Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akihutubia wanachama
wa CCM na wananchi katika Uwanja wa CCM mkoani Manyara baada ya kupokea orodha
ya majina 42,405 waliomdhamini kugombea urais
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akipokea orodha ya
majina 42,405 kwa Katibu wa CCM Wilaya Manyara, Daniel Ole Porukwa, waliomdhamini kugombea urais
Lowassa akisalimiana na wananchi wa Manyara.
Msafara huo
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (katikati),akifurahia
jambo katika Mkutano wa wanachama cha
Mapinduzi (CCM) wakati wa kupokea orodha ya majina 42,405 waliomdhamini
kugombea urais leo.
Msafara wa Lowassa.
Kada wa CCM Mkoani Manyara, akitembea kwa mikono kuonyesha
kuanza safari ya matumani kuanza rasmi,wakati wa kumkabidhi Waziri Mkuu wa
zamani,orodha ya majina 42,405 waliomdhamini kugombea urais
Akipeana mkono na kada huyo.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
On Thursday, June 25, 2015
No comments
Makamu wa Rais wa Burundi, Gervais Rufyikiri ameondoka
nchini humo kwa kile alichodai kukimbia kusumbuliwa baada ya kupingana na Rais Pierre
Nkurunzinza wa Burundi kutaka kuongeza kipindi cha tatu cha kuitawala nchi
hiyo.
Rufyikiri ameiambia kituo cha Televisheni cha France24, kuongeza
muhula wa tatu kwa Rais itakuwa ni kinyume cha matakwa ya katiba.
Aidha Msemaji wa serikali ya Burundi amekanusha madai hayo na kusema kuwa Rufyikiri,
amesafiri nje ya nchi kwa shughuli za kikazi.
Bwana Rufikiri amesema amekimbilia usalama wake akidai kuwa maisha yake yamo hatarini.
Msemaji huyo wa serikali amesema iwapo bwana Rufikiri ametoroka Burundi ni kwa maslahi yake mwenyewe wala hakuna yeyote aliyemtishia maisha yake.
Bwana Rufikiri amesema amekimbilia usalama wake akidai kuwa maisha yake yamo hatarini.
Msemaji huyo wa serikali amesema iwapo bwana Rufikiri ametoroka Burundi ni kwa maslahi yake mwenyewe wala hakuna yeyote aliyemtishia maisha yake.
Pia taarifa zinasema kuwa mbali na Makamu huyo wa Rais
lakini pia Spika wa Bunge la Burundi, Pie Ntavyohanyuma hayupo nchini humo na inasemekana amekwenda Ubelgiji kwa matibabu.
Spika huyo pia anadaiwa kupingana na hitaji hilo la Rais
Nkurunzinza la kugombea tena.
Tangu mwezi Aprili mwaka huu Burundi inakabiliwa na
maandamano ya mara kwa mara na watu kufa kutokana uamuzi wa Rais Nkurunzinza
kutaka kugombea tena katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.
On Thursday, June 25, 2015
No comments
Mwandishi wa habari Edson Kamukara (pichani) amefariki dunia leo.
Taarifa
zilizotufikia zinaarifu kuwa Mwandishi huyo aliyepata kuandikia gazeti
la Tanzania Daima na baadae kuhamia Mwanahalisi amefikwa na umauti baada
ya kulipukiwa na jiko la gesi nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es
Salaam.
Aidha
habari kutoka kwa majirani zinaarifu kuwa Kamukara amerejea kutoka
Bukoba, na alijisikia vibaya wakati anaenda dukani kununua dawa
akaanguka na majirani kusaidia kumpepea na baade kupelekwa kwake ambako
alipumzika hadi alipopata nguvu na kuamua kujiandalia chakula na ndipo
ajali hiyo kumfika na kugharimu maisha yake.
Father Kidevu Blog inatoa pole kwa wote waliofikwa na Msiba huo na italeta taarifa kamili hapo baadae.
Edson
(kushoto) enzi za uhai wake akiwa na waandishi wenzake. Kutoka Kulia
Mpigapicha Michael Matemanga, Mary Edward, Abdalla Bawaziri na Kurwa
Karedia.
Edson (wapili kulia) akiwa na wanahabari wenzake enzi za uhai wake.
No comments:
Post a Comment