Katika taarifa kwa taifa, makamu wa rais wa
Venezuela Nicholas Marduro ametangaza kufariki dunia kwa rais Hugo
Chavez, 58, kufuatia kuugua muda mrefu maradhi ya Saratani.
Rais Chavez ametoweka katika hadhira ya nchi hiyo kwa muda mrefu ambapo alikuwa anapokea matibabu nchi jirani ya Cuba.
Alirejea , mjini Caracas mnamo Februari 18 kwa
mara ya kwanza tangu maradhi yake yamzidie ambapo alipelekwa hospitali
ya kijeshi kuendelea kupokea matibabu. Hata hivyo maelezo zaidi
hayakutolewa juu ya afya yake. Waandamanaji waliandamana katika mji mkuu
Caracas mwishoni mwa-juma wakidai kuwa watu wa Venezuela wanapaswa
kupewa habari zaidi kuhusu afya ya rais wao.Rais Chavez ametoweka katika hadhira ya nchi hiyo kwa muda mrefu ambapo alikuwa anapokea matibabu nchi jirani ya Cuba.
Ujumbe wa Jeshi:
Taarifa kutoka kwa jeshi imesema kuwa wataendelea kuilinda hadhi ya nchi na kuimarisha usalama. Pia jeshi limeahidi kuendelea kuwa waaminifu kwa makamu wa rais Nicholas Marduro na wakatoa wito kwa raia kuwa watulivu.
Wasifu wa Chaves:
Hugo Chavez alijitosa katika siasa za
Venezuela mnamo Februari 1992 akiwa luteni katika jeshi. Aliongoza
mapinduzi dhidi ya rais wa wakati huo Carlos Andres Perez.
Lakini
kutokana na kukosa usaidizi wa kutosha wa kijeshi, Chavez na wanamgambo
wenzake walishindwa kunyakua madaraka hayo. Alikiri kushindwa na
aliwekwa korokoroni.
Aliingia uongozini baada ya ushindi mkubwa
ulioviondosha vyama vya kisiasa wakati huo. Katika kuapishwa kwake mnamo
February 1999, Hugo Chavez alitangaza wazi kwamba mipango yake ya
mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi sio kampeni tu. Alitimiza ahadi yake
na kuiongoza nchi hiyo katika mabadiliko ambayo hayakuwahi kushuhudiwa
katika muda wa miongo kadhaa. Alibadili muundo wa bunge na kulifanya
kuwa la kikatiba, ambalo liliiunda katiba mpya baada ya kura ya maoni
iliyoidhinishwa na 88% ya wapiga kura.
Rais Chavez alitaifisha rasilimali ukiwemo
utajiri wake mkubwa wa mafuta. Sera kama hizi zilimfanya azozane na
kampuni za kimataifa za mafuta, lakini alipata uungwaji mkono mkubwa wa
watu maskini.
Chaves na jamii ya kimataifa:Kutokana na urafiki wake na viongozi wa mlengo wa kushoto kama vile rais wa Cuba, Fidel Castro, ambaye walikuwa na uhusiano wa karibu aligongana kidiplomasia na Marekani, ambayo ni mshirika wake mkuu wa kibiashara.
Chavez alipendwa nyumbani na wafuasi wake lakini alipingwa na baadhi ya watu nchini humo na katika nchi za nje. Alionekana sio tu kama bingwa wa jamii maskini lakini pia kama muingiliaji wa siasa za nchi jirani. Katika miaka ya hivi karibuni alilenga kukabiliana na masuala ya ndani ya Venezuela, kama uhalifu, kuinua uchumi wa nchi na kukabiliana na rushwa.
No comments:
Post a Comment