Monday, April 15, 2013

NDEGE YAANGUKA JIJINI ARUSHA NA KUUA MTU MMOJA

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba ndege iliyokuwa inamilikiwa na Wakili maarufu Marehemu Nyaga Mawala aliyefariki wiki 3 zilizopita na kuzikwa huko Nairobi imeanguka ikiwa katika hatua za mwisho za kutua  katika kiwanja cha ndege cha arusha.

Taarifa zinasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na rubani pekee anayejulikana kwa jina la Jamal B S, au maarufu kama Bob Sambeke aliyekuwa anatokea West Kilimanjaro.


Taarifa zaidi zinasema kuwa  rubani huyo   amefariki  muda  mfupi  baada  ya  ajali  hiyo  kutokea  na   mwili  wake  umekimbizwa   hospitali ya Mount Meru
...

Maelezo zaidi kuhusu ajali hiyo ni kwamba ndege hiyo ilijaribu kutua baada ya masaa ya kawaida ya kufunga kiwanja(saa 12.30jioni) kupita.


Kiwanja cha ndege cha Arusha hakina taa za AGL, hivyo huwa kinamaliza au kufunga shughuli zake saa 12.30 za jioni, na hivyo kina'operate kwa masaa 12 tu.Na kawaida ma'controller huondoka baada ya closure ya kiwanja..

Mungu  ailaze  mahali  pema  roho  ya  marehemu
...
Picha ya ndege iliyoanguka
Name:  DSC03435.JPG
Views: 0
Size:  7.26 MB


Name:  DSC03444.JPG
Views: 0
Size:  6.98 MB
Eneo ambalo ndege iliyoanguka, kutoka eneo hilo mpaka landing truck ni kama 1km. Mbele ya mabaki hayo ya ndege kuna mti mmoja ambao unasadikiwa kuwa  ndege hiyo ilijigonga na kudondoka chini.

No comments:

Post a Comment