WAHARIRIR WAIGOMEA SHERIA YA MTANDAONI
Ni kama wamegoma, Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini wameitaka serikali kuacha kuharakisha zoezi la kutia saini sheria ya mtandaoni badala yake wajikite kutoa Elimu kwa watanzania ili sheria hiyo ifahamike,
Wakizungumza katika Mkutano maalum
ulioitishwa na wizara ukilenga kuwapa elimu juu ya sheria hiyo
inayosubiri kuwekwa saini na Mh. Rais Jakaya Kiwete, wamesema sheria
hiyo inamatatizo na inahitaji muda wadau waipitie na kuielewa,
Wamesema makosa yaliyoainishwa katika sheria hiyo
ambao kama ikitiwa saini na kuanza kutumika, inaweza kuwabana watu ambao
hawahusiki.
Baadhi ya makosa yaliyoanishwa katika sheria hiyo
ni pamoja na kutuma taarifa bila ridhaa ya mtu, kusambaza picha za ngono
na za utupu, udanganyifu unaohusiana na kompyuta, makosa yanayohusiana
na utambuzi, kughushi kunakohusiana na masuala ya kompyuta na kusambaza
picha za utupu za watoto.
Mengine ni unyanyasaji kwa kutumia mtandao,
kuchapisha taarifa yoyote ambayo itasababisha mauaji ya kimbari, uongo
na matusi ya kibaguzi, huku adhabu kali ikiwa ni faini ya Sh50 milioni
au kifungo kisichopungua miaka saba, kwa mtu atakayebainika kusambaza
picha za ngono mtandaoni.
Sheria hiyo pia iliwahi pia kulalamikiwa na
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika aliyeitaka Serikali ikusanye
maoni ya wadau kabla ya kuwasilisha muswada huo kwa hati ya dharua
kutokana na umuhimu wake kwa jamii.
Wamedai kuwa sheria hiyo inaweza kuifanya Tanzania ikawa ni
kati ya nchi adui wa matumizi ya mtandao wa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (Tehama).
“Sheria hii itamuathiri mtu yeyote anayeweza
kutumia mtandao wa intaneti kwa kutumia kifaa chochote iwe kompyuta
kubwa au vifaa vyenye uwezo wa kufanya kazi kama kompyuta kama simu za
kiganjani, televisheni na vifaa vingine vinavyoendana na hivyo,”Amesema Peter Nyanje Mhariri wa the Citizen.
No comments:
Post a Comment