full kujiamini...safi mama...umethubutu na umeweza...
katika wadada wanaojiamini mjini si mwingine ni Sinta....daaa..namkubali ile mbayaaa alipoingia yeye tuuuu shughuli ilinogajeee...coz alichelewa alisema alikuwa kwenye kikao, ila alijitahidi kadiri ya uwezo wake na kuwakilisha...upoo juu mama, hapa akiwa na warembo wa Kidoti waliovaa baadhi ya nywele zake.
Carren Mgonja
MWANAMITINDO anayetamba kwa
sasa hapa nchini Jokate Mwegelo ‘Jokete’ jana amefungua rasmi kampuni yake
yenye Chapa ya Kidoti inayojihusisha na masuala mbalimbali ya Urembo.
Akizungumza na jijini Dar es
Salaam Jokate alisema, ameamua kuanzisha kampuni hiyo ambayo kwa sasa imeanza
na uuzaji wa Nywele na baadae ataendelea na mambo mengine mbalimbali ya urembo
ikiwemo nguo na vifuasi vya urembo na vipodozi.
Alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 2011 na kuzinduliwa rasmi jana, kwa nia ya kubadilisha mtazamo mzima wa tasnia ya mitindo na kusema kuwa Chapa hii itasheheni bidhaa mbalimbali zikiwemo nywele za sanisi.
“Katika nywele hizi tuna staili nane tofauti kwa kuanzia ambazo tumezipa majina ya reysa, dessy, fania, Whitney curls, jokate, Myra, Selita na nayomi.
Napenda kusema what is fashion without hair? Hizi nywele mabibi na mabwana zimefanyiwa utafiti kwa takribani mwaka mzima ili kuhakikisha tunasaidia kuboresha mitazamo ya nywele za kuongezea kwa wasichana, wadada mpaka akina mama. Ni nywele safi zenye ubora wa hali ya juu, hazifungamani, ziko katika mawimbi, rangi na style za kisasa, ni nyepesi, rahisi kusukia, zinadumu kwa muda mrefu na muhimu kuliko yote zinapatikana kwa bei nafuu sana. Sasa mwanamke anaweza kupendeza kichwani kwa style tofauti bila ya kuharibu sana bajeti yake ya mwezi ama mwaka na kila paketi ina ujazo wa kutosha kichwa kizima. Ni bidhaa inayomfaa mwanamke wa kisasa.
Utengenezwaji wa nywele hizi nimezisimamia mwenyewe nikiongozwa na watengenezaji wangu, kama binti ninayejiamini na kupenda kupendeza, ninayetazamwa na watanzania kwa uwigni wao na wengi kuulizia style mbalimbali ninazofanya ni nimepata faraja kubwa sana kuweza kutengeza nywele hizi kwa ajili ya kina dada wenzangu, wasichana na akina mama.
Nywele hizi zinakuhamasisha wewe u-ainishe urembo wako, ujitambue kupitia nywele hizi hizi vile vile tunasema katika packeti ya nywele mmoja unaweza kupata staili kibao yaani nywele mmoja staili kibao. Tumezoa kuona weaving kwa mfano zikitumiwa kusukiwa tu lakini Leo hii tunakwambia kupitia hio nywele unaweza pia ukapata staili za kubana na hivyo kubadilisha muonekano wako Mara nyingi uwezavyo. Mambo ya Kidoti hayo

“Nywele hizi
zinamfaa mtu yoyote,na ninaimani kubwa wadau wangu watazipenda kwa kuwa nywele
moja mitindo tofauti na leo zinaanza kutoka na katika saluni mbalimbali
zitakuwepo”alisema Jokate na kuongeza kuwa nguo za Kidoti zitatambulishwa rasmi
katika soko mwakani zikifuatiwa na vifuasi vya urembo pamoja na vipodozi.
“Msingi wa ubunifu
wangu ni mchanganyiko wa kipekee wa kiini cha utamaduni wa Kiafrika pamoja na
mitindo ya kisasa ulimwenguni kwa ajili ya wanawake na wanaume wa kisasa.
Nachukua muda kusoma mienendo ya soko na kujua wateja wangu wanataka nini katika
maisha yao na hivyo kutumia ubunifu wangu katika
mitindo kuwasaidia kuyafikia malengo yao,”
alimalizia Jokate.
Aliongeza kuwa harakati
ya Kidoti inaendeshwa na timu ya vijana wabunifu na pamoja na kwamba shughuli
za Kidoti zinaendeshwa kutoka Dar es Salaam, chapa hii ni ya kiulimwengu zaidi
na kuwaomba wadau mbalimbali kumpa sapoti juu ya bidhaa hiyo.
No comments:
Post a Comment