Sunday, June 28, 2015

FAIZA: NAJUTA KUVAA NGUO INAYOONESHA MAKALIO YANGU

Faiza Allly huyooo
Nguo aliyoivaa usiku wa June 13 kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro kwa nia ya kutoka kitofauti, imegeuka kuwa zimwi linalomtesa kiasi cha kumfanya apokonywe mtoto wake kwa amri ya mahakama na mzazi mwenzake, mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu. Faiza Ally anajuta!
“Siwezi kurudia kosa, nitakuwa... makini zaidi katika mavazi yangu,” Faiza aliliambia gazeti ambalo alienda kwenye ofisi zake kuelezea anavyojutia uamuzi huo uliomgharimu.

“Wasanii wengi ni wabunifu na hufanya mambo kwa nia ya kufurahisha mashabiki kama ambavyo amekuwa akifanya Joti kuvaa nguo za kike na kupaka rangi ya mdomo, hivyo mavazi yangu yalikuwa na lengo la kutoka tofauti mbele za mashabiki wangu, lakini kwa yaliyonikuta hasa kwenye vazi la Kili niliomba msamaha kwa jamii na bado naomba wanisamehe,” alisema Faiza huku akidaiwa kububujikwa na machozi.

“Hakika nimejikuta kwenye wakati mgumu na sivyo ambavyo baadhi ya watu wanafikiri. Hali hiyo ilinitokea nikiwa kule kule kwenye Kilimanjaro Music Award tena baada ya kubaini picha zinazoonyesha makalio yangu zimewekwa kwenye mitandao. Niliamua kuondoka haraka katika eneo hilo, kabla ya muda niliyokusudia,” aliliambia Mwananchi.


“Ingawa nimezoea kuvaa nguo fupi lakini sikupanga kuonyesha makalio, bahati mbaya ni kwamba ile nguo nilipoivaa awali kabla ya kuondoka nyumbani ilikuwa imekaa vyema. Nafikiri baada ya kukaa kwenye gari ilifumuka bila mimi kujua, hadi nafika ukumbini na kuingia pale kwenye zulia jekundu natembea kumbe huko nyuma mapaparazi wanapiga picha. Hakuna hata aliyenishtua. Napenda kuweka wazi naumizwa na watu ambao wanaendelea kusambaza hizo picha za makalio, watambue tu leo imenifika mimi lakini siku nyingine itawafika na wao maana sisi sote ni binadamu, tunafanya makosa kwa nyakati tofauti.”

“Namshukuru Mungu nimeweza kuhimili hali hii kwa kiasi fulani, maana naamini mtu mwingine angeweza hata kuamua kuwa mlevi au kuwa mbaya lakini nashukuru nina uamuzi wa kubadilika, nampenda mwanangu sitaki kuwa mbali naye.”

Sugu atoa ufafanuzi


Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu' wiki hii amesimama Bungeni na kulitokea Ufafanuzi swala la Mahakama kumpa haki ya kumlea mtoto kutoka... kwa Mama yake Mzazi Faiza Ally..

baba na mwana....


“Mheshimiwa naibu spika, kwa vile masuala haya binafsi mimi na mzazi mwenzangu na binti yetu, yameletwa hadharani mbele ya bunge tukufu, kwa vile masuala haya ni binafsi na ya kiunyumba yamevishwa joho la haki za wanawake na watoto na tuhuma nzito kutolewa juu yangu, mimi nalazimika kwa masikitiko makubwa na moyo mmzito kabisa kuyazungumzia hadharani mbele ya bunge lako tukufu,” alisema Sugu.

“Mheshimiwa naibu spika binti yangu Sasha Desteria anaishi Dar es Salaam na mama yake tangu alivyozaliwa tarehe 26 September 2012 na katika kipindi chote hicho mimi nimempelekea mama yake takriban shilingi 500,000 kwa mwezi kwaajili ya matunzo ya binti yetu kila mwezi. Aidha tangu awe na umri wa miaka miwili mimi nimemlipia Sasha ada yake ya shule takribani milioni 3 kila mwaka ambayo ni shilingi 750,000 kwa semester. Malipo haya ni nje ya fedha za nguo, chakula, vifaa vya kuchezea watoto pamoja na kulipia gharama za television za watoto ya cartoon katika kipindi chote tangu binti yangu alipozaliwa.

Mheshimiwa naibu spika, mzazi mwenzangu anayedaiwa kuwa mwanamke mnyonge na mheshimiwa Mlata, ni mwanamke anayejulikana katika kumbi za starehe karibu nchi nzima kwa kutokuwa na haya mbele ya hadhara wala mbele ya jamii. Ni mwanamke katika sherehe za tuzo za Kilimanjaro Music Awards zilizofanyika jijini Dar es salaam mwezi mmoja uliopita, alivalia nguo ambazo ziliacha sehemu zake za siri hadharani ili mpita njia azione. Picha zake katika mavazi hayo zilisambaa katika mitandao ya kijamii ya kuleta fedheha kubwa kwangu binafsi na bila shaka kwa watanzania wote wanaojali maadili katika masuala ya mavazi ya hadharani.

Kabla ya hapo picha zake nyingine wakati amevalia nepi ya mtoto yaani Diapers na kisha kusambaza katika mitandao ya kijamii. Kama angetaka mheshimiwa Mlata angeweza kupata taarifa hizi kabla ya kurusha tuhuma nzito ndani ya bunge tukufu,” alisisitiza Sugu.

Pia Sugu alizungumzia jinsi alivyolipeleka suala lake mahakamani mpaka mahakama kutoa uamuzi wa kutaka Faiza amkabidhi mtoto kwa Sugu.

Sugu akicheza na mtoto wake Sasha

'Enzi' za mapenzi yao

“Mahakama ya mwanzo Manzese iliridhika na ushahidi wangu kwamba mzazi mwenzangu hakuwa na maadili yoyote ya kuweza kumlea mtoto wetu. Mahakama hiyo iliamuru kwamba binti yetu Sasha Desteria akabidhiwe kwangu ili niweze kumlea katika mazingira ya maadili ya usawa kwa mtoto na kwa umri wake. Hivyo mheshimiwa naibu spika kile ambacho kimedaiwa na mheshimiwa Mlata cha uporaji wa mtoto kiukweli ni amri halali ya mahakama ya Manzese iliyotolewa baada ya kusikiliza pande zote kuzingatia ushahidi uliotolewa.”

Hata hivyo Sugu alisema bado hajamchukua mtoto huyo kutoka kwa Faiza, na kwamba kuna uwezekano wa kufanyika mazungumzo ya kifamilia kulimaliza suala hilo kwa amani.

Mwisho Sugu alipomaliza Kuongea Alionekana Akitokwa na Machozi Usoni Mwake..

kilichompoza Faiza


MAFURIKO YA LOWASSA YAHAMIA JIJINI DAR, AKOMBA UDHAMINI WA WANACCM 212, 150

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akifurahia jambo wakati Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Ramadhan Madabida (hayupo pichani) akizungumza jambo, wakati Mh. Lowassa alipofika ofisi ya CCM Mkoa huo, Mtaa wa Lumumba, leo Juni 27, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Ramadhan Madabida akizungumza jambo kumuhusu, Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (kulia), wakati alipofika kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam kusaini kitabu leo Juni 27, 2015, wakati akiwa katika ziara yake ya kutafuta saini za WanaCCM wakumdhamini ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 212, 150 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi ya WanaCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakimshangia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Ramadhan Madabida (hayupo pichani) .
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, Mkewe Mama Regina Lowassa pamoja na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu wakiwa sambamba na wanaCCM wengine wakati wakiwasili kwenye Ofisi za CCM Tawi la Ilala Kota, Mchikichini jijini Dar leo, Juni 27, 2015.

Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Ernest Chale akikabidhi fomu za Wadhamini kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa leo Juni 27, 2015. Jumla ya WanaCCM 44,299 wa Wilaya ya Ilala Wamemdhamini Mh. Lowassa ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.

Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu akiwasalimia wananchi wake.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akiwasalimia wanaCCM wa Wilaya ya Ilala, Jijini Dar.





Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia WanaCCM wa Wilaya ya Ilala, waliokusanyika kwa wingi kwenye Uwanja wa CCM Tawi la Kota, Mchikichini Jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2015.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Assah Simba akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa kuwasalimia na kuwashukuru wanaCCM wa Wilaya ya Ilala waliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni 27, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na kuwashukuru wanaCCM wa Wilaya ya Ilala waliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni 27, 2015.
Sehemu ya Vijana wa CCM wakifatilia kwa makini salam za Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya kinamama wenye ulemavu wa Miguu waliokuwepo kwenye hadhara hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na kinamama wa CCM Wilaya ya Ilala.
Umati wa Watu ukiwa umejipanga barabarani kumuona Mh. Lowassa akipita kuelekewa Ofisi ya CCM Wilaya ya Temeke, Jijini Dar leo Juni 27, 2015.
MwanaCCM Wilaya ya Temeke akisini fomu ya Udhamini mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa.
Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke, Robert Kerenge akikabidhi fomu za Wadhamini kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa leo Juni 27, 2015. Jumla ya WanaCCM 72, 100 wa Wilaya ya Temeke Wamemdhamini Mh. Lowassa ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akisalimia wananchi wake.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na kuwashukuru wanaCCM wa Wilaya ya Temeke kwa kumdhamini ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Jiji la Dar leo ilikuwa ni shangwe tupu kwa kila alieweza kumuona Mh. Lowassa akipita kwenye njia zilizo jirani na maeneo yao ya kazi.
Dereva akipuliza tarumbeta kuonyesha furaha yake kwa Mh. Lowassa.
Mh. Lowassa akiwasili kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni, Mkajuni jijini Dar.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Mtoto Shadrack Samuel (5) alitaka kumsalimia na kumuona leo Juni 27, 2015. 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru leo Juni 27, 2015. 
Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan akisalimia wananchi wake.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Dodoma akiwasalimia wanaCCM wa Kinondoni jijini Dar.
Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akizungumza machache na WanaCCM wa Wilaya ya Kinondoni, Waliomdhamini Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa. ambapo kwa wilaya ya Kinondoni amepata udhamini wa wanaCCM 95, 251 na kufanya jumla kuu kuwa 212, 150 na kuifanya Dar es salaam kuwa Mkoa wa kwanza kuwa na idadi kubwa ya WanaCCM waliomdhamini Mh. Lowassa.
Wadau Mkutanoni.

Mama Regina Lowassa akisalimia wanaCCM wa Kinondoni.
Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisani fomu ya udhamini mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono mgombea huyo. zoezi hili limefanyika jioni ya leo Juni 27, 2015 kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni Jijini Dar. ambapo kwa wilaya ya Kinondoni amepata udhamini wa wanaCCM 95, 251 na kufanya jumla kuu kuwa 212, 150 na kuifanya Dar es salaam kuwa Mkoa wa kwanza kuwa na idadi kubwa ya WanaCCM waliomdhamini Mh. Lowassa.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akizungumza jambo mbele ya umati wa WanaCCM wa Wilaya hiyo leo Juni 27, 2015.
WanaCCM wa Kinondoni wakisikiliza kwa Makini Salamu za Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na kuwashukuru wanaCCM wa Wilaya ya Kinondini Jijini Dar es Salaam kwa kumdhamini ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Jumla ya WanaCCM 212, 150 wamdhamini Mh. Lowassa jijini Dar.