Leo
ilikuwa ndiyo siku ya hukumu dhidi ya watuhumiwa watatu wa mauaji ya
marehemu Swetu Fundikira aliyeuawa kwa kupigwa miaka miwili iliyopita.
Mara baada ya watuhumiwa hao kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa, ndugu na
jamaa wa marehemu waliangua kilio na wengine hadi kuzimia kama
walivyoshuhudiwa na paparazi wetu aliyeweka kambi mahakamani hapo.
Kushoto ni dada wa marehemu Rehema Fundikira, Hadija Mdemu shemeji wa
marehemu.
ndugu wakilia
ASKARI wa
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Sajent Rhoda
Robert, Koplo Ally Ngumbe na Mohamed Rashidi waliokuwa
wakikabiliwa na Kesi ya mauaji ya
Marehemu Swetu Fundikira imetolewa leo na Askari hao kuhukumiwa
Kunyongwa hadi kufa.
Hukumu hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na ndugu jamaa na
marafiki wa Swetu duniani kote ilitolewa leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania
jijini Dar es Salaam.
Washtakiwa hao watatu wametiwa hatiani baada ya kufanya kosa hilo siku
ya Jumamosi tarehe 23 Januari, 2010 kwa kumpiga bila huruma Swetu Fundikira
katika maeneo ya Kinondoni katika makutano ya barabara za
Mwinjuma na Kawawa jijini Dar es salaam mpaka kusababisha kifo
chake.
Marehemu Fundikira enzi za uhai wake.
picha kwa hisani ya globalpublishers.com
No comments:
Post a Comment