Wednesday, September 12, 2012
Masiga wa BloveM aja kivingine.....
Masiga akiwa katika pozi na mke wake.......hongera kaka....imetulia hiyo.
Baada ya kukaa kimya katika game bila kufahamika wapi alipo nini anafanya, msanii wa muziki wa kizazi kipya katika miondoko ya R&B Alex Masiga ameibuka upya lakini kwa sasa ameibuka akiwa kama producer wa muziki pamoja na video.
Akizungumza na Rahateletz leo msanii huyo ambaye ni kwa sasa ni baba wa watoto wawili huku mwingine akiwa anatarajiwa mwishoni mwa mwaka huu alisema ameamua kufungua studio hiyo ambayo ameipa jina la 'Kazi Kwanza Record' ili kusaidia wasanii chipukizi.
"Nimeanzisha studio hizi kwa nia mbalimbali, nataka wasanii wenzangu wasinyanyasike kama sehemu zingine zilivyo, bei yangu itakuwa powa kuliko mfano, nataka iwe mfano kwa wasanii wenzangu wote....," alisema Masiga ambaye kwa sasa ni meneja mauzo wa Tigo katika mikoa ya Dar es Salaam na Zanzibar.
Masiga akiwa na Banana Zorro waliunda kundi la B Love M ambalo walitamba na wimbo wao Anakudanganya pamoja na nyingine nyingi alipoulizwa kuwa kwa sasa ameamua kuacha muziki na kujikita na kazi hizo alisema,
"Sijaacha muziki kabisaa mimi bado ni msanii, muziki naupenda kutoka moyoni, ila niliamua kusimama kwa muda ili niweze kumaliza elimu yangu ya chuo kikuu ambayo leo hii ndio imenisaidia kufika hapa, na kwa sasa naanza kutoa vitu,"alisisitiza.
Alisema tayari amesharekodi wimbo wake mpya alioupa jina la Mshakji wangu ambapo ndani yake mshkaji wake wa siku nyingi Darasa ameweka misitari miwili mitatu kwa ajili ya kuipa heshima zaidi songi hilo.
Masiga amesema kuwa songi hilo amerekodi katika studio za Maneke ambapo video anatarajia kuanza kurekodi wiki ijayo katika studio zake yeye mwenyewe zilizopo jijini Dar es Salaam maeneo ya Temeke Sabasaba......
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment