Mkurugenzi wa LINO AGENCY na mratibu wa shindano la kumsaka Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza na waandishi wa habari, kushoto ni meneja wa kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro na kulia ni Miss Tanzania 2012 Salha Israel pamoja na mshindi wa nne JenniferKakolaki.
Mashindano ya
Redds Miss Tanzania kwa sasa yamekamilika katika hatua zote na hatua ya mwisho
ilikuwa hatua ya kanda ambayo kwa sasa imekamilika na kufanikiwa kuwapa warembo
jumla ya 30 .
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa LINO AGENCY Hashim
Lundenga alisema mashindano kiujumla katika ngazi zote hadi kanda yamekuwa na
mafanikio makubwa na kuonyesha kuwa fainali ya Taifa ya mwaka huu itakuwa na
ushindani wa hali ya Juu.
Washiriki wengi wa
mwaka huu kwa asilmia 90 ni wasomi wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wengine
wanatarajia kujiunga na Vyuo Vikuu, jambo ambalo litaleta hamasa kubwa katika
shindano la mwaka huu.
Baada ya
kukamilika kwa mashindano hayo ya Kanda kwa sasa tunatangaza rasmi kuwa warembo
wote 30 walioshinda na kuingia katika kinyang,anyiro cha Redds Miss Tanzania
2012 wataingia kambini siku ya jumanne October 2,2012 katika Hotel yenye hadhi
ya kitalii ya GIRAFFE HOTEL Iliyopo hapa
Jijini Dar Es salaam,Washiriki hao watakuwa kambini kwa muda wa mwezi mmoja.
"Tunapenda
kuwajulisha wadau wa tasnia ya urembo kwamba shindano la REDDS MISS TANZANIA
2012 litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 03 November 2012 katika Ukumbi wa
Hotel ya Blue Peal (Ubungo Plaza)".
Kwa Upande wake
Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro alisema wao kama
wadhamini wakuu wa Redds Miss Tanzania wamejipanga kwa nguvu kubwa kutoa
burudani ya aina yake kwa wadau wote wa tasnia ya urembo hapa nchini sambamba
na kuhakikisha warembo wote waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali watapata
fursa ya kujifunza mambo mbalimbali.
Kwa kuzingatia
mabadiliko ya Kalenda ya Mashindano ya urembo ya Dunia, Mrembo wa Tanzania
atakuwa na muda mrefu wa maandalizi
kwani atatakiwa kuripoti katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia
katikati ya mwaka ujao.
No comments:
Post a Comment