Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema.
……………………………………………………………….
1.
KATIKA KUELEKEA SIKUKUU YA PASAKA, INAYOTARAJIWA KUWAADHIMISHWA
KUANZIA TAREHE 29 MACHI HADI TAREHE 1 APRILI, 2013. JESHI LA POLISI
LINAPENDA KUWAONDOA HOFU WANANCHI WOTE KUWA LIMEJIPANGA KIKAMILIFU
KATIKA KUIMARISHA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO KWA KIPINDI CHOTE CHA
SIKUKUU NA BAADA YA SIKUKUU, HIVYO WANANCHI WASHEREKEA SIKUKUU KWA
AMANI NA UTULIVU, PASIPO VITENDO AMA VIASHIRIA VYOVYOTE VYA UVUNJIFU WA
AMANI.
2.
IKUMBUKWE KUWA, WANANCHI WENYE IMANI YA KIKRISTO NA HATA MADHEHEBU
MENGINE HUTUMIA MUDA HUO KWENDA KUABUDU PAMOJA NA MUENDELEZO WA SHEREHE
HIZO KWENYE MAENEO MBALIMBALI YA STAREHE. UZOEFU UNAONYESHA KUWA BAADHI
YA WATU HUTUMIA KIPINDI HICHO CHA SIKUKUU KUFANYA MATUKIO YA UHALIFU
KUTOKANA NA MIKUSANYIKO HIYO YA WATU KATIKA MAENEO MBALIMBALI.
3.JESHI
LA POLISI LINAPENDA KUWAONDOA HOFU WANANCHI NA WAUMINI WOTE KUWA,
ULINZI UMEIMARISHWA KWENYE MAENEO YOTE YA KUABUDIA, FUKWE ZA BAHARI,
SEHEMU ZA STAREHE NA MAENEO MENGINE YOTE AMBAYO YATAKUWA NA MIKUSANYIKO
MIKUBWA YA WATU.AIDHA, TUNAPENDA KUWATAHADHARISHA WALE WOTE AMBAO
WATAKUWA WAKITUMIA BARABARA, KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI NA HASA KWA MADEREVA KUEPUKA KWENDA MWENDO KASI NA
KUTUMIA VILEVI WAWAPO KAZINI.
4
VILEVILE, JESHI LA POLISI LINAWATAKA WANANCHI KUONDOA HOFU NA KUWAPUUZA
WATU WACHACHE AMA KIKUNDI CHA WATU WANAOTUMIA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU
KUWATIA HOFU KWA KUSAMBAZA MESEJI ZA VITISHO KWA WATU MBALIMBALI KWA
LENGO LA KUVURUGA AMANI NA UTULIVU KATIKA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU.
KITENDO HICHO CHA KUSAMBAZA MESEJI ZA VITISHO KWA WANANCHI NI UHALIFU
KAMA UHALIFU MWINGINE NA WAKIBAINIKA HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA
DHIDI YAO.
5.
KATIKA KUHAKIKISHA USALAMA KWENYE KUMBI ZA STAREHE, WAMILIKI WA KUMBI
HIZO WAZINGATIE UHALALI NA MATUMIZI YA KUMBI ZAO KATIKA UINGIZAJI WA
WATU KULINGANA NA UWEZO WA KUMBI HIZO, BADALA YA KUENDEKEZA TAMAA YA
FEDHA KWA KUJAZA WATU KUPITA KIASI. VILEVILE, WAZAZI WAWE MAKINI NA
WATOTO WAO NA HASA DISKO TOTO, ILI KUEPUKA AJALI NA MATUKIO MENGINE
YANAYOWEZA KUSABABISHA MADHARA JUU YAO.
6.
JESHI LA POLISI LINATOA TAHADHARI KWA WANANCHI WOTE KWAMBA, WATOKAPO
KWENYE MAKAZI YAO WASIACHE NYUMBA WAZI AMA BILA MTU NA WATOE TAARIFA KWA
MAJIRANI ZAO, NA PALE WANAPOWATILIA MASHAKA WATU WASIOWAFAHAMU WASIKAE
KIMYA BALI WATOE TAARIFA KWA JESHI LA POLISI AU VIONGOZI WAO WA SERIKALI
YA MTAA, SHEHIA, KIJIJI AU KITONGOJI ILI HATUA ZA HARAKA ZIWEZE
KUCHUKULIWA.
7.
MWISHO, NAPENDA KUWAHAKIKISHIA WANANCHI KWAMBA, JESHI LA POLISI
LINATEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA KUZINGATIA SHERIA ZA NCHI NA HIVYO
HALITAWAJIBIKA KUMWONEA HURUMA AMA UPENDELEO MTU YEYOTE ATAKAYEENDA
KINYUME NA SHERIA ZA NCHI.
NAWATAKIENI WATANZANIA WOTE PASAKA NJEMA.
IMETOLEWA NA:
ADVERA SENSO
MSEMAJI WA JESHI LA POLISI (T)
No comments:
Post a Comment