LADY JAYDEE
Mkurugenzi wa Machozi Band, Lady
Jaydee akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salalaam leo
wakati wa uzinduzi wa kipindi chake cha 'Diary Ya Lady Jaydee'
kitakachoanza kurushwa hewani kila siku ya Jumapili kupitia televisheni
ya EATV. Kushoto ni Mkuu wa Vipindi EATV, Lydia Igarabuza.
Mkuu wa vipindi wa Televisheni ya EATV, Lydia Karabuza akifafanua jambo
wakati wa uzinduzi wa kipindi cha televisheni cha 'Diary Ya Lady Jaydee
kitakachoanza kurushwa hewani kuanzia Jumapili.
DAR ES SALAAM, Tanzania
Msanii, Lady Jaydee amefanikiwa na kutambulika katika kiwanda cha muziki ndani
na nje ya nchi, huku akitunukiwa tunzo nyingi zaidi akiwa albamu zake tano.
Pamoja na kuwa anaendelea na fani yake ya muziki, Lady Jaydee ameamua kuwafikia
na kuwaburudisha wapenzi wa kazi zake kwa njia nyingine.
Lady
Jaydee sasa anaanza sura mpya ya burudani kwa kuleta kipindi cha TV kiitwacho
DIARY YA LADY JAYDEE, ambacho kutaonekana katika kituo cha TV cha EATV
Diary
Ya Lady Jaydee itaonesha maisha na hadithi za kweli za Lady Jaydee kwa lengo la
Kuburudisha
kwa kuonesha mambo yate mazuri anayopitia au kuyaona Lady Jaydee
Kuelimisha
kwa kushiriki mambo ya kijamii
Kutia
moyo wengine wafuate ndoto zao kwa uadilifu
Kuongeza
Kipato kama msanii kwa kutangaza biashara mbalimbali na hatimae kudumisha ajira
binafsi kwa njia ya sanaa.
SHUKRANI
Lady
Jaydee anatoa shukrani kwa mashabiki kwa kuendelea kumpokea, jambo ambalo
linampa nguvu zaidi ya kufanya kaza.
pia
anashukuru sana vyombo vya habari na zaidi anawashukuru EATV na washirika wake
kwa kumpa nafasi ya kurusha kipndi chake kipya Diary Ya Lady Jaydee.
EATV
imekuwa mchango wa aina yake katika kuwakuza wasanii Tanzania.
WITO
Lady
Jaydee anatoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea kushirikiana na naye kwa
kila namna, ili kukuza na kuendeleza kipaji chake na sanaa ya muziki wa
Tanzania kwa ujumla wake.
Zaidi
anatoa wito kwa makampuni kishiriki na kuungana nae ili waweze kumpa nguvu
msanii, kutangaza biashara zao na kushawishi ajira katika fani ya muziki.
Na
mwisho Lady Jaydee anawaribisha wote kusikiliza CDs zake au kuburidika na kundi
lake la Machozi Band au kupata chakula ktk mgahawa wake wa kisasa Nyumbani Lounge
au ukiwa umepumzika nyumbani utazame kipindi chake Diary Ya Lady Jaydee ktk
EATV.
No comments:
Post a Comment