Siti binti Saad |
Siti binti Saad
Alizaliwa katika kijiji cha Fumba, Zanzibari mwaka 1880. Alipozaliwa alipewa jina la 'Mtumwa' hii ni kwa vile alizaliwa katika kipindi cha utumwa wa Kiarabu. Jina la Siti alipewa na mkabaila mmoja wa kiarabu.
Baba yake bwana Saadi alikuwa ni Mnyamwezi kutoka Tabora na mama yake alikuwa ni Mzigua toka Tanga,
lakini wote wawili walizaliwa Zanzibari. Hali ya maisha ya familia yao
ilikuwa ni duni sana na walijishughulisha zaidi katika shughuli za
kilimo na ufinyanzi kazi ambazo Siti alijifunza na kuzimudu vizuri pia.
Maisha ya awali:
Kama waswahili wasemavyo 'kuzaliwa masikini si kufa masikini' Siti
alibarikiwa kuwa na kipaji cha pekee cha uimbaji. Kipaji hiki
kilimsaidia sana tangu siku za awali za maisha yake kwani alitumia
uimbaji wake kuuza vyungu vya mama yake alivyokuwa akimsaidia
kuvitembeza. Siti alipoimba sauti yake iliweza kupaa na kusafiri kwa
umbali wa maili nyingi na hii ndio ilikuwa ishara ya watu kujua kwamba
vyungu vya kina Mtumwa vinapita leo. Alifananishwa kuwa na mapafu yenye
nguvu kama ya simba kutokana na alivyoweza kupaza sauti yake mbali na bila kuachia pumzi.
Kutokana na wakati huo elimu kwa watoto wa kike kutotiliwa mkazo, Siti hakuwahi kwenda shule wala kuhudhuria mafunzo ya Kurani.
Hivyo mnamo mwaka 1911 aliona ni bora ahamie mjini ili kubooresha
maisha yake zaidi. Ujio wake wa mjini ulikuwa wa neema kwani alikutana
na bwana mmoja wa kundi la muziki wa Taarabu
la "Nadi Ikhwani Safaa" aliyeitwa Muhsin Ali. Katika kipindi hicho hilo
ndilo lilikuwa kundi pekee la muziki wa taarabu lililoanzishwa na
Sultani mpenda starehe na anasa bwana Seyyid Barghash Said. Kundi hili
lilikuwa ni la wanaume peke yake , wanawake hawakuruhusiwa kujiunga na
vikundi vya muziki kwa vile ilikuwa ikichukuliwa kama ni uhuni. Bwana
Muhsin alikiona kipaji cha pekee cha Siti na hivyo akajitolea
kumfundisha kuimba kwa kufuata vyombo vya muziki na lugha ya kiarabu.
Baada ya hapo alikwenda kumtambulisha kwa wanamuziki wenzie wa "Nadi
Ikhwani Safaa" ambao bila kusita wakaanza kufanya naye maonyesho
mbalimbali katika jamii. Walipata mialiko mingi hasa kutoka kwa Sultani
na matajiri wengine wa Kiarabu, pia katika maharusi na sherehe zingine
mbalimbali, inasemekana ulifika wakati ambapo sherehe ilishindwa kufana
kama Siti binti Saadi hakuwepo kutumbuiza. Siti alikuwa ni moto wa
kuotea mbali na jina lake lilivuma kwa haraka sana hadi nje ya mipaka ya
nchi na bara la Afrika. Na punde Siti alianza kufananishwa na 'Umm
Kulthum', mwimbaji mahiri wa kike aliyetamba wakati huo kutoka Misri.
Kazi ya muziki
Kama nilivyosema moto wa Siti ulikuwa si wa kuusogelea karibu, mwaka
1928 kampuni ya kurekodi muziki ya Columbia and His Master's voice yenye
makazi yake Mumbai India
ilisikia umaarufu wa Siti binti Saadi na hivyo ikamwalika yeye pamoja
na kundi lake kwenda kurekodi kwa lugha ya Kiswahili ili kujaribu kama
muziki wake utauzika. Kampuni ile haikuweza kuamini jinsi muziki ule
ulivyouzika kwa kasi kubwa kwani wastani wa santuri 900 ziliweza kuuzika
katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo, na hadi kufikia 1931 santuri
72,000 zilikuwa zimeuzwa. Kutokana na kusambaa kwa santuri hizi,
umaarufu wa Siti ulizidi mara dufu watu kutoka sehemu mbalimbali za
dunia walikuwa wakija Zanzibari kuja kumwona. Mambo yalizidi kuwa mazuri
kwa Siti hadi ikafikia hatua kampuni ya kurekodi ya Columbia kuamua
kujenga studio ya kurekodi muziki palepale Zanzibar maalumu kwa ajili ya
Siti binti Saadi.
Hatua hiyo ya hadi kujengewa studio iliwaumiza wengi wenye wivu,
hivyo wakaanza kumtungia nyimbo za kumkejeli ili kumshusha na hasa
walitumia kigezo kwamba hana uzuri wa sura.
Siti aliendelea na shughuli yake ya muziki Hadi uzeeni, muda mfupi Kabla ya kifo chake alikutana na Mwandishi maarufu na mwanamashairi Shaaban Robert ambaye alimhoji na kuweza kuandika wasifu kuamka katika kitabu alichokiita "Wasifu wa Siti Binti Saadi." Wasifu Huu unaonekana kuwa bora zaidi Ndio uliowahi kuandikwa katika fasihi ya Tanzania. Kitabu hiki kinatumika kufundishia Shule za sekondari za Tanzania.
Tarehe 8 Julai, 1950 Siti Binti Saadi alifariki Dunia na kuacha pengo Kubwa katika Fani ya Taarabu. Ingawa pengo hilo haliwezi kuzibika lakini Kuna watu wengi walioweza kuibuka na umaarufu wa kuimba taarabu kupitia kwake, mfano hai nai Bi Kidude.
Hii ilikuwa baada ya kifo chake Jina ziwa bado linatumika sana Kama kielelezo cha ushujaa kutokana, Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA), kimetumia Jina ziwa kulipa Jina gazeti la Chama Chao "Sauti ya Siti". Hadi leo kufuatilia Siti hutumika Kama kipimo cha kufundishia uimbaji wa Taarabu. Na anakumbukwa katika historia yake ya kuwa Mwanamke wa Kwanza Afrika Mashariki kurekodi muziki katika santuri.
No comments:
Post a Comment