Wednesday, August 29, 2012

MWILI WA MAREHEMU MZEE BUKUMBI WAAGWA JIJINI MWANZA LEO



mke wa marehemu, Bi Asteria Bukumbi akipita katika mwili wa mume wake kipenzi mzee Bukumbi.

mtoto wa marehemu, Erick James Shigongo akipita mbele ya mwili wa baba yake kipenzi kwa kuaga, Mungu ailaze roho ya marehemu James Bukumbu, mahali pema peponi...amen


MWILI wa marehemu Mzee James Bukumbi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili, Agosti 26, 2012 jijini Dar, leo umeagwa na mamia ya waombolezaji waliofika nyumbani kwake eneo la Mecco Nyakato, jijini Mwanza. Ibada ya kuuombea mwili wa marehemu imefanyika katika kanisa la RC Nyakato - Nundu jijini Mwanza. Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho asubuhi kupelekwa Bupandwamhela, Sengerema kwa maziko yatakayofanyika saa 9 alasiri.

No comments:

Post a Comment