|
Mwenyekiti akifungua kikaooooo |
|
mama akisisitiza jambo kwa mwanachama mpya wa Habari Group... |
|
mama, dada na mwalimu wakiwasikiliza ndugu zao... |
|
na mimi na pozi languuu |
|
mtu na dada yake jamani haoooo....mmmh |
|
haaaaaaa........ |
NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki amewataka wanachama wa kikundi cha waandishi wa habari cha kujikomboa kiuchumi (Habari Group) kupendana na kuaminiana ili kukifikisha
kikundi hicho mbali.
Kairuki ambaye pia ni mlezi wa Habari Group, alikitaka kikundi hicho kutokuwa wachoyo wa kusaidia waandishi wa habari wengine wenye nia ya kuungana na kufanikiwa kimaisha.
Akizungumza na kikundi hicho Dar es Salaam juzi, alisema ili mtu afanikiwe ni lazima awe mwenye upendo na kusaidia wengine pale penye mwanya wa kufanya hivyo na kuwataka wanachama wote kuwa na
moyo wa kujitolea kwa ajili ya kikundi.
"Sitopenda kusikia kikundi hiki kimekufa kwa sababu ya mifarakano na chuki miongoni mwenu kwani kwa kufanya hivyo hamtofikia malengo mliyokusudia," alisema Kairuki.
Aliongeza kuwa wakati anaingia madarakani aliweka vipaumbele kwa wafanyakazi wa majumbani, madereva wa aina zote, wafanyakazi wa mashambani, wahudumu wa baa na nyumba za wageni, walinzi na
waandishi wa habari.
Na kwamba ameanza kushughulikia haki mbalimbali za makundi hayo, ambapo kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuishinikiza serikali kusaini mkataba wa kuridhia haki za wasichana wa majumbani.
Aliwapongeza waandishi wa habari kwamba pamoja na changamoto nyingi wanazokutana nazo, lakini hawakati tamaa na wamekuwa wakifanya kazi yao kwa moyo mmoja na kwa bidii.
Kama mkakati wake wa kuwasaidia waandishi wa habari, alisema atasimamia Habari Group ili wawe mabalozi wazuri kwenye mambo mbalimbali kwa jamii, ikiwemo kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali, kuwapa elimu ya umuhimu wa cheti cha kuzaliwa, sambamba na kushirikiana nao bega kwa bega kwenye mambo muhimu ya kijamii.
"Kuwasidia kwenu ni miongoni mwa malengo yangu niliyojiwekea ya kupigania haki ya baadhi ya makundi ambyo nimeona haki zao kama wafanyakazi hazitekelezwi,"aliongeza.
Akizungumza katika hafla hiyo mwanamitindo maarufu nchini Jokate Mwegelo alisema kikundi hicho kitafika mbali endapo watajenga upendo baina yao.
“Haya maisha lazima mjikomboe, na kujikomboa ni kama hivi mnajiunga katika vikundi na mtasonga mbele kinachotakiwa ni kuwa na moyo na kile mnachokifanya…” alisisitiza Jokate.
Alisema kuwa hivi karibuni alianzisha kampuni yake ya kutengeneza nywele na muda si mrefu atasonga mbele kwa kufyatua bidhaa nyingine mpya.
“Tusitegemee wanaume tujenge uwezo wa kusimama sisi kama sisi na tuataendelea, leo hii Beyonce (Mwanamuziki wa Marekani) anaweza kusisimama hata kama akiwa ameachana na Jay Z na hilo ndilo lengo langu, lengo langu ni kukuwa kibiashara zaidi na zaidi nataka kuwa kama Bakhressa” alisisitiza Jokate.