Tuesday, December 15, 2015

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO AFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KATIKA KITUO FOREPLAN CLINIC KINACHOMILIKIWA NA DK. MWAKA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwasili katika kituo cha Foreplan Clinic kinachotoa tiba mbadala kilichopo Ilala Bungoni,  jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo jumatatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na tiba Mbadala Dk.Paul Mhame kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akipokelewa na mmoja wa wauguzi wa kituo hicho ambapo jina lake halikupatikana kwa haraka baada ya mkurugenzi wa kituo hicho Dk. Mwaka Juma Mwaka kutokuwepo kwenye kituo chake cha Foreplan Clinic kilichopo Ilala Bungoni,  jijini Dar es Salaam 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wananchi waliofika kupata matibabu katika kituo cha Foreplan Clinic kuhusu huduma zitolewazo katika kituo hicho kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka.
Masaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya akimtolea ufafanuzi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala kuhusu huduma zitolewazo katika kituo cha Foreplan Clinic mara baada ya kuanza kukagua kituo hicho kinachotoa Tiba 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akikikagua kifaa kinachotumika kufanyia vipimo kwenye kituo cha Foreplan Clinic wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo jioni siku ya jumatatu
Hiki ndicho kifaa kinachotumika kupimia wagonjwa kwenye maabara ya kituo hicho cha Tiba Mnadala
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwauliza maswali wasaizizi wa kituo hicho wakiongozwa na  Bi Teddy L. Mbuya mara baada ya kukuta hari ya sintofahamu katika kituo hicho
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akikagua moja ya dawa zinazotolewa kwa wangonjwa wanaokuja kutibiwa kwatika kituohicho cha tiba Mbadala
Bi. Rozaria Antoni ambaye ni muhudumu wa dawa akikaa kimya baada ya kuulizwa maswali na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala na kukosa la kujibu.
Hizi ni dawa za asili zinazouzwa katika kituo hicho cha afya
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akimpa maelekezo Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na mbadala Dk.Paul Mhame kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala leo majira ya jioni amefanyaziara ya kushtukiza  katika kituo kinachotoa tiba mbadala cha Foreplan Clinic kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka  kilichopo Ilala Bungoni na kujionea hali halisi ya kituo hicho. Mara baada ya kufika alianza kufanya ukaguzi kuanzia sehemu ya Mapokezi mpaka kwenye vyumba vya matabibu lakini katika vyumba vyote hakuna daktari aliyekuwa anatoa huduma.
Akizungumza na wagonjwa waliokuwa wakisubilia tiba alisema kuna waliofika katika kituo hicho ili kutibiwa lakini kituo hicho hakina uwezo wa kuwahudumia wagonjwa hao. Na kuwataka wagonjwa hao waende kwenye hospitali ili wapate matibabu yanayoendana na magonjwa wanayoumwa.
Akizungumza msaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya alisema yeye hawezi kusema kuhusu kituo hicho maana yeye sio msemaji mkuu bali alimwomba Naibu waziri kufanya ukaguzi katika kituo hicho pamoja na kuwaliza maswali wahusika mbalimbali wa vitengo vya ktuo hicho.
Baada ya ukaguzi wa kituo hicho Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amemwagiza Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na mbadala Dk.Paul Mhame ndani ya wiki moja kufanya ukaguzi kwa  kituo cha Dk. Mwaka na aletewe taarifa iliyokamilika kuhusu taaruma yeke pamoja na washirika wake na pia dawa anazozitumia kama ni rafiki kwa wananchi wanaotumia dwa hizo pamoja na kufanya ukaguzi wa vituo vyote vinavyotoa tiba mbadala na tiba asilia kama Dk. Ndodi, Dk. Rahabu nk. ili kuwabaini wanaowalaghai wananchi. 
Pia amesema Dk Mwaka Juma Mwaka amekuwa akijitangaza kupitia vyombo mbalimbali hapa nchini ambavyo ni kosa la kutangaza kama unafanya kazi za tiba tabibu. Alisema madaktari wana miiko na katika miiko hiyo ambayo inatumika na mojawapo ikiwa ni kutojitangaza. Naibu waziri aliendelea kusema kuwa Dk. Mwaka amekuwa akijiita Dokta na amekuwa akichambua mwili wa binadamu kama vile ameusomea udakitari wakati sheria ya tiba asilia na tiba mbadala hairuhusu watu wa tibaAsilia na Tiba Mbadala  kutumia maneno  ya tiba ya kisasa.
Pia Naibu Waziri amamtaka Dk. Mwaka Juma Mwaka kufika wizarani kesho saa mbili asubuhi akiwa na nyaraka zake zote zinazohusu utoaji wa huduma ya Tiba Mbadala kwani amekuwa akijiita majina ya tiba za kisasa na pia kutibu kwa njia ya kisasa badala ya kutibu kwa njia ya Asilia au Tabibu.

No comments:

Post a Comment