Friday, November 27, 2015

a ya kuagwa na maziko ya marehemu Alphonce Mawazo wa Chadema hii hapa, Lowassa, Sumaye na Mbowe kuongoza maombolezo Ratiba ya shughuli ya utoaji heshima za mwisho na mazishi ya Kamanda Mawazo Leo Siku ya Ijumaa, Novemba 27 saa 2 asubuhi, mwili wa Mpiganaji na Kiongozi wetu Alphonce Mawazo utachukuliwa Hospitali ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba yake mdogo, eneo la Nyegezi-Swea kwa ajili heshima za familia kabla ya kuelekea Viwanja vya Furahisha ambapo Viongozi waandamizi wa UKAWA, wakiongozwa wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, Mgombea Urais Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, wabunge wa UKAWA, wataongoza maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mawazo. Baada ya Viwanja vya Furahisha, mwili wa Mpiganaji Mawazo utasafirishwa kuelekea Geita kwa ajili ya kuwapatia nafasi wakazi wa Mkoa wa Geita kumuaga Kiongozi wao siku ya Jumamosi, Novemba 28 kuanzia asubuhi mapema ambapo baadae mchana mwili huo utapelekwa Mji Mdogo wa Katoro, mkoani Geita, ambapo pia wananchi watapata fursa ya kumpatia heshima za mwisho na kumuaga Mawazo ambaye alikuwa ni Mgombea wao wa Ubunge wa Jimbo la Busanda. Baada ya wakazi wa Katoro kushiriki tukio hilo, mwili wa Kamanda Mawazo utapelekwa nyumbani kwao kijijini Chikobe tayari kumhifadhi kwenye nyumba ya milele shambani kwake, siku a Jumapili, Novemba 29, baada ya familia, ndugu, jamaa na wakazi wa kijiji hicho kutoa heshima zao za mwisho. Tumaini Makene Msemaji Mkuu Chadema Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu

Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu

Sentensi 7 za Mbowe nje ya Mahakama baada ya kuruhusiwa kuaga mwili wa marehemu Mawazo Mwanza.

Ishu ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kuzuiwa kuaga mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Geita imekuwa ikiripotiwa na kuandikwa kwenye vyombo vya habari huku ikisubiriwa kutolewa majibu na Mahakama Kuu Mwanza kuhusu hatma ya zuio hilo.
Leo maamuzi ya Mahakama Kuu Mwanza yametoka na majibu kwamba wanaCHADEMA na viongozi wao wamepata kibali cha Mahakama hiyo kuendelea na shughuli za kuaga pamoja na mazishi ya kiongozi huyo.
Marehemu Alphoince Mawazo kwenye Jukwaa la Kampeni enzi za uhai wake.
Marehemu Alphonce Mawazo kwenye Jukwaa la Kampeni enzi za uhai wake.
Nje ya Mahakama Kuu Mwanza, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe alipata dakika chache kuongea na wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa wakisubiri kusikia maamuzi ya Mahakama >>>> “Ni lazima tukae vikao kupanga ratiba ya kumuaga Kamanda Mawazo, Jaji ametoa maelekezo kwamba viongozi wa CHADEMA, familia ya marehemu na Jeshi la Polisi wakae pamoja kupanga ratiba kamili.”
index-II3
Tutaheshimu maelekezo ya Jaji lakini hatutakubali kuonewa, muwe na imani kwamba haki itatendeka… tunakwenda kwenye vikao lakini tunahitaji kumaliza jambo hili kuanzia kesho, tutamuaga Mawazo kwa heshima anayostahili katika eneo ambalo tutawatangazia.” >>> Freeman Mbowe.
CDM
Ezekiel Wenje na Salum Mwalimu wakiwa ndani ya Mahakama Mwanza.
index VI
index III
Watu wa usalama nje ya Mahakama Kuu Mwanza.
index IV
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wanaCHADEMA
index V
index
Wakili wa CHADEMA, John Mallya.

Kwa hisani ya Millart Ayo.com
Ratiba ya kuagwa na maziko ya marehemu Alphonce Mawazo wa Chadema hii hapa, Lowassa, Sumaye na Mbowe kuongoza maombolezo Ratiba ya shughuli ya utoaji heshima za mwisho na mazishi ya Kamanda Mawazo Leo Siku ya Ijumaa, Novemba 27 saa 2 asubuhi, mwili wa Mpiganaji na Kiongozi wetu Alphonce Mawazo utachukuliwa Hospitali ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba yake mdogo, eneo la Nyegezi-Swea kwa ajili heshima za familia kabla ya kuelekea Viwanja vya Furahisha ambapo Viongozi waandamizi wa UKAWA, wakiongozwa wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, Mgombea Urais Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, wabunge wa UKAWA, wataongoza maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mawazo. Baada ya Viwanja vya Furahisha, mwili wa Mpiganaji Mawazo utasafirishwa kuelekea Geita kwa ajili ya kuwapatia nafasi wakazi wa Mkoa wa Geita kumuaga Kiongozi wao siku ya Jumamosi, Novemba 28 kuanzia asubuhi mapema ambapo baadae mchana mwili huo utapelekwa Mji Mdogo wa Katoro, mkoani Geita, ambapo pia wananchi watapata fursa ya kumpatia heshima za mwisho na kumuaga Mawazo ambaye alikuwa ni Mgombea wao wa Ubunge wa Jimbo la Busanda. Baada ya wakazi wa Katoro kushiriki tukio hilo, mwili wa Kamanda Mawazo utapelekwa nyumbani kwao kijijini Chikobe tayari kumhifadhi kwenye nyumba ya milele shambani kwake, siku a Jumapili, Novemba 29, baada ya familia, ndugu, jamaa na wakazi wa kijiji hicho kutoa heshima zao za mwisho. Tumaini Makene Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu

Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu

No comments:

Post a Comment