Wednesday, February 20, 2013

PICHA ZA KWENYE IBADA YA MWISHO YA PADRI MUSHI

Kanisa la St. Joseph Minara miwili.
.
.
.
Ibada maalum ya kumuombea Padre Evarist Mushi imefanyika leo Zanzibar kwenye kanisa katoliki la St. Joseph la Minara miwili na kuongozwa na Askofu mkuu Muadhama Polycarp Cardinal Pengo na kuhudhuriwa na mamia ya waumini wa kanisa hilo.
Wengine waliohudhuria ni viongozi mbalimbali wa kiserikali wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein ambapo baada ya ibada safari ya kuelekea Kitope kwenye maziko ilianza kwa msafara wa magari mengi kupita mitaani huku ukiongozwa na gari la Polisi.
Padri Evarist Mushi wa Kanisa katoliki la St Joseph la Minara Miwili aliuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akielekea kwenye ibada ya jumapili ya Kanisa la St. Theresia lililoko Mtoni.

by millard ayo.com

No comments:

Post a Comment