MWANAMUZIKI wa kizazi
kipya, kutoka uzazi wa kwanza wa BSS, Jumanne Idd ametangaza kurudi upya katika
game baada ya kukaa kimya akipiga kitabu.
Akizungumza na
mtandao huu jana, Idd alisema kuwa kukaa kwake kimya kulitokana na yeye
kujikita shuleni zaidi na pia kuwa mikoani kwa muda mrefu akisaidiana na
taasisi ya kupambana na maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi pamoja na jinsi
ya kuishi na virusi vya Ukimwi, mradi huo ambao umepewa jina la Mradi wa Ujana.
Alisema kwa sasa
ameachia song lake alilolipa jina la WAUE, ambao umezungumzia maisha
yake kutoka alipokuwa mwanzo kabla ya BSS na baada ya kuibuka mshindi wa BSS.
"Kwa sasa song
hilo lipo hewani linapigwa sana katika redio mbalimbali ambazo tayari
nimeshazisambaza katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini, na baadaye
Mungu akipenda ndani ya mwaka huu au mwaka ujao nitaachia albamu yangu ambayo
mpaka sasa bado sijaipa jina japokuwa baadhi ya nyimbo tayari
nimeshamaliza" alisema Jumanne Idd.
Wakati huohuo, Jumanne amesema kuwa wiki hii anatarajia kuzindua bendi yake aliyoipa jina la Tatoo, (Tatoo Band) itakayokuwa na maskani yake Ilala jijini Dar es Salaam, akizungumza na mtandao huu, Idd alisema bendi yake ambayo ina vifaa vyote vinavyohitajika itazinduliwa jumamosi hii (15.9.2012)katika ukumbi wa Masai Club iliyopo Ilala.
"Kila kitu kimekaa sawa, hakuna tatizo, bendi yangu ina wasanii 12, na wasanii wangu kwa sasa wapo kambini wakijifua kwa ajili ya uzinduzi huo, yaani itakuwa ni moto ile mbayaaa......tunataka kuwapa ladha safi wabongo yaani watapata kitu ambacho walikikosa long time.."alisema Idd.
Baadhi ya wasanii wanaonda kundi la Tatoo.......jamaa wana tatoo mwili mzima...haaaaa
Idd alitaja wasanii wanaounda kundi hilo kuwa ni, Salum Hamisi, Mamboleo Nassoro, Nuru Dismas, Salehe Dafar, Furaha Salum, Vumbi, Azizi Mohammed, Juma Shabani, Amir, Eloi pamoja na Said Mohammed.
vimwana wanaonda kundi la Tatoo wakiwa katika pozi nene......
No comments:
Post a Comment