Saturday, September 29, 2012

Jumba la EBSS-2012 linatisha kwa uzuri


huu ndio mlango wa kuingia ndani ya mjengo wenyewe, Madam Ritta anaingia hapa....


 
SHINDANO la kusaka vipaji vya uimbaji la Bongo Star Search limeanza tena, ambapo mwaka huu itakuwa na washiriki 12 na mmoja wao atakayeshinda ataibuka na kitita cha Shilingi MIlioni 50.
Kila mwaka shindano hili ninazidi kuboreshwa na kuwa na muonekano bora, safari hii shindano hilo linafahamika kama Epiq Bongo Star Search (EBSS) kutokana na kampuni ya Simu ya Zantel kuamua kuunga mkono kwa kutoa ufadhili.
Kwenye maboresho ya EBSS washiriki wote 12 watakuwa wakiishi katika nyumba moja, wakiwa ndani watafanya kazi mbalimbali pamoja na kupata mafunzo ya muziki kutoka kwa wakufunzi wenye utaalamu wa masuala ya muziki.
Jaji Mkuu wa EBSS Ritta Paulsen maarufu kama `Madame Ritta'alisema jumba hilo lenye kila kitu ndani ni moja ya alama kuu ya maboresho ya shindano hilo na kuwa la Kimataifa zaidi.
"Jumba la EBSS ni moja ya nyumba yenye ubora nchini, washiriki wataishi humo kwa muda wa wiki nane wakati kusaka msindi wetu, wakiwa ndani watafurahi, watajifunza mambo mbalimbali pamoja na kuongeza uzoefu wa kuishi kwa kujituma," alisema Ritta.
Ufunguzi wa jumba hilo ulifanyika mapema wiki hii, ambapo watu mbalimbali wakio\wemo viongozi wa Zantel walishuhudia sherehe ya uzinduzi.

ENEO ILIPO EBSS HOUSE
Jumba hilo la kifahari  lipo katika eneo la Kawe Mzimuni, imezungukwa na majumba ya kifahari pamoja na kambi ya Jeshi ya Lugalo.
Sehemu hiyo ni tulivu, kitu ambacho kinasababisha washiriki kujifunza vizuri wakiwemo ndani ya nyumba pamoja na kufanya shughuli zao kwa utulivu mkubwa.

NDANI YA NYUMBA.
Ukumbi wa mazoezi: Mara unapoingia ndani kupitia lango kuu wenye kunakshiwa na marembo ya Kizanzibar, utakumbana na chumba kikubwa, ambapo hapo ndipo sehemu maalum ya kufanyia mazoezi ya uimbaji.
Kwenye chumba hicho kuna vyombo mbalimbali vya muziki vitakavyotumiwa na washiriki wakati mazoezi yao ya vitendo.

Dadasa: Kwa upande wa kushoto ndani ya jumba hilo kuna chumba kidogo chenye viti pamoja na ubao. Kwa mujibu wa Muandaaji wa Shindano hilo Ritta paulsen chumba hicho kitatumika kama darasa, washiriki watapewa mafunzo mbalimbali ya jinsi ya kutumia toni za muziki kwa nadharia.

Jiko: Upande wa mbele kabisa kuna chumba maalum kwa ajili ya kupikia, humo kuna vifaa vyote vya mazuala ya upishi, hivyo itakuwa rahisi kwa washiriki wenyewe kupika chakula wanachotaka endapo hawatapenda kula vile wanavyopikiwa na wapishi maalum waliokuwemo ndani ya nyumba.

Vyumba vya kulala washiriki: Katika shindano hilo kunakuwa na mtu ambaye anaitwa Mkuu wa nyumba, huyu ni mshiriki ambaye ameshinda kutokana na kufanya jitiahada kubwa katika kazi zake na hukabidhiwa kazi ya kuwaongoza wenzake. Safari hii Mkuu wa nyumba atakuwa na chumba chake cha kulala chenye kila kitu ndani yake, hivyo anaweza kujifanyia shughuli zake hata akiwa ndani ya chumba chake. Kwa upande wa washiriki kuna chumba kikubwa chenye vitanda vitakavyowatosheleza kulala washiriki wote.

Vitu Vingine: Baadhi ya vitu vingine vilivyokuwemo kwenye nyumba hiyo ni pamoja na bwawa la kuogelea, chumba cha kulia chakula, sehemu ya kupumzikia pamoja na bustani nzuri ya kufanyia mazongezi.

Washiriki waliofanikiwa kuingia ndani ya nyumba hiyo ni Godfrey Kato, Husna Nassoro, Linias Mhaya, Menynah Atiki, Norman Severina, Nsami Nkwabi, Nshoma Ng'hangasamala, Salma Mahin, Vicent Mushi, Wababa Mtuka na walter Chilambo.

Friday, September 28, 2012

Waziri wa Utalii Balozi Kagasheki, ndani ya Spain

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Taleb Rifai katika Makao Makuu ya Shirika hilo mjini Madrid, Hispania
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki (wanne kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Taleb Rifai (wa tano kushoto) katika Makao Makuu ya Shirika hilo mjini Madrid, Hispania. Wengine katika picha ni wajumbe wa sekretarieti ya shirika hilo pamoja na ujumbe uliofuatana na Waziri Kagasheki.

Na Carren Mgonja
Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) Bw. Taleb Rifai amewataka Watanzania kuutumia mkutano ujao wa masuala ya Uhifadhi na Utalii utakaofanyika nchini kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo kwa washiriki wa mkutano huo.

Rifai aliyasema hayo jana mjini Madrid alipokutana na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.


Rifai alisema kuwa Tanzania inavivutio vingi vya utalii lakini jitihada za makusudi zinahitajika kuvifanya vifahamike ulimwenguni  na hivyo kuongeza idadi ya watalii nchini ambayo hadi sasa haijafika milioni moja licha ya utajiri wa vivutio vilivyopo na kuongeza kuwa mkutano wa ujao wa masuala ya uhifadhi na utalii utakaofanyika mjini Arusha mwezi ujao ni fursa muhimu kwa nchi yetu kujitangaza ipasavyo

‘Sekta ya Utalii ndiyo yenye matumaini mazuri kwa uchumi wa Tanzania iwapo itatumika ipasavyo kwani itaweza kuongeza idadi ya wageni na hivyo kuongeza pato la taifa pamoja na kutoa ajira kwa wananchi wengi zaidi’ alisema Rifai.


Kwa upande wake Balozi Kagasheki alisema kuwa serikali imeamua kwa dhati kabisa kuifanya sekta ya utalii kuwa na tija kwa uchumi wa nchi kwa kuweka malengo ya kuwa na idadi ya watalii milioni moja katika muda mfupi ujao na kusema kuwa hilo litafanikiwa kutokana na mikakati mizuri iliyowekwa kuhakikisha lengo hilo linafikiwa.


Balozi Kagasheki alilitaka shirika la UNWTO kushirikiana vema na serikali ili kuhakikisha kuwa pande zote zinanufaika. Aidha, alipongeza uamuzi wa shirika hilo kuuleta mkutano huo nchini ambao unafanyika kwa mara ya kwanza nchini katika Bara la Afrika na kuahidi kuwa serikali itatoa kila aina ya ushirikiano ili kufanikisha  mkutano huo.


Waziri Kagasheki na ujumbe wake walitembelea Makao Makuu ya UNWTO kwa ajili kuzungumzia masuala mbalimbali ya uhifadhi na utalii nchini hususan mkutano ujao ambao utahusisha washiriki mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali duniani.


Mkutano wa First Pan African Conference utafanyika mjini Arusha kuanzia tarehe 15-18 mwezi ujao na utalenga katika masuala ya changamoto na fursa zilizopo katika eneo la utalii endelevu na uhifadhi kwa lengo la kuangalia namna uhifadhi na utalii unavyoweza kufanya kazi kwa pamoja bila kuathiri upande wowote.

Thursday, September 27, 2012

Sinta 'amvua nguo Okwi' hadharaniii....



Hivi karibuni kulikuwepo na uvumi juu ya mshambuliaji hatari wa timu ya Simba, Emmanuel Okwi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Sinta....jamaa Okwi sijui kitu gani kilimkurupua huko alipo aliibuka na status yake kwenye wall yake ya facebook ambayo bila kuongeza neno ilisema hivi....
"Hi ladies and gentlemen, I wanna take this opportunity tomake my self clear on an issue that has been going on about me and Christine Sinta.. A lot has been published in newspapers and on her blog that we are moving out togetherwhich is WRONG.. I just hope that u will all understand me.. It's been too much for me, i really tried to ignore all that was said about us but i believe it's high time u all know the truth.. Am not moving out with her as she claims.. No truth behind whatever she writes..Thanks to u all for your support..God bless u all..One love.."  

Alikuwa akimaanisha hivi katika lugha yetu ya madafu:
“Mabibi na mabwana, nachukua nafasi hii kuweka sawa uhusiano wangu na Christine Sinta, mengi yameandikwa kwenye vyombo vya habari na mitandano ya kijamii kama blog kuwa tupo pamoja, nasema siyo kweli.“Naamini mtanielewa, nimekwazika sana, nimejitaidi kupuuza yanayosemwa na sasa naamini ni wakati muafaka kujua ukweli,” alisema Okwi.
Ujumbe wake unaendelea: “Sina uhusiano wowote wa kimapenzi na yeye (Sintah) kama anavyodai, na hakuna ukweli wowote kwa anayoyaandika. Nawashukuru wote kwa sapoti yetu, Mungu awabariki.”
Ndugu yangu Sinta baada ya kusoma hayo cheki alivyojibu kwenye blog yake ya Sinta.com....mapenzi ya kibongo bwana...

Ohhhhh yeahhh we chop our money coz we don care
im having my own siesta with ma ladies thats y my baby boy loves me so much
lolest a certain villager wants to stop the unstoppable not knowing that the jiggas are still controlling his mind, when you asked for a war you should be ready because Im a lioness  even if it doesnt eat  for a week will not  become a thin as a goat that eats for everyday .
if you had a gun, i have a bullet proof body, look your self in the mirror and see weather u deserve me????
tell the same people u told that your dating me that you wanted a job to  polish my shoes and washing my  panties for 100usd per month,  and finally O you dont look good at all.
poachers are looking for u in Buwindi  game reserve because you escaped, Gorilla go back where u belong mxiuuuuu.
i get paid for everything i do but you first pay for everything you do.
if ure on heat fold  your p***s and f**k ya a*ss
life goes on under the S,,,,K,,,,,Y.

you look like a gateman you can never make a list of my  pet dogs.
and never  joke with the monk coz always be a  monk.
you should thank Mr Mulindwa  who made u see the black board .
the hunter becomes the hunted so dance  to the tune of my music, you have stepped in hell and now yo will get fire.
go back and take your ajono.
malooooh came from chaloo,eating kaloooooo driving gadigadii,,  okwiiiiii go and cut your filimbi (circumcised) .
im a sophisticated empowered woman and your sophisticated lost dog looking for bones, and at our home dogs eat bread.
 finish what you have started ,this is another side of sexy baby j wake lo
you have just tickled a private part of a tiger lolest.
 i go by the name sintah
j wake lo
the unstoppable
mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe
Nothing but confidence.
 katala-  mtu mjinga
tadoba-kibatari kwasababu ni mweusi kijijini alipooka anahitaji mwanga
halafu sihitaji ushauri nasaha, mkamshauri yeye alieandika fb akijua sitojibu fb ana watu 2000 my website inaangaliwa dunia nzima.
swali nani imekula kwake?? watu 2000 fb au watu zaidi ya million ktk hii no 1 website
muniwacheeee

hiyo ikapita, Sinta akaona haitoshi leo katoa kingine cha ukweli ambacho ametoa lake la rohoni...jamani mapenzi hayaaa.....soma hapa...ila Sinta hata mimi namkubali kama mwanamke anayejiamini safi mama...jiamini.

"Stopppppp kuniandikia pumba huku kuhusu mtu mwenye govinda kaandia fb  hayanihusu
i dont deal with people who have un-sustainable career uwiiii the whole of me the lope lope of all trades haaaaa,
 usisihindane na mimi maana i have got three career hata kama sifanyi moja ninakula je yeye mwenzangu mguu ukivunjika kuna kitu tena???
MA  International relations and Diplomacy as well as queen wa entertainment industry sasa kazi kwako wewe kinuka mkojo
usitukane mamba na bado unapiga simu post itolewe hapa hakitoki kitu ulianza  na mimi namaliza..."
  walitoklezeaga.....

RICK ROSS ndani ya FIESTA 2012........




 Hapa msanii huyu akifanyiwa interview na vyombo vya habari....cheki tumbo

Kwa wale wapenzi wa Fiesta mwaka huu na mpenzi wa msanii mkali duniani, kampuni inayoaanda tamasha kubwa kila mwaka nchini ya Prime Time imeamua kuwapa kile kitu ambacho roho yenu napenda.

Prime Time inawaletea msanii mkali dunia, RICK ROSS ambaye atatumbuiza katika tamasha hilo litakalofanyika October 6 kwenye viwanja vya Leaders Club.....

Endelea kufatilia hapa tukupe habari kamili juu ya ujio huu....

Miss Tanzania Nov 3

Mkurugenzi wa LINO AGENCY na mratibu wa shindano la kumsaka Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza na waandishi wa habari, kushoto ni meneja wa kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro na kulia ni Miss Tanzania 2012 Salha Israel pamoja na mshindi wa nne JenniferKakolaki.
Mashindano ya Redds Miss Tanzania kwa sasa yamekamilika katika hatua zote na hatua ya mwisho ilikuwa hatua ya kanda ambayo kwa sasa imekamilika na kufanikiwa kuwapa warembo jumla ya 30 .
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa LINO AGENCY Hashim Lundenga alisema mashindano kiujumla katika ngazi zote hadi kanda yamekuwa na mafanikio makubwa na kuonyesha kuwa fainali ya Taifa ya mwaka huu itakuwa na ushindani wa hali ya Juu.
 
Washiriki wengi wa mwaka huu kwa asilmia 90   ni wasomi  wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wengine wanatarajia kujiunga na Vyuo Vikuu, jambo ambalo litaleta hamasa kubwa katika shindano la mwaka huu.
 
Baada ya kukamilika kwa mashindano hayo ya Kanda kwa sasa tunatangaza rasmi kuwa warembo wote 30 walioshinda na kuingia katika kinyang,anyiro cha Redds Miss Tanzania 2012 wataingia kambini siku ya jumanne October 2,2012 katika Hotel yenye hadhi ya kitalii ya GIRAFFE HOTEL  Iliyopo hapa Jijini Dar Es salaam,Washiriki hao watakuwa kambini kwa muda wa mwezi mmoja. 
"Tunapenda kuwajulisha wadau wa tasnia ya urembo kwamba shindano la REDDS MISS TANZANIA 2012 litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 03 November 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Peal (Ubungo Plaza)".
 
Kwa Upande wake Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro alisema wao kama wadhamini wakuu wa Redds Miss Tanzania wamejipanga kwa nguvu kubwa kutoa burudani ya aina yake kwa wadau wote wa tasnia ya urembo hapa nchini sambamba na kuhakikisha warembo wote waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali.
 
Kwa kuzingatia mabadiliko ya Kalenda ya Mashindano ya urembo ya Dunia, Mrembo wa Tanzania atakuwa na muda  mrefu wa maandalizi kwani atatakiwa kuripoti katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia katikati ya mwaka ujao.

Wednesday, September 26, 2012

Mamia wamuaga Agnes Yamo


Marehemu Agnes Yamo-enzi za uhai wake....





Mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima, Agness Christopher Yamo umeagwa leo mchana Buguruni, Dar es Salaam, tayari kwa safari ya mazishi kesho mjini Morogoro. Yamo aliyewahi pia kufanya New Habari 2006 Limited, alifariki dunia jana katika hospitali ya Jeshi, Lugalo, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Katika kuaga mwili wa marehemu, aliyekuwa mcheshi na rafiki wa wengi, mamia walijitokeza na wengi walishindwa kujizuia kiasi cha kulia hadi kupoteza fahamu. Hakika ilikuwa huzuni, simanzi na majonzi eneo la tukio. Agness ameliza watu. Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu, Amin.

Saturday, September 22, 2012

Yanga yatimua kocha aliyepokewa kwa mbwembwe....


kocha wa Yanga akicheki vijana wake...hapa kabla hajafukuzwa... 

Fukuza fukuza ya klabu ya Yanga iliyoanza baada ya mkutano wa wajumbe wa kamati ya utendaji uliofanyika makao makuu ya klabu imeendelea na imemkumba kocha mkuu wa klabu hiyo Mbelgiji Tom Saintfiet.
Taarifa za uhakika kutoka kwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga ni kwamba  uongozi wa timu hiyo umefikia maamuzi ya kumtimua kazi kocha huyo aliyeajiriwa miezi mitatu iliyopita kutokana na kutofautiana sera za namna ya kuiendesha klabu na uongozi wa juu wa mabingwa hao wa Afrika mashariki na kati.
kamati ya utendaji ilisimamisha ajira za viongozi waajiriwa wote wa klabu hiyo akiwemo katibu mkuu Celestine Mwesigwa na msemaji Luis Sendeu huku ikitoa onyo kwa kocha Saintfiet kwa tabia yake ya kuongea na waandishi wa habari bila mpangilio wa klabu lakini baada ya taarifa hizo kutoka usiku wa kuamkia leo kocha huyo akaonekana akiongea kwenye television mojawapo nchini akizungumzia mambo mbalimbali kuihusu Yanga.
Kwa mujibu wa Sanga anasema kwamba sakata lote la jinsi kocha huyo alivyopoteza kazi yake litatolewa ufafanuzi.
Wakati huo huo aliyekuwa katibu mkuu wa Yanga kabla ya Mwesigwa, Lawrence Mwalusako amepewa jukumu la kukaimu nafasi hiyo ya ukatibu mkuu wa Yanga kwa muda wakati mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Seikolojo Chambua akikabidhiwa majukumu ya kuwa meneja wa timu hiyo akichukua nafasi ya Hafidh Salehe ambaye nae aliondolewa.
Nafasi ya usemaji wa Yanga mpaka sasa imekuwa kitendawili, tetesi zinasema kuwa mtangazaji wa Clouds FM NA Clouds TV Abdul Mohamed na Mwanahabari Mahmoud Zubeiry mmojawapo anaweza kula shavu la kumrithi Sendeu.
Stori imeandikwa na shaffihdauda.com

Friday, September 21, 2012

Yanga yatimua viongozi wake.....sababu...



msemaji wa zamani ya Yanga, Louis Sendeu....

Viongozi wa Yanga wakiongea na waandishi wa habari

 Na Mahmoud Zubeiry
UONGOZI wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, umeisimamisha kazi Sekretarieti nzima ya klabu, akiwemo Katibu Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis Sendeu, kutokana na kile ilichoeleza utendaji usioridhisha.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ‘mida  hii’ makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema kwamba maamuzi hayo yamefuatia kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika tangu saa 5:30 leo hadi saa 9:30.
Wengine wanaokumbwa na panga hilo ni Masoud Saad, aliyekuwa Ofisa Utawala, Philip Chifuka aliyekuwa Mhasibu na Hafidh Saleh aliyekuwa Meneja ambaye anahamishiwa kwenye majukumu mengine.
“Tumesitisha mikataba ya sekretarieti nzima, pia tumefanya marekebisho, tumemtoa Meneja wa timu na muda si mrefu tutamtangaza Meneja mwingie pamoja na sekretarieti mpya,”alisema Sanga. 
Aidha, Sanga alisema Kocha Mbelgiji, Tom Saintfieti anapewa onyo kali kwa kuzungumza ovyo na vyombo vya habari.
“Tumekwishakutana naye mara kadhaa kumpa utaratibu wa kuzungumza na vyombo vya habari, sasa tutamuandikia barua ya kumkumbusha wajibu wake na kuzingatia wajibu wake, kutozungumza na vyombo vya habari holela,”alisema.
Kwa ujumla maamuzi haya yanakuja baada ya Yanga kuanza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikiambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili za awali, kutokana na sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi na Jumatano ikachapwa mabao 3-0 Morogoro Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Thursday, September 20, 2012

Redd’s Miss Temeke, Kanda ya Ziwa kutoa 'macho' leo

 Walimu wakiwapa somo la fainali mamisi wetu wa Temeke.....

Kila mtu akiwa full kujiamini.......hao ni Temeke..

KUMEKUCHA! Kama ni mtoto hatumwi dukani, kutokana na mashindano mawili makubwa yanayohusisha Redd’s Miss Tanzania ambayo yanatarajiwa kufanyika leo na kesho.
Kinyang’nyiro cha kwanza kipo leo wakati warembo 12 watapopanda jukwaani katika Ukumbi wa PTA uliopo Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba), kuwania taji hilo.
 Wakati Temeke wakifanyiana kweli leo, kazi ipo kwa Redd’s Miss Kanda ya Ziwa, wakati warembo 20 watyakapochuana katika Uwanja wa Soka Kahama, Shinyanga kuwania taji la kanda hiyo.
Katika Redd’s Miss Temeke, juzi ilitembelewa na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga aliyefuatana na wasaidizi wake kadhaa ili kuwapa somo la mwisho.
Katika shindano la Redd’s Miss Temeke, kiingilio kwa viti maalumu itakuwa Sh 50,000 na viwango vingine, huku kukiwa na burudani kadhaa za aina yake.
Akizungumzia shindano la Redd’s Miss Kanda ya Ziwa, mratibu wa mpambano huo, Clara Mwasa, alisema warembo hao watawania taji linaloshikiliwa na Trecy Magulla ambaye pia ni Miss Tanzania namba pili.
Katika shindano hilo kiingilio kitakuwa ni Sh 30,000 kwa viti maalumu na Sh 20,000 na Sh 10,000 kwa vile vya kawaida.
“Kuna kitu cha ajabu kitatokea Kahama, wasanii kibao kutoka Uganda watakuwepo, litakuwa shindano la kufunga kazi,” alisema Clara.
Redd’s Original inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ndio ambao wamedhamini kinyang’anyiro cha Miss Tanzania kwa muda wa miaka mitatu.

Wednesday, September 19, 2012

Mwili wa Wema Sepetu balaa......


Maumbile ya nyuma ya Wema Sepetu hadharani...cheki michiriki.......

Kwani Siku hizi imekuwa fasheni kuonyesha mikalio yenu nyinyi wasanii? hamuona mnajidhalilisha? wapenzi wenu wamekuwa wakichekelea wakiona mambo haya kwa steji lakini kaeni mtambue kuwa nyuma ya picha wanawasema vibaya na itafika muda watawachoka, mkipita mnazomewa.

Wema Sepetu mwaka jana ukiwa kwenye fiesta mjini Morogoro na x-boy wako Diamond ulipanda jukwaani pasipokuangalia nguo yako uliyovaa na kumsaidia chorus x-boy wako ulionyesha maumbile yako yote ya nyuma, kwa kweli wapenzi wako wengi walisikitika, walidhani labda ulipitiwa, lakini mwaka huu tena ona tako linavyoonekana, unajisikiaje...fresh.....ama....nilidhani ungeacha, hii michirizi mekundu ni nini...? cna jibu.
Mdudu wa kukaa nusu uchi umemwambukiza na 'shosti wako Ant Ezekiel ona sasa....kajiachia na wengi wanajiuliza inakuwaje kule nyuma kumelowa.....kama ni pombe jamani ziacheni au ndio mnaogopa kuonekana washamba? bora muwe washamba ndugu zangu. Tutafika kweli...?

Tuesday, September 18, 2012

Kesi ya Lulu majaji wawabana mawakili

Lulu akiwa katika pozi mahakamani jana, pembeni yake ni ofisa magereza.

"Nipigeni picha, mkichoka mtaniambia" akiwapa uhuru wapiga picha kujiachia.... pamoja yupo mahakabu lakini bado anadai...

Mapitio ya maombi ya utata wa umri wa msanii Elizabeth Michael 'LULU' (18) anayekabiliwa na shtaka la mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba (28) jana yamechukua sura mpya baada ya jopo la majaji watatu wa mahakama ya Rufani Tanzania kuhoji mawakili wa pande zote kwanini wamelifikisha suala hilo mahakamani hapo badala ya kusubiri usikilizwaji wa awali.
Jopo la majaji watatu liliketi jana wakiongozwa na mwenyekiti  wake Jaji January Msoffe, Bernard Luanda pamoja na Edward Rutakangwa saa 3:00 asubuhi ambapo walianza kuuhoji upande wa Jamhuri kwa sababu gani ameomba mahakama hiyo ifanye mapitio.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na wakili mwandamizi wa serikali Faraja Nchimbi akisaidiana na wakili wa serikali Shadrack Kimaro ulidai kuwa umeomba mapitio kwa sababu uamuzi uliotolewa na Jaji Dr Fauz Twaib alikiri maombi ya utetezi hayakuwasilishwa mahakamani kihalali kwa mujibu wa sheria.
Alidai kuwa jaji Dr.Twaib alitakiwa kuyaondoa maombi hayo lakini badala yake alikubali kuyasikiliza ilihali alibaini kuwa hayako sahihi.
"Jaji Dr Twaib alikosea kutoa tafsiri ya kifungu 44 (1) cha sheria ya mahakimu alipaswa kutoa maelekezo kwa mahakama ya Kisutu kulingana na makosa aliyoyaona katika uamuzi wa hakimu mkazi Augustina Mmbando na siyo kuyasikiliza yeye mwenyewe...tumeamua kuomba mapitio ili yasikilizwe kwa haraka badala ya kukata rufaa," alidai Nchimbi.
Alifafanua kwamba msingi wa malalamiko yao mahakamani hapo ni kuhusu uamuzi uliotolewa na jaji Dr Twaib ulikuwa na dosari kwa kuzingatia bado hoja ya msingi ilikuwa pembeni.
 Jaji Msofe aliuhoji upande wa utetezi kwanini shauri hilo limefika Mahakama Kuu ya Tanzania, wakati Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji na kwa sababu gani wasingesubiri shauri hilo lianze kusikilizwa katika usikilizwaji wa awali mahakama kuu badala ya upelelezi kukamilika.
Akijibu hoja hizo, wakili wa utetezi Peter Kibatala alidai kuwa waliwasilisha maombi yao kwa sababu ya kulinda na maslahi ya mtoto (mshtakiwa).

haya ni mahojiano yalivyokuwa:
Jaji Msofe: kwanini mmelizungusha kote huku suala la umri wakati lingeweza kutazamwa katika usikilizwaji wa awali utakapoanza mahakama kuu au mngeweza kuipa nafasi kesi ikaendelea kule mahakama ya Kisutu ambako ingekuwa imeshapiga hatua mbele sasa lakini kama mnapoteza muda kutaka utata wa umri usikilizwe ili iweje|?
Kibatala:Watukufu majaji lengo letu ni kulinda maslahi ya mtoto (mshtakiwa) hii ni kesi ya mauaji ni lazima kuwe na namna ya kuweka kumbukumbu wakati wa ushahidi wake.
Jaji Msofe: Najisikia vibaya leo hii kukaona katoto kamekaa pale kizimbani, huu ubishi wa kesi hii ya mauaji inayomkabili mshtakiwa kuhusu umri ili iweje?
Kibatala:Hatukuwa na namna ya kuingiza ushahidi wa umri isipokuwa kwa kuomba mahakama ichunguze umri ili itakapofikia usikilizwaji wa kesi ya msingi iweze kuwa na kumbukumbu sahihi.
Jaji Luanda: huyu sio mtoto wa kwanza kushtakiwa kwa kesi ya mauaji, kifungu cha 26 cha kanuni ya ashabu lazima kiangalie adhabu ya mtoto anayekabiliwa na kesi kama hii labda mngeweza kutuambia kwamba Lulu hawezi kushtakiwa, mnatuambia umri wake ili iweje?
Kibatala: Tutaondoa shauri kwa ajili ya kurejesha mahakama ya kisutu ili kuendelea na usikilizwaji wa awali kabla ya upelelezi haujakamilika na kuhamishiwa mahakama kuu kwa ajili  ya usikilizwaji wa kesi ya msingi.
 Mwenyekiti wa jopo hilo, Jaji Msofe alisema watakwenda kutafakari hoja zilizotolewa na pande zote mbili ambapo atazijulisha pande hizo tarehe ya hukumu kama kesi hiyo iendelee kusikilizwa utata wa umri mahakama kuu au jalada lirejeshwe mahakama ya kisutu kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.
Katika kesi hiyo Lulu anadaiwa kuwa April 7 mwaka huu huko Sinza Vatcan jijini Dar es Salaam mshtakiwa alimuua Steven Kanumba.
Aidha kwa mujibu wa mwenendo wa sheria ya makosa ya jinai (CPA) Lulu hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji lakini mara upelelezi utakapokamilika itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

Friday, September 14, 2012

Hii imetulia jamani.....

Karuka,  karuka tena karuka...kakutana na kijana black tayari kasha mpa vitu, hii imetulia ile mbaya.

Na hawa je....? jamaaa naye huyu katembea weeee...hapa toooop

kwa wale wanaopenda nguo za mitoko, kitu hicho, mmekiona? kimetoklezea...

Mkubwa Fella aibua vichwa kibaooo.....


Baadhi ya wasanii wanaounda kituo hicho chenye wasanii 37.

BAADA ya kuliongoza kwa mafanikio makubwa kundi nzima la TMK Wanaume family, meneja wa kundi hilo 'Mkubwa' Fella ameamua kuibuka tena safari hii akisaka vipaji ambayo havifahamiki kabisaaaa.

"Huku uswahili kuna vipaji si-vya kitoto, lakini wanapata tabu kwenda na kurudi studio matokeo yake wanaamua kukaa nyumbani na hatimaye vipaji hivyo vinakufa, lakini nimesikia kilio chao hapa Temeke mikoroshini nimefungua studio, nimefungua studio pamoja na kituo hiki kwa nia ya kuwaokoa wasanii wote wa huku chipukizi na hata wale maarufu ambao wengine walidondoka kimaisha na mimi nitawarekodia kwa mkataba na kuwa-manage," alisema Fella.

Alisema tangu kuanzishwa kituo hicho miaka kadhaa iliyopita tayari wasani kadhaa wameishaibuliwa akiwa Bibi Cheka pamoja na Dogo Aslay huku wasanii kibao dhaidi ya 37 wakiwa njiani kuibuliwa na kituo hicho wakiimba mchiriku, zouk pamoja na taarabu.


baadhi ya wasanii wa kike waliokuwemo kwenye kituo hicho.

Wednesday, September 12, 2012

Masiga wa BloveM aja kivingine.....



Masiga akiwa katika pozi na mke wake.......hongera kaka....imetulia hiyo.

Baada ya kukaa kimya katika game bila kufahamika wapi alipo nini anafanya, msanii wa muziki wa kizazi kipya katika miondoko ya R&B Alex Masiga ameibuka upya lakini kwa sasa ameibuka akiwa kama producer wa muziki pamoja na video.

Akizungumza na Rahateletz leo msanii huyo ambaye ni kwa sasa ni baba wa watoto wawili huku mwingine akiwa anatarajiwa mwishoni mwa mwaka huu alisema ameamua kufungua studio hiyo ambayo ameipa jina la 'Kazi Kwanza Record' ili kusaidia wasanii chipukizi.

"Nimeanzisha studio hizi kwa nia mbalimbali, nataka wasanii wenzangu wasinyanyasike kama sehemu zingine zilivyo, bei yangu itakuwa powa kuliko mfano, nataka iwe mfano kwa wasanii wenzangu wote....," alisema Masiga ambaye kwa sasa ni meneja mauzo wa Tigo katika mikoa ya Dar es Salaam na Zanzibar.

Masiga akiwa na Banana Zorro waliunda kundi la B Love M ambalo walitamba na wimbo wao Anakudanganya pamoja na nyingine nyingi alipoulizwa kuwa kwa sasa ameamua kuacha muziki na kujikita na kazi hizo alisema,

"Sijaacha muziki kabisaa mimi bado ni msanii, muziki naupenda kutoka moyoni, ila niliamua kusimama kwa muda ili niweze kumaliza elimu yangu ya chuo kikuu ambayo leo hii ndio imenisaidia kufika hapa, na kwa sasa naanza kutoa vitu,"alisisitiza.

Alisema tayari amesharekodi wimbo wake mpya alioupa jina la Mshakji wangu ambapo ndani yake mshkaji wake wa siku nyingi Darasa ameweka misitari miwili mitatu kwa ajili ya kuipa heshima zaidi songi hilo.

Masiga amesema kuwa songi hilo amerekodi katika studio za Maneke ambapo video anatarajia kuanza kurekodi wiki ijayo katika studio zake yeye mwenyewe zilizopo jijini Dar es Salaam maeneo ya Temeke Sabasaba......

Tuesday, September 11, 2012

Waandishi waandamana, Nchimbi atimuliwa







                        Dk Nchimbi akitolewa 'mkuku' katika maandamano hayo.





       Mhariri mtendaji wa C10 Dinna Chahali akitoa dukuduku lake leo.
                               Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania,Nevil Meena akitoa Tamko.

"Kunawatu wanahoji tunaandamana alafu iweje wakati siye ndio wenye vyombo vya habari si  tuandike tu? Hapana kuandamana kwetu kunamaana sana tumeandamana sikama hatuna uwezo wakufanya kitu zaidi ya kuandamana, tunazo silaha kubwa zaidi ya maandamano lakini hii ni hatua ya pili baada ya matamko mbalimbali kutolewa.

Aidha Meena akahoji hivyo inakuaje kama sikumoja watu wakaamka wakakuta hakuna chombo chochote cha habari kilicho hewani hakuna tv, hakuna radio na wala hakuna magazeti nchi hii itakuwaje?

Wanahabari waendelee kuwa na utulivu hatua mbalimbali zitakazoendelea kuchukuliwa watafahamishwa kuhusiana na tukio hilo."

Viongozi wengi wa vyama vya waandishi wa habari waliotoa maoni yao kwenye mkusanyiko huo waliitaka serikali wachukue hatua na damu ya Mwangosi iwe shule kwao.

Katika tukio lingine, Waziri wa mambo ya ndani, Dk Emannuel Nchimbi alitimuliwa katika tukio hilo kwa kuwa hakutakiwa kuwa eneo hilo.

Dk Nchimbi alifika hapo kwa nia ya kutaka kuzungumza na waandishi hao kutoka vyombo mbalimbali vya habari, lakini hali ilikuwa tofauti baada ya kundi la waandishi hao kukataa kuhutubiwa na waziri Nchimbi.

Kukataa kuhutubiwa na Nchimbi kuliendelea na kuzomewa na kisha kusindikizwa na wapambe wake hadi katika eneo alilokuwa amepaki gari lake ambalo halikuwa na namba za waziri.

Maandamano hayo yaliyokuwa ya amani yalilindwa vyema na jeshi la polisi, pia yalikuwa ya nchi nzima yalihudhuriwa na idadi kubwa ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

Naye mhariri wa gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu,"Sisi tunawalipa kodi polisi wapate sehemu za kuishi, bunduki, magwanda pamoja na buti na lengo ni kulinda raia na na mali zake na sio kuua watu, vitendo hivyi havivumiliki,".