utamtakaaaaa.....
SERENGETI Fiesta 2012, nani anayeifanya iwe na joto kali ile
mbaya? Kuna ‘mnyamwezi’ mmoja mwenye midevu na mwili mkubwa, anayepiga Hip hop
ya kigumu anakwenda kwa jina la Rick Ross. Nani mwingine? Ndiyo huyo.
Jamaa anatua Dar es Salaam keshokutwa kwa ajili ya show ya
kilele cha Serengeti Fiesta 2012, kwenye viwanja vya Leaders Club, mwishoni mwa
wiki.
Akizungumzia ujio wa msanii mkubwa kama huyo katika
mahijiano maalum jijini Dar es Salaam jana, meneja wa bia ya Serengeti bw.
Allan Chonjo amesema tamasha la Serengeti Fiesta limekuwa likifanya vizuri sana
katika mzunguko wake na kwamba watanzania wamekuwa wakifurahia uwepo wa tamasha
hilo kutokana na mafanikio mbalimbali ambayo wamekuwa wakiyapata kila ilipofika
msimu wa Serengeti Fiesta “mwaka huu
tutakuwa na Rick Ross na kwamba watanzania waendelee kujenga imani na Kampuni
ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager, kwani kila kilele cha msimu wa tamasha hili
ndio mwanzo wa maandalizi ya msimu unaofuata”.
Rick Ross ambaye ni mmoja kati ya wasanii wanaotamba sana
katika miondoko ya kurap (hip hop) nchini marekani, atawasili hapa nchini siku
ya alhamisi tayari kabisa kutumbuiza katika maadhimisho ya kilele cha tamasha
la Serengeti Fiesta siku ya jumamosi mwishoni mwa wiki hii.
Msimu wa Serengeti fiesta ulianzia katika mikoa ya
Kilimanjaro, Tanga, Musoma, Shinyanga, Mwanza, Tabora, Singida, Dodoma,
Morogoro, Mbeya na Iringa ambapo wakazi wake walipata burudani na ladha ileile
ya bia ya Serengeti kabla ya kufikia mwisho wa msimu wake wiki hii.
Wasanii waliburudisha katika tamasha la Serengeti Fiesta
nyanda za juu kusini ni pamoja na Inspector Haroun, Juma Nature, Roma
Mkatoliki, Linah, Amini, Supa nyota Serengeti fiesta 2012 na wengine.
Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani
wanatarijwa kumiminika katika viwanja vya Leaders Club kushuhudia burudani
mbalimbali zitakazotolewa na wasanii wa hapa nchini, kabla ya kilele cha msimu
wa ‘BHAAAS’ kumaliziwa na msanii Rick Ross na kundi lake kwa kiingilo cha
shilingi 20,000/= za kitanzania kwa wale watakaonunua tiketi zao mapema na elfu
25,000/= kwa wale watakaonunu tiketi getini.
Katika tamasha la Serengeti Fiesta msimu wa uliopita
uliokuwa ukijulikana kama ‘Haina Majotroo’ Kampuni ya bia ya Serengeti
iliwaleta wasanii maarufu ambapo msanii wa muziki wa raga ‘Shaggy’ alitumbuiza
katika uzinduzi wa msimu huo jijini Mwanza na msanii nyota kutoka nchini
Marekani Ludacris alihitimisha msimu wa kwa kuwaburudisha wakazi wa jiji la Dar
Es Salaam na majirani zake kama kawaida katika viwanja vya Leaders Club.
Umaarufu wa tamasha Serengeti Fiesta umekuwa ukitengeneza
ajira mbalimbali za muda mfupi na kudumu, na pia nyingine zikianzishwa kupitia
Serengeti Fiesta katika maeneo yote ambayo tamasha hilo lilipata kupita
zikiwemo kuibuliwa kwa wasanii chipukizi na baadaye kujitegemea kimuziki,
kujengeka kwa majina ya wasanii mbalimbali ambao hawakupata kufahamika zaidi
kwa mashabiki wa muziki pamoja na kuibuka kwa wasanii wa filamu kupitia tamasha
hili la Serengeti Fiesta,linalodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia
bia ya Serengeti Premium Lager.
HUYU NDIYE RICK ROSS:
Oktoba 14 mwaka jana, rapa Rick Ross alipata ugonjwa wa moyo
mara mbili kwa siku moja, mara ya kwanza alipata shambulio hilo la moyo asubuhi
kabla ya kurejea mara ya pili wakati wa jioni akiwa ndani ya ndege.
Rafiki wa karibu wa Ross alimtaarifu mpenzi wake kuwa moyo
wa rapa huyo umesimama na wataalamu wanahangaika kuhakikisha hapotezi maisha.
“Madaktari hawajasema kama amekufa, hivyo bado tuna
matumaini, tuendeleeni kumuomba Mungu,” anasema rafiki huyo, maombi hayo
yalionekana kusaidia na hali kuwa nzuri.
Shambulio hilo la moyo la pili lilimpata jioni hiyo ya
Oktoba 14 baada ya lile la kwanza la asubuhi, akiwa ndani ya ndege ya Delta Airlines,
wahudumu wa ndege hiyo na rubani waliamua kutua kwa dharura Fort Lauderdale na
kupatiwa matibabu katika hospitali ya uwanja huo wa ndege na hali yake kuwa
nzuri, kisha kukodiwa ndege ya binafsi kuendelea na safari yake.
Mwenyewe alituma picha za video kwenye akaunti yake ya
mtandao wa Twitter, akisema kuwa hali yake iko sawa: “Niko sawa,” anasema rapa
huyo.
Rick Ross, au The Boss jina lake halisi ni William Leonard
Roberts II, alizaliwa Januari 28 mwaka 1976, eneo la Coahoma County,
Mississippi nchini Marekani.
Jina la Rick Ross, alilipata kutoka kwa askari wa barabarani
aliyekuwa akihusika na kudhibiti dawa za kulevya (Ricky Ross), ambapo alimshitaki
rapa huyo na kulipwa dola milioni 10 kwa kutumia jina lake.
Kabla ya kupigwa faini ya dola milioni 10, Jay-Z alitakiwa
kutoa ushahidi juu ya jina hilo kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa
kampuni ya Def Jam, ambako Ross alikuwa ameingia mkataba wa kufanya kazi katika
studio hiyo.
Baadaye alikataa taarifa za kuwa ana mpango wa kubadilisha
jina hilo, badala ya Rick Ross kuwa Ricky
Rozay, kutokana na tatizo lililotokea la kupigwa faini, lakini alipinga vikali
jambo hilo.
Baada ya kuingia mkataba na kampuni ya Suave House Records,
iliyokuwa ikitumiwa na 8Ball & MJG, baadaye aliingia mkataba mwingine na
Slip-n-Slide Records, iliyokuwa chini ya Def Jam tangu mwaka 2006.
Albamu yake ya kwanza aliitwayo Port of Miami iliachiwa
Agosti mwaka 2006 na kushika nafasi za juu kwenye chati za Billboard kati ya
albamu 200.
Albamu hiyo iliuza nakala 187,000 katika wiki ya kwanza, na
kushirikishwa katika wimbo wa DJ Khaled Born-N-Raised na Holla at Me.
Machi mwaka 2008, alitoa albamu yake ya pili iliyoitwa
Trilla, ambapo moja ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ilikuwa ni Speedin,
aliyomshirikisha R. Kelly na kufanya vizuri.
Nyingine ilikuwa The Boss aliyompa shavu T-Pain ilishika
nafasi ya 17 katika nyimbo 100, pamoja na Here I Am aliyofanya na Nelly na
Avery Storm.
Katika kituo cha luninga cha MTV walimtaja kama rapa namba
nne katika marapa 10, katika kipengele
chao cha Hottest MCs In The Game, huku akitoa ‘single’ yake ya This Is The Life
akimshirikisha Trey Songz.
Albamu ya Deeper Than Rap ilitoka mwaka 2009 na wimbo wa
Valley of Death ulifanya vizuri katika albamu hiyo, kisha waliachia albamu
nyingine ya Teflon Don Julai 6, mwaka 2010.
Wimbo uliofanya vizuri katika albamu hiyo ya Teflon Don
ulikuwa ni Super High, akimshirikisha Ne-Yo na mwigizaji Stacey Dash akionekana
kwenye video ya wimbo huo.
Kibao cha pili kilichoachiwa kutoka kwenye albamu hiyo ni
Live Fast, Die Young, ambacho kilitayarishwa na rapa Kanye West, ambaye pia
alishirikishwa na kushika nafasi ya pili katika chati za Billboard katika
nyimbo 200 na kuuza nakala 176,000 kwa wiki ya kwanza.
Novemba mwaka 2010, rapa P Diddy alitangaza kupitia mtandao
wa kijamii wa YouTube, kwamba anatarajia kufanya albamu ya pamoja na Ross
ambayo itaachiwa mwaka 2011 na kibao kimoja cha Another One kiliachiwa katika
mradi huo wa pamoja.
Nyota huyo alitangaza kuwa Desemba 13 mwaka huu, ataachia
albamu ya God Forgives, I Don't, lakini
Novemba 17 mwaka huu, alitangaza
kusogeza mbele albamu hiyo hadi mwakani.
Ross alikamatwa na polisi akiwa na silaha na bangi Januari
mwaka 2008, DJ Vlad alimfungulia kesi rapa huyo akimshutumu kumpiga.
Vlad anasema kuwa Ross alipanga ugomvi huo na watu wakampiga
mjini Houston, Texas.
Machi 26 mwaka 2011, alikamatwa na polisi eneo la Shreveport
akiwa na bangi, na taarifa ya polisi zilisema kuwa bangi hizo zilikutwa kwenye
chumba chake.
Julai mwaka 2008, mtandao mmoja ulitoa taarifa kwamba Ross,
alikuwa ofisa wa kukusanya mapato, mjini Florida, ikabandikwa picha yake akiwa
amevaa sare za wakusanya mapato, lakini alikanusha na kusema picha hiyo haikuwa
yake.
Baadaye Ross alikubali kuwa alikuwa akikusanya mapato miaka
ya 90 katika mji huo wa Florida, hiyo ilitokana na kupatikana kwa ushahidi wa
kutosha picha yake akiwa amevaa mavazi ya watoza ushuru na jamii kuiona picha
hiyo.
Januari mwaka 2009, Ross alianzisha ugomvi na rapa 50 Cent,
akisema Cent alimuangalia vibaya wakati wa onyesho la tuzo za BET, lakini 50 Cent anasema hakumbuki kama
alimuona Ross katika hafla hiyo ya kukabidhi tuzo.
Baadaye, taarifa
zilisema kuwa Ross ‘alimchana’ Cent katika kibao chake cha Mafia Music, siku
chache baadaye 50 Cent, aliachia kibao kiitwacho Officer Ricky (Go Head, Try
Me), akimjibu Ross maneno aliyoyasema kwenye kibao cha Mafia Music.
Kabla ya 50 Cent kwenda Venezuela, aliachia video ya Warning
Shot, ambayo alianza kwa kumponda Ross, katika mashairi ya wimbo huo, kisha
baadaye 50 Cent aliachia katuni za Officer Ricky.
Februari mwa huo wa 2009, 50 Cent aliachia video nyngine
akimfanyia mahojiano Tia, mama wa mmoja wa watoto wa Ross, ambaye aliweka wazi
kuwa Ross alikuwa ofisa wa kukusanya ushuru na kuongeza kuwa maisha yake yote
anayoishi ni ya uongo.
Alhamisi, Februari 5, mwaka 2009, rapa aitwaye Game, ambaye
alikuwa na ‘beef’ na 50 kwa muda mrefu, akihojiwa kwenye kituo cha KUBE,
akiulizwa kuhusu ugomvi wa wawili hao, alijibu kuwa mambo yanaonekana si mazuri
kwa Ross.
Game aliamua kumsaidia Ross akianzia kwenye wimbo wa kwenye
albamu ya Deeper Than Rap, wimbo wa In Cold Blood, ambapo video yake
ilimuonyesha 50 Cent akiomboleza makaburini na Ross kutangaza amemaliza kipaji
cha 50 Cent.
Ross alitoa wimbo mwingine Push ‘Em Over The Edge ‘akimdiss’
50 Cent, ambaye na yeye aliachia video iitwayo A Psychic Told Me, akimponda DJ
Khaled na Februari 12, 2009, alimjibu Ross na kibao cha Tia Told Me,
akimshirikisha Lloyd Banks, alitoa nyingine kama Officer Down na Somebody
Snitched.
Kwa muhtasari huyo, ndiye Rick Ross atakayefanya Serengeti Fiesta
2012 iwe taamu mpaka bhaaaaaas!
WASIFU WAKE:
JINA: William Leonard Roberts II
KUZALIWA: JanuarI 28, 1976 (35)
ALIPOZALIWA: Carol City, Florida, Marekani
KAZI: Muziki/Rapa
AINA YA MUZIKI: Hip hop, Mafioso Rap, Pop
ALBAMU ALIZOTOA:
2006: Port of Miami
2008: Trilla
2009: Deeper Than Rap
2010: Teflon Don
2012: God Forgives, I Don't [42]
No comments:
Post a Comment