NAIBU WAZIRI WA
AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO AFANYA ZIARA ZA
KUSHTUKIZA KATIKA KITUO FOREPLAN CLINIC KINACHOMILIKIWA NA DK. MWAKA
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwasili katika kituo cha Foreplan Clinic kinachotoa tiba mbadala kilichopo
Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam
alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo jumatatu kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi Tiba Asilia na tiba Mbadala Dk.Paul Mhame kutoka wizara ya
Afya na Ustawi wa jamii.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akipokelewa na mmoja wa wauguzi
wa kituo hicho ambapo jina lake halikupatikana kwa haraka baada ya mkurugenzi
wa kituo hicho Dk. Mwaka Juma Mwaka kutokuwepo kwenye kituo chake cha Foreplan Clinic kilichopo Ilala Bungoni, jijini Dar es
Salaam
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wananchi waliofika kupata matibabu katika kituo cha Foreplan Clinic kuhusu huduma zitolewazo katika kituo hicho kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka.
Masaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya akimtolea ufafanuzi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala kuhusu huduma zitolewazo katika kituo cha Foreplan Clinic mara baada ya kuanza kukagua kituo hicho kinachotoa Tiba
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala akikikagua kifaa kinachotumika kufanyia vipimo kwenye kituo
cha Foreplan Clinic wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo jioni siku ya jumatatu
Hiki ndicho kifaa kinachotumika kupimia wagonjwa kwenye maabara ya kituo hicho cha Tiba Mnadala
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala akiwauliza maswali wasaizizi wa kituo hicho wakiongozwa na Bi Teddy L. Mbuya mara baada ya kukuta hari ya sintofahamu katika kituo hicho
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala akikagua moja ya dawa zinazotolewa kwa wangonjwa wanaokuja
kutibiwa kwatika kituohicho cha tiba Mbadala
Bi. Rozaria Antoni ambaye ni muhudumu wa dawa akikaa kimya baada ya kuulizwa maswali na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala na kukosa la kujibu.
Hizi ni dawa za asili zinazouzwa katika kituo hicho cha afya
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala akimpa maelekezo Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na mbadala Dk.Paul Mhame kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.
Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala leo
majira ya jioni amefanyaziara ya kushtukiza katika kituo kinachotoa tiba
mbadala cha Foreplan Clinic kinachomilikiwa na Dk. Mwaka
Juma Mwaka kilichopo Ilala Bungoni na kujionea hali halisi ya kituo
hicho. Mara baada ya kufika alianza kufanya ukaguzi kuanzia sehemu ya Mapokezi
mpaka kwenye vyumba vya matabibu lakini katika vyumba vyote hakuna daktari
aliyekuwa anatoa huduma.
Akizungumza na wagonjwa waliokuwa wakisubilia tiba alisema kuna
waliofika katika kituo hicho ili kutibiwa lakini kituo hicho hakina uwezo wa
kuwahudumia wagonjwa hao. Na kuwataka wagonjwa hao waende kwenye hospitali ili
wapate matibabu yanayoendana na magonjwa wanayoumwa.
Akizungumza msaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy
L. Mbuya alisema yeye hawezi kusema kuhusu kituo hicho maana yeye sio
msemaji mkuu bali alimwomba Naibu waziri kufanya ukaguzi katika kituo
hicho pamoja na kuwaliza maswali wahusika mbalimbali wa vitengo vya ktuo
hicho.
Baada ya ukaguzi wa kituo hicho Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amemwagiza Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na mbadala Dk.Paul Mhame ndani ya wiki moja kufanya ukaguzi kwa
kituo cha Dk. Mwaka na aletewe taarifa iliyokamilika kuhusu taaruma
yeke pamoja na washirika wake na pia dawa anazozitumia kama ni rafiki
kwa wananchi wanaotumia dwa hizo pamoja na kufanya ukaguzi wa vituo
vyote vinavyotoa tiba mbadala na tiba asilia kama Dk. Ndodi, Dk. Rahabu
nk. ili kuwabaini wanaowalaghai wananchi.
Pia
amesema Dk Mwaka Juma Mwaka amekuwa akijitangaza kupitia vyombo
mbalimbali hapa nchini ambavyo ni kosa la kutangaza kama unafanya kazi
za tiba tabibu. Alisema madaktari wana miiko na katika miiko hiyo ambayo
inatumika na mojawapo ikiwa ni kutojitangaza. Naibu waziri aliendelea
kusema kuwa Dk. Mwaka amekuwa akijiita Dokta na amekuwa akichambua mwili
wa binadamu kama vile ameusomea udakitari wakati sheria ya tiba asilia
na tiba mbadala hairuhusu watu wa tibaAsilia na Tiba Mbadala kutumia
maneno ya tiba ya kisasa.
Pia
Naibu Waziri amamtaka Dk. Mwaka Juma Mwaka kufika wizarani kesho saa
mbili asubuhi akiwa na nyaraka zake zote zinazohusu utoaji wa huduma ya
Tiba Mbadala kwani amekuwa akijiita majina ya tiba za kisasa na pia
kutibu kwa njia ya kisasa badala ya kutibu kwa njia ya Asilia au Tabibu.