratiba ya kumuaga Kamanda Mawazo, Jaji
ametoa maelekezo kwamba viongozi wa CHADEMA, familia ya marehemu na
Jeshi la Polisi wakae pamoja kupanga ratiba kamili.”
“Tutaheshimu
maelekezo ya Jaji lakini hatutakubali kuonewa, muwe na imani kwamba
haki itatendeka… tunakwenda kwenye vikao lakini tunahitaji kumaliza
jambo hili kuanzia kesho, tutamuaga Mawazo kwa heshima anayostahili
katika eneo ambalo tutawatangazia.” >>> Freeman Mbowe.
Kwa hisani ya Millart Ayo.com
Ratiba ya kuagwa na
maziko ya marehemu Alphonce Mawazo wa Chadema hii hapa, Lowassa, Sumaye
na Mbowe kuongoza maombolezo Ratiba ya shughuli ya utoaji heshima za
mwisho na mazishi ya Kamanda Mawazo Leo Siku ya Ijumaa, Novemba 27 saa 2
asubuhi, mwili wa Mpiganaji na Kiongozi wetu Alphonce Mawazo
utachukuliwa Hospitali ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba yake mdogo,
eneo la Nyegezi-Swea kwa ajili heshima za familia kabla ya kuelekea
Viwanja vya Furahisha ambapo Viongozi waandamizi wa UKAWA, wakiongozwa
wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, Mgombea Urais Edward
Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, wabunge wa UKAWA,
wataongoza maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake kutoa
heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mawazo. Baada ya Viwanja vya
Furahisha, mwili wa Mpiganaji Mawazo utasafirishwa kuelekea Geita kwa
ajili ya kuwapatia nafasi wakazi wa Mkoa wa Geita kumuaga Kiongozi wao
siku ya Jumamosi, Novemba 28 kuanzia asubuhi mapema ambapo baadae mchana
mwili huo utapelekwa Mji Mdogo wa Katoro, mkoani Geita, ambapo pia
wananchi watapata fursa ya kumpatia heshima za mwisho na kumuaga Mawazo
ambaye alikuwa ni Mgombea wao wa Ubunge wa Jimbo la Busanda. Baada ya
wakazi wa Katoro kushiriki tukio hilo, mwili wa Kamanda Mawazo
utapelekwa nyumbani kwao kijijini Chikobe tayari kumhifadhi kwenye
nyumba ya milele shambani kwake, siku a Jumapili, Novemba 29, baada ya
familia, ndugu, jamaa na wakazi wa kijiji hicho kutoa heshima zao za
mwisho. Tumaini Makene
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
No comments:
Post a Comment