Thursday, July 4, 2013

Obama day.......

Ndege ya Rais wa Marekani, Barrack Obama, 'Airforce One' ikiwa imetua tayari, uwajani hapo.Maofisa Usalama wa Marekani, wakiingia Uwanja wa Ndgege wa Zamani, jijini Dar es Salaam, ilikotua ndege ya Rais Barrack Obama wa Marekani  kwa ajili ya kuimarisha ulinzi uwanjani hapo jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)



Maofisa Usalama wa Marekani, wakiwa juu ya paa la Uwanja wa Ndgege wa Zamani, jijini Dar es Salaam, ilikotua ndege ya Rais Barrack Obama wa Marekani kwa ajili ya kuimarisha ulinzi uwanjani hapojana.


Rais Jakaya Kikwete, akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (wa tatu kushoto), alipowasili Uwanjani hapo kwa ajili ya kumpokea mgeni wake, Rais wa Marekani, Barrack Obama.


 
Rais Barraka Obama akishuka na mtoto wake mkubwa Mallya, uwanjani hapo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku mbili nchini.


Mke wa Rais wa Marekani, Barrack Obama, Michelle Obama, akishuka kwenye ndege hiyo na mtoto wake, Sasha.


Mke wa Rais wa Marekani, Barrack Obama 'First lady' akikumbatiana na Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya kuwasili uwanjani hapo na mumewe (kulia), leo mchana.


 Rais Obama akipokea maua kutoka kwa mtoto Zakia Minja, uwanjani hapo.


Rais Barrack Obama akiongozana na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili uwanjani hapo jana mchana.


Rais Obama akikagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili na kupigiwa mizinga 21.


Rais Obama akitoka kukagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili na kupigiwa mizinga 21, uwanjani hapo jana.


Rais Barrack Obama akiwa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete akipokea gwaride la heshima uwanjani hapo, mara baada ya kuwasili jana mchana.


Rais Barrack Obama akisalimiana na mke wa Rais Kikwete, Mama Salama mara baada ya kupokea gwaride la heshima uwanjani hapo.


 Rais Barrack Obama, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.


 Akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.


 Hapa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.


 Akisalimiana na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi.


Hapa Rais Obama na mwenyeji wake, Rais Kikwete, wakifurahia ngoma ya Mganda ya asili ya Wangoni, mkoani Songea.


Hapa Rais Barrack Obama akiongozana na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuondoka Uwanja wa ndege.


Wananchi wakiwa wamekusanyika nje ya jengo la Ikulu kwa ajili ya kumkaribisha Rais Barrack Obama.


Wananchi waliokusanyika nje ya jengo la Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumkaribisha Rais Barrack Obama,wakipunga bendera za Tanzania na Marekani. 





Maofisa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakiwa nje ya Ikulu, kumkaribisha Rais, Barrack Obama.


Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma (kulia), akiwa na mgeni wake, First lady, Michelle Obama, kwenye Ofisi za Wama.


Hapa wakiwa Makumbusho ya Taifa, wakipokea mau kwa ajili ya kuweka kwenye mabaki ya vifaa vilivyolipuliwa na bomu kwenye Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam.


Wake hao wa Marais wa Marekani na Tanzania, wakiweka mashada hayo kwenye mabaki hayo kwa ajili ya kuwakumbuka waliopoteza maisha yao kwenye tukio hilo.


Wakiwaombea wahanga hao, mara baada ya kuweka mashada hayo ya maua.

Mapokezi ya Rais Barack Obama wa Marekani na Mkewe yalivyokuwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Barack Obama wa Marekani (kushoto) akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari wa Tanzania na Kimataifa Ikulu Jijini Dar es Salaam jioni hii ambapo mbali na kuzungumzia mstakabali wa ziara yake nchini Tanzania na Afrika pia amezungumzia masulala mbalimbali ya Kimataifa ukiwepo mgogoro na Vurugu zinazoendelea nchini Misri na Congo DRC.

  Rais Obama akipanda mti aina ya mpingo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa maelezo ya mti wa mpingo anaotaka kuupanda katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho kikwete akimsindikiza mgeni wake baada ya kumpatia mapokezi ya kihistoria leo Ikulu,

Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle watumbuizwa na ngoma za asili baada ya dhifa ya kitaifa Ikulu Dar es salaam July 1, 2013










No comments:

Post a Comment