Sunday, April 19, 2015


WAHARIRIR WAIGOMEA SHERIA YA MTANDAONI





Ni kama wamegoma, Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini wameitaka serikali kuacha kuharakisha zoezi la kutia saini sheria ya mtandaoni badala yake wajikite kutoa Elimu kwa watanzania ili sheria hiyo ifahamike,
Wakizungumza katika Mkutano maalum ulioitishwa na wizara ukilenga kuwapa elimu juu ya sheria hiyo inayosubiri kuwekwa saini na Mh. Rais Jakaya Kiwete, wamesema sheria hiyo inamatatizo na inahitaji muda wadau waipitie na kuielewa,

Wamesema makosa yaliyoainishwa katika sheria hiyo ambao kama ikitiwa saini na kuanza kutumika, inaweza kuwabana watu ambao hawahusiki.
Baadhi ya makosa yaliyoanishwa katika sheria hiyo ni pamoja na kutuma taarifa bila ridhaa ya mtu, kusambaza picha za ngono na za utupu, udanganyifu unaohusiana na kompyuta, makosa yanayohusiana na utambuzi, kughushi kunakohusiana na masuala ya kompyuta na kusambaza picha za utupu za watoto.
Mengine ni unyanyasaji kwa kutumia mtandao, kuchapisha taarifa yoyote ambayo itasababisha mauaji ya kimbari, uongo na matusi ya kibaguzi, huku adhabu kali ikiwa ni faini ya Sh50 milioni au kifungo kisichopungua  miaka saba, kwa mtu atakayebainika kusambaza picha za ngono mtandaoni.
Sheria hiyo pia iliwahi pia kulalamikiwa na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika aliyeitaka Serikali ikusanye maoni ya wadau kabla ya kuwasilisha muswada huo kwa hati ya dharua kutokana na umuhimu wake kwa jamii.
Wamedai kuwa sheria hiyo inaweza kuifanya Tanzania ikawa ni kati ya nchi adui wa matumizi ya mtandao wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).
“Sheria hii itamuathiri mtu yeyote anayeweza kutumia mtandao wa intaneti kwa kutumia kifaa chochote iwe kompyuta kubwa au vifaa vyenye uwezo wa kufanya kazi kama kompyuta kama simu za kiganjani, televisheni na vifaa vingine vinavyoendana na hivyo,”Amesema Peter Nyanje Mhariri wa the Citizen.

No comments:

Post a Comment