Tuesday, November 20, 2012

HUKUMU YA FUNDIKIRA WATU WALIA NA KUZIMIA MAHAKAMANI

 
Leo ilikuwa ndiyo siku ya hukumu dhidi ya watuhumiwa watatu wa mauaji ya marehemu Swetu Fundikira aliyeuawa kwa kupigwa miaka miwili iliyopita. Mara baada ya watuhumiwa hao kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa, ndugu na jamaa wa marehemu waliangua kilio na wengine hadi kuzimia kama walivyoshuhudiwa na paparazi wetu aliyeweka kambi mahakamani hapo. Kushoto ni dada wa marehemu Rehema Fundikira, Hadija Mdemu shemeji wa marehemu.
....mmoja wa ndugu wa Fundikira akibebwa mara baada ya kuzimia na kudondoka sakafuni
....akipepewa huduma ya kwanza kwa kupepewa
....akipata nafuu kiasi
.....ndugu wakilia
ndugu wakilia
...ilikuwa ni saa ya majonzi na huzuni
Watuhumiwa wakiwa mahakamani kabla ya hukumu kusomwa. kutoka kulia ni Rhoda Robert, Ally Gube na Mohamed Ally.
...safari ya huzuni ya Rhoda Robert kuanza maisha mapya gerezani mara baada ya hukumu,

ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Sajent Rhoda Robert, Koplo Ally Ngumbe na Mohamed Rashidi waliokuwa wakikabiliwa na Kesi ya mauaji ya Marehemu Swetu Fundikira imetolewa leo na Askari hao kuhukumiwa Kunyongwa hadi kufa.

Hukumu hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na ndugu jamaa na marafiki wa Swetu duniani kote ilitolewa leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hao watatu wametiwa hatiani baada ya kufanya kosa hilo siku ya Jumamosi tarehe 23 Januari, 2010 kwa kumpiga bila huruma Swetu Fundikira katika maeneo ya Kinondoni katika makutano ya barabara  za Mwinjuma na Kawawa jijini Dar es salaam mpaka kusababisha kifo chake.

Baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo vilio vimetawala kwa ndugu wa watuhumiwa hao huku baadhi ya watu wakidai sheria imechukua mkondo wake ipasavyo.
Marehemu Fundikira enzi za uhai wake.

picha kwa hisani ya globalpublishers.com

No comments:

Post a Comment