Walimu wakiwapa somo la fainali mamisi wetu wa Temeke.....
Kila mtu akiwa full kujiamini.......hao ni Temeke..
KUMEKUCHA! Kama ni mtoto hatumwi dukani, kutokana na mashindano mawili makubwa yanayohusisha Redd’s Miss Tanzania ambayo yanatarajiwa kufanyika leo na kesho.
Kinyang’nyiro cha kwanza kipo leo wakati warembo 12 watapopanda jukwaani katika Ukumbi wa PTA uliopo Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba), kuwania taji hilo.
Wakati Temeke wakifanyiana kweli leo, kazi ipo kwa Redd’s Miss Kanda ya Ziwa, wakati warembo 20 watyakapochuana katika Uwanja wa Soka Kahama, Shinyanga kuwania taji la kanda hiyo.
Katika Redd’s Miss Temeke, juzi ilitembelewa na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga aliyefuatana na wasaidizi wake kadhaa ili kuwapa somo la mwisho.
Katika shindano la Redd’s Miss Temeke, kiingilio kwa viti maalumu itakuwa Sh 50,000 na viwango vingine, huku kukiwa na burudani kadhaa za aina yake.
Akizungumzia shindano la Redd’s Miss Kanda ya Ziwa, mratibu wa mpambano huo, Clara Mwasa, alisema warembo hao watawania taji linaloshikiliwa na Trecy Magulla ambaye pia ni Miss Tanzania namba pili.
Katika shindano hilo kiingilio kitakuwa ni Sh 30,000 kwa viti maalumu na Sh 20,000 na Sh 10,000 kwa vile vya kawaida.
“Kuna kitu cha ajabu kitatokea Kahama, wasanii kibao kutoka Uganda watakuwepo, litakuwa shindano la kufunga kazi,” alisema Clara.
Redd’s Original inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ndio ambao wamedhamini kinyang’anyiro cha Miss Tanzania kwa muda wa miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment