Monday, December 17, 2012

Dunia yalaani mauaji ya watoto 20 nchini Marekan

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amemtumia salamu za rambirambi gavana wa jimbo hilo akilaani tukio hilo na kusema kuwa kushambulia watoto ni kosa la uhaini.
Pamoja na Ban Ki Moon, Mkuu wa sera za umoja wa Ulaya Cathrine Ashton na mkuu wa tume ya umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso nao wameelezea kushtushwa na kushangazwa na tukio hilo huku Baroso akieleza kuwa maisha machanga ya vijana wenye matumaini yameharibiwa.
Mauaji hayo yametekelezwa na kijana mmoja aliyekuwa na silaha nzito mara baada ya kuingia katika shule ya awali ya Sandy Hook Elementary ambapo watoto 18 walifariki papo hapo wawili walifariki kutokana na majeraha wakiwa hospitalini.
Watu wazima waliopoteza maisha ni pamoja na mkuu wa shule hiyo huku taarifa zikieleza kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo kabla ya kuondoka katika eneo la tukio naye aliuwawa kwa risasi ingawa haijajfahamika kuwa aliuwawa na polisi ama alijiua mwenyewe.

No comments:

Post a Comment