- Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina
la Bi Kidude amefariki dunia leo mchana huko Bububu
Zanzibar, sehemu alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa.
- Mwili wake
utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho.
-
Bi Kidude
alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo..Alikuwa binti... wa mchuuzi wa
nazi naA hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata
mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102.
-
-
Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi
vya sanaa kule kwao...mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya
Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule .....
-
Mwaka
1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa
kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.
-
-
Bi Kidude pia liwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake,
na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba
katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni
|
No comments:
Post a Comment