Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza
rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa-QT.
---------------
TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA MAARIFA (QT) NA KIDATO CHA NNE (CSEE)
ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012
---------------------
1.0 UTANGULIZI
Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini kote kuanzia tarehe 8-25 Oktoba 2012. Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi matokeo ya mitihani hiyo kama ifuatavyo :
2.0 MTIHANI WA MAARIFA (QT)
2.1 Usajili na Mahudhurio
Katika Mtihani wa Maarifa 2012 watahiniwa waliosajiliwa ni 21,310 ambapo wasichana walikuwa ni 13,134 na wavulana ni 8,176.
Jumla ya watahiniwa 17,137 sawa na asilimia 80.42 ya waliosajiliwa wamefanya Mtihani.
2.2 Matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT)
Watahiniwa 5,984 kati ya 17,137 waliofanya mtihani wamefaulu Mtihani wa Maarifa (QT).
3.0 MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012
Jumla ya vituo 5,058 vilitumika katika kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ambapo vituo 4,155 vilikuwa vya watahiniwa wa shule na vituo 903 vilikuwa ni vya watahiniwa wa kujitegemea.
3.1 Usajili na Mahudhurio ya Watahiniwa
(a) Watahiniwa Wote
Jumla ya watahiniwa 480,036 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wakiwemo wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67. Watahiniwa waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ni 456,137 sawa na asilimia 95.44. Watahiniwa 21,820 sawa na asilimia 4.55 ya watahiniwa wote waliosajiliwa hawakufanya mtihani.
(b) Watahiniwa wa Shule
Watahiniwa wa shule waliosajiliwa ni 411,230 wakiwemo wasichana 182,978 sawa na asilimia 44.50 na wavulana 228,252 sawa na asilimia 55.50. Watahiniwa wa shule waliofanya mtihani walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57. Aidha, watahiniwa 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, ugonjwa na vifo.
(c) Watahiniwa wa Kujitegemea
Watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa ni 68,806 wakiwemo wasichana 34,605 sawa na asilimia 50.29 na wavulana 34,201 sawa na asilimia 49.71. Watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,917 na wavulana 30,084 wamefanya mtihani wakati watahiniwa 7,730 sawa na asilimia 11.23 hawakufanya mtihani.
4.0 MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
(a) Watahiniwa wa Shule
Jumla ya watahiniwa wa shule 126,847 kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 46,161 na wavulana ni 80,686.
(b) Watahiniwa wa Kujitegemea
Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 16,112 kati ya watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani. Wasichana waliofaulu ni 6,751 na wavulana ni 9,361.
5.0 UBORA WA UFAULU KWA MADARAJA NA JINSI
Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 23,520 wamefaulu katika madaraja I – III ambapo kati yao wasichana ni 7,178 na wavulana ni 16,342.
Mchanganuo wa ufaulu kwa kila Daraja kwa jinsi kwa Watahiniwa wa Shule mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:
|
Idadi ya Wavulana
|
Idadi ya Wasichana
|
Jumla
|
I
|
1,073
|
568
|
1,641
|
II
|
4,456
|
1,997
|
6,453
|
III
|
10,813
|
4,613
|
15,426
|
I-III
|
16,342
|
7,178
|
23,520
|
IV
|
64,344
|
38,983
|
103,327
|
0
|
120,664
|
120,239
|
240,903
|
6.0 SHULE ISHIRINI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI
------------
Ubora wa ufaulu wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha “Grade Point Average” (GPA) kuanzia A = 1 hadi F = 5. Shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ziko 3,391. Shule ya kwanza hadi ya ishirini zimeainishwa kwenye Jedwali lifuatalo :
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
ST. FRANCIS GIRLS
|
90
|
MBEYA
|
2
|
MARIAN BOYS S.S
|
75
|
PWANI
|
3
|
FEZA BOYS S.S
|
69
|
DAR ES SALAAM
|
4
|
MARIAN GIRLS S.S
|
88
|
PWANI
|
5
|
ROSMINI S S
|
78
|
TANGA
|
6
|
CANOSSA S.S
|
66
|
DAR ES SALAAM
|
7
|
JUDE MOSHONO S S
|
51
|
ARUSHA
|
8
|
ST. MARY’S MAZINDE JUU
|
83
|
TANGA
|
9
|
ANWARITE GIRLS S S
|
49
|
KILIMANJARO
|
10
|
KIFUNGILO GIRLS S S
|
86
|
TANGA
|
11
|
FEZA GIRLS
|
49
|
DAR ES SALAAM
|
12
|
KANDOTO SAYANSI GIRLS SS
|
124
|
KILIMANJARO
|
13
|
DON BOSCO SEMINARY SS
|
43
|
IRINGA
|
14
|
ST.JOSEPH MILLENIUM
|
133
|
DAR ES SALAAM
|
15
|
ST.JOSEPH’S ITERAMBOGO SS
|
64
|
KIGOMA
|
16
|
ST.JAMES SEMINARY SS
|
44
|
KILIMANJARO
|
17
|
MZUMBE SS
|
104
|
MOROGORO
|
18
|
KIBAHA SS
|
108
|
PWANI
|
19
|
NYEGEZI SEMINARY SS
|
68
|
MWANZA
|
20
|
TENGERU BOYS SS
|
76
|
ARUSHA
|
7.0 SHULE KUMI AMBAZO HAZIKUFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
MIBUYUNI S.S
|
40
|
LINDI
|
2
|
NDAME S.S
|
41
|
UNGUJA
|
3
|
MAMNDIMKONGO S.S
|
63
|
PWANI
|
4
|
CHITEKETE S.S
|
57
|
MTWARA
|
5
|
MAENDELEO S.S
|
103
|
DAR ES SALAAM
|
6
|
KWAMNDOLWA S.S
|
89
|
TANGA
|
7
|
UNGULU S.S
|
62
|
MOROGORO
|
8
|
KIKALE S.S
|
60
|
PWANI
|
9
|
NKUMBA S.S
|
152
|
TANGA
|
10
|
TONGONI S.S
|
56
|
TANGA
|
8.0 TATHMINI YA UFAULU WA WATAHINIWA WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012
8.1 Tathmini
ya awali iliyofanyika kuhusu ufaulu wa watahiniwa katika shule
mbalimbali inaonesha kuwa shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo
zina mahitaji yote ya msingi ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu na
vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Aidha, shule zenye ufaulu wa chini
ni zile ambazo zina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
(i)
Baadhi ya shule za vijijini hazina kabisa walimu wa masomo ya Sayansi
na Hisabati na pia zina upungufu mkubwa wa walimu wa masomo mengine;
(ii) Kutokuwepo kwa maabara kwa shule zenye mikondo ya sayansi na pia kutokuwepo kwa maktaba kwa ajili ya kujisomea; na
(iii) Upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada. Katika baadhi ya shule uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:10.
8.2 Mkakati wa Serikali ni kuendelea kupunguza changamoto hizo kila mwaka ikiwa ni pamoja na kufanya mambo yafuatayo:
(i) Kuajiri walimu kila mwaka ili kuondoa upungufu uliopo katika shule zetu. Mwaka 2011/2012 Serikali iliajiri walimu wa sekodari 13,246 na mwaka huu wa fedha 2012/2013 imeajiri walimu 12,973 ambao
wamepangwa katika shule zenye upungufu mkubwa wa walimu. Ajira ya
walimu wapya mwaka huu umetuwezesha kuwa na wastani wa walimu 2-3 kwa shule. Hali hii itaendelea kuboreka kadri tunavyoendela kuajiri walimu.
(ii)
Kuboresha miundombinu iliyoko katika shule zetu ikiwa ni pamoja na
kujenga nyumba za walimu, madarasa na maabara. Mwaka 2012/2013 Serikali imepanga kuboresha miundombinu katika shule 264 zilizopo katika mazingira magumu ikiwemo miundombinu ya maabara na nyumba za walimu.
(iii) Kuendelea kutoa ruzuku ya Tsh 25,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka, ambapo asilimia 50
ya fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia na
kujifunzia ili kuziwezesha shule kununua vitabu pamoja na vifaa vingine
muhimu kitaaluma.
(iv) Wizara kuendelea kuzishauri Halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo baina ya shule na shule.
(v)
Wizara itaendelea kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa Shule pamoja na
kuwawezesha Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule kufanya ukaguzi wa
ndani katika Shule za Sekondari zilizo katika maeneo yao.
9.0 MATOKEO YA MITIHANI YALIYOZUIWA
Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya:
(a) Watahiniwa 28,582 wa
Shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada wanayodaiwa
pamoja na faini; na ikiwa hawatalipa katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.
(b) Watahiniwa 65 wa kujitegemea na 71
waliofanya Mtihani wa Maarifa (QT) mwaka 2012 bila ya kulipa ada ya
Mtihani hadi watakapolipa ada pamoja na faini. Ikiwa hawatalipa ada hiyo
katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.
10.0 MATOKEO YA MITIHANI YALIYOFUTWA
10.1 Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Udanganyifu
Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo yao yote ya mtihani kwa mujibu wa kifungu Na.52(b) cha Kanuni za Mitihani baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu katika mitihani ya Oktoba 2012. Kati yao, watahiniwa wa shule ni 624 na watahiniwa wa kujitegema ni 148 na watahiniwa wa Mtihani wa Maarifa (QT) ni 17.
Aina ya udanganyifu uliobainika na idadi ya watahiniwa husika ni kama ifuatavyo:
S/N
|
AINA YA UDANGANYIFU
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
(i)
|
Watahiniwa
kubainika kuwa na skripti zenye miandiko tofauti au kuwa na miandiko
tofauti katika skripti ya somo moja au zaidi ya moja.
|
04
|
(ii)
|
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mtihani wakiwa na ‘notes.’
|
170
|
(iii)
|
Watahiniwa kubainika kuwa na mfanano usio wa kawaida wa majibu.
|
590
|
(iv)
|
Watu kukamatwa wakiwafanyia watahiniwa wengine mtihani ‘impersonation”.
|
04
|
(v)
|
Watahiniwa kukamatwa na simu ndani ya chumba cha mtihani.
|
06
|
(vi)
|
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi wakibadilisha karatasi za maswali au skripti kwa lengo la kufanya udanganyifu.
|
15
|
|
JUMLA
|
789
|
10.2 Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Watahiniwa Kuandika Matusi Katika Skripti Zao
-----------
(i) Jumla ya watahiniwa 24 waliandika matusi kwenye skripti zao za masomo mbalimbali. Kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 5(13) cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka:
“Written
responses to any examination question which carry words, drawings or
pictures connected to sex or abusive language in such a way that it
becomes offensive shall consitute an examination offence and a candidate
who commits such an offence shall be punished by the Council.”
Kutokana na kosa hilo Baraza la Mitihani limefuta matokeo yao yote kwa mujibu wa Kifungu cha 6(2)(a) cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka:
“A candidate found to have committed an examination offence shall – (a) have his examination results nullified”
(ii)
Kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu (skripti)
kinaonesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Serikali haitaweza
kuwavumilia hata kidogo watahiniwa wa aina hiyo. Hivyo, Serikali
itaangalia hatua zaidi za kisheria za kuchukua dhidi ya watahiniwa wote
walioandika matusi.
Kwa mujibu wa kifungu Na. 6(2)(b)
cha Kanuni za Mitihani, watahiniwa wote waliobainika kufanya
udanganyifu katika mitihani au kuandika matusi katika skripti zao
hawataruhusiwa kufanya mitihani inayoendeshwa na Baraza la Mitihani la
Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja (01) kuanzia tarehe ya kutangazwa kwa matokeo.
11.0 KUANGALIA MATOKEO YA MTIHANI WA CSEE na QT, 2012
(a) Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), 2012 yanapatikana katika tovuti zifuatazo:
(b) Matokeo yanaweza kupatikana pia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15311. Jinsi ya kutuma ujumbe andika:
MATOKEOXNAMBA YA KITUOXNAMBA YA MTAHINIWA
(Mfano : matokeoxS0101x0503)
Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb)
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
18 Februari 2013