Thursday, November 15, 2012

KIPINDI CHA 'DIARY YA LADY JAYDEE' KURUSHWA EATV KILA JUMAPILI

 LADY JAYDEE
  Mkurugenzi wa Machozi Band,  Lady Jaydee akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salalaam leo wakati wa uzinduzi wa kipindi chake cha 'Diary Ya Lady Jaydee' kitakachoanza kurushwa hewani kila siku ya Jumapili kupitia televisheni ya EATV. Kushoto ni Mkuu wa Vipindi EATV, Lydia Igarabuza.

Mkuu wa vipindi wa Televisheni ya EATV, Lydia Karabuza akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kipindi cha televisheni cha 'Diary Ya Lady Jaydee kitakachoanza kurushwa hewani kuanzia Jumapili.
DAR ES SALAAM, Tanzania 
Msanii, Lady Jaydee amefanikiwa na kutambulika katika kiwanda cha muziki ndani na nje ya nchi, huku akitunukiwa tunzo nyingi zaidi akiwa albamu zake tano. Pamoja na kuwa anaendelea na fani yake ya muziki, Lady Jaydee ameamua kuwafikia na kuwaburudisha wapenzi wa kazi zake kwa njia nyingine.
Lady Jaydee sasa anaanza sura mpya ya burudani kwa kuleta kipindi cha TV kiitwacho DIARY YA LADY JAYDEE, ambacho kutaonekana katika kituo cha TV cha EATV
Diary Ya Lady Jaydee itaonesha maisha na hadithi za kweli za Lady Jaydee kwa lengo la
Kuburudisha kwa kuonesha mambo yate mazuri anayopitia au kuyaona Lady Jaydee
Kuelimisha kwa kushiriki mambo ya kijamii
Kutia moyo wengine wafuate ndoto zao kwa uadilifu
Kuongeza Kipato kama msanii kwa kutangaza biashara mbalimbali na hatimae kudumisha ajira binafsi kwa njia ya sanaa.
SHUKRANI
Lady Jaydee anatoa shukrani kwa mashabiki kwa kuendelea kumpokea, jambo ambalo linampa nguvu zaidi ya kufanya kaza.
pia anashukuru sana vyombo vya habari na zaidi anawashukuru EATV na washirika wake kwa kumpa nafasi ya kurusha kipndi chake kipya Diary Ya Lady Jaydee.
EATV imekuwa mchango wa aina yake katika kuwakuza wasanii Tanzania.
WITO
Lady Jaydee anatoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea kushirikiana na naye kwa kila namna, ili kukuza na kuendeleza kipaji chake na sanaa ya muziki wa Tanzania kwa ujumla wake.
Zaidi anatoa wito kwa makampuni kishiriki na kuungana nae ili waweze kumpa nguvu msanii, kutangaza biashara zao na kushawishi ajira katika fani ya muziki.
Na mwisho Lady Jaydee anawaribisha wote kusikiliza CDs zake au kuburidika na kundi lake la Machozi Band au kupata chakula ktk mgahawa wake wa kisasa Nyumbani Lounge au ukiwa umepumzika nyumbani utazame kipindi chake Diary Ya Lady Jaydee ktk EATV.

No comments:

Post a Comment