Diwani Mkubwa Fella na wenzake waapishwa
2015 inakamilika huku tukishudia list
kubwa ya wasanii na watu wengine wenye umaarufu mkubwa wakijitosa kuivaa
siasa kwa miguu miwili.
Mkurugenzi wa kundi la ‘Mkubwa na Wanae’, Said Hassan maarufu kwa jina la Mkubwa Fella, aliingia
kwenye siasa na kugombea nafasi ya Udiwani ambapo kura zikamtosha na
akathibiotishwa kushika nafasi hiyo kwa miaka mitano ijayo…. leo ilikuwa
ndio siku yenyewe ambapo Mkubwa Fella ameungana na Madiwani wengine kuapishwa katika Ofisi za Halmashauri ya Temeke.
Mkubwa Fella baada ya kula kiapo cha kuwatumikia wakazi wa Kata ya Kilungule kwa ngazi ya Udiwani, alikuwa na hizi sentensi chache >>>“Kwanza
nashukuru Mungu pili Wadau wangu wote wa Kata yetu ya Kilungule, na
Tasnia yetu ya sanaa nawashukuru wasanii wote walionisapoti… pia
namshukuru sana rafiki yetu wa wasanii Mh Jakaya Kikwete na Rafiki yangu January Makamba“– Mkubwa Fella.
No comments:
Post a Comment