Tuesday, November 20, 2012

HUKUMU YA FUNDIKIRA WATU WALIA NA KUZIMIA MAHAKAMANI

 
Leo ilikuwa ndiyo siku ya hukumu dhidi ya watuhumiwa watatu wa mauaji ya marehemu Swetu Fundikira aliyeuawa kwa kupigwa miaka miwili iliyopita. Mara baada ya watuhumiwa hao kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa, ndugu na jamaa wa marehemu waliangua kilio na wengine hadi kuzimia kama walivyoshuhudiwa na paparazi wetu aliyeweka kambi mahakamani hapo. Kushoto ni dada wa marehemu Rehema Fundikira, Hadija Mdemu shemeji wa marehemu.
....mmoja wa ndugu wa Fundikira akibebwa mara baada ya kuzimia na kudondoka sakafuni
....akipepewa huduma ya kwanza kwa kupepewa
....akipata nafuu kiasi
.....ndugu wakilia
ndugu wakilia
...ilikuwa ni saa ya majonzi na huzuni
Watuhumiwa wakiwa mahakamani kabla ya hukumu kusomwa. kutoka kulia ni Rhoda Robert, Ally Gube na Mohamed Ally.
...safari ya huzuni ya Rhoda Robert kuanza maisha mapya gerezani mara baada ya hukumu,

ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Sajent Rhoda Robert, Koplo Ally Ngumbe na Mohamed Rashidi waliokuwa wakikabiliwa na Kesi ya mauaji ya Marehemu Swetu Fundikira imetolewa leo na Askari hao kuhukumiwa Kunyongwa hadi kufa.

Hukumu hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na ndugu jamaa na marafiki wa Swetu duniani kote ilitolewa leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hao watatu wametiwa hatiani baada ya kufanya kosa hilo siku ya Jumamosi tarehe 23 Januari, 2010 kwa kumpiga bila huruma Swetu Fundikira katika maeneo ya Kinondoni katika makutano ya barabara  za Mwinjuma na Kawawa jijini Dar es salaam mpaka kusababisha kifo chake.

Baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo vilio vimetawala kwa ndugu wa watuhumiwa hao huku baadhi ya watu wakidai sheria imechukua mkondo wake ipasavyo.
Marehemu Fundikira enzi za uhai wake.

picha kwa hisani ya globalpublishers.com

Friday, November 16, 2012

HUYU NDIYE MUME WA AUNT EZEKIEL.....

Rahma n Demonte hongereni
dada huyo ameolewaaaa lolest
wanameremeta,,wanameremeta

KINANA ARIPOTI KAZINI OFISI ZA LUMUMBA, DAR

 Wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, wakimkaribisha, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliporipoto kwa mara ya kwanza kwenye ofisi hiyo, leo, baada ya kuteuliwa juzi mjini Dodoma..
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.


by Bashir Nkoromo

Thursday, November 15, 2012

PONDA AFIKISHWA MAHAKAMANI CHINI YA ULINZI MKALI

 Ulinzio uliimarishwa katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakati kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda
 Watu waliofika kusikiliza kesi zao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu walipekuliwa na walinzi
 Ponda akiwa Mahakamani
 Askari Magereza akimfunga pingu Sheikh Ponda Issa Ponda baada ya kesi yake kuahirishwa hadi tarehe 29 novemba.
 Watuhumiwa wakiwa mahakamani
 Sheikh Ponda Issa Ponda akizungumza na wakili wake
Sheikh Ponda Issa Ponda akirudishwa rumande

KIPINDI CHA 'DIARY YA LADY JAYDEE' KURUSHWA EATV KILA JUMAPILI

 LADY JAYDEE
  Mkurugenzi wa Machozi Band,  Lady Jaydee akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salalaam leo wakati wa uzinduzi wa kipindi chake cha 'Diary Ya Lady Jaydee' kitakachoanza kurushwa hewani kila siku ya Jumapili kupitia televisheni ya EATV. Kushoto ni Mkuu wa Vipindi EATV, Lydia Igarabuza.

Mkuu wa vipindi wa Televisheni ya EATV, Lydia Karabuza akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kipindi cha televisheni cha 'Diary Ya Lady Jaydee kitakachoanza kurushwa hewani kuanzia Jumapili.
DAR ES SALAAM, Tanzania 
Msanii, Lady Jaydee amefanikiwa na kutambulika katika kiwanda cha muziki ndani na nje ya nchi, huku akitunukiwa tunzo nyingi zaidi akiwa albamu zake tano. Pamoja na kuwa anaendelea na fani yake ya muziki, Lady Jaydee ameamua kuwafikia na kuwaburudisha wapenzi wa kazi zake kwa njia nyingine.
Lady Jaydee sasa anaanza sura mpya ya burudani kwa kuleta kipindi cha TV kiitwacho DIARY YA LADY JAYDEE, ambacho kutaonekana katika kituo cha TV cha EATV
Diary Ya Lady Jaydee itaonesha maisha na hadithi za kweli za Lady Jaydee kwa lengo la
Kuburudisha kwa kuonesha mambo yate mazuri anayopitia au kuyaona Lady Jaydee
Kuelimisha kwa kushiriki mambo ya kijamii
Kutia moyo wengine wafuate ndoto zao kwa uadilifu
Kuongeza Kipato kama msanii kwa kutangaza biashara mbalimbali na hatimae kudumisha ajira binafsi kwa njia ya sanaa.
SHUKRANI
Lady Jaydee anatoa shukrani kwa mashabiki kwa kuendelea kumpokea, jambo ambalo linampa nguvu zaidi ya kufanya kaza.
pia anashukuru sana vyombo vya habari na zaidi anawashukuru EATV na washirika wake kwa kumpa nafasi ya kurusha kipndi chake kipya Diary Ya Lady Jaydee.
EATV imekuwa mchango wa aina yake katika kuwakuza wasanii Tanzania.
WITO
Lady Jaydee anatoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea kushirikiana na naye kwa kila namna, ili kukuza na kuendeleza kipaji chake na sanaa ya muziki wa Tanzania kwa ujumla wake.
Zaidi anatoa wito kwa makampuni kishiriki na kuungana nae ili waweze kumpa nguvu msanii, kutangaza biashara zao na kushawishi ajira katika fani ya muziki.
Na mwisho Lady Jaydee anawaribisha wote kusikiliza CDs zake au kuburidika na kundi lake la Machozi Band au kupata chakula ktk mgahawa wake wa kisasa Nyumbani Lounge au ukiwa umepumzika nyumbani utazame kipindi chake Diary Ya Lady Jaydee ktk EATV.

Saturday, November 10, 2012

WADAU WALIVYOJIACHIA KATIKA HARUSI YA MONYO


 Ankal akiwa na my wife wake
 Mama wa Rahateletz.blogspot.com nikiwa bize nia nikupe 'LIVE' kutoka ukumbini
 Wafanyakazi na watangazaji wa ITV
Gilian Lewis akiwa katika pozi na mume wake

HARUSI YA GODFREY MONYO LIVE UKUMBINI


HHuu ndio ukumbi wetu wa leo ni Mnazi Mmoja...
Maharusi wakipewa pombe ya asili aina ya mbege
 Maharusi wakiingia ukumbini
Ni tamu
Wageni waalikwa
Baadhi ya wafanyakazi wa IPP
Wadau waliwakilisha
 Hawa ndio mc wetu katika sherehe yetu ya leo juu ni REGNA MWALEKWA  chini ni GODWIN GONDE