Wednesday, June 12, 2013


Mfanyakazi wa ndani wa Jaji Kileo auwawa kikatili dar...

MFANYAKAZI wa jaji Kileo, Philemon Laizer (27) anadaiwa kumchinja mtumishi wa ndani wa jaji ambaye ni raia wa Kenya Perpetua Mainab (30).

Mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa ni mtunza bustani katika nyumba ya Jaji Kileo alifanya unyama huo wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema mwili wa mtumishi huyo wa ndani ulikutwa ukiwa umetupwa kwenye dampo la kutupia takataka maeneo ya Mikocheni B.
 "Tukio hilo lilitokea karibu na dampo la kutupa takataka pamoja na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mfanyakazi huyo wa ndani alikuwa akiwa ameshakufa baada ya mwili wake kuchinjwa sehemu ya shingo na jeraha mkono wa kushoto karibu na kiganja, jeraha kwenye paji la uso na mwili wake ukiwa umepatapakaa damu sehemu za kichwani," alisema Kova.
 Alieleza kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akifanya kazi pamoja na marehemu alikiri kuwa na marehemu siku hiyo ya Ijumaa ya Juni 8 mwaka huu.
Alisema baada ya polisi kufanya upelelezi mtuhumiwa alikutwa na kiatu kimoja cha marehemu na nguo alizovaa siku ya tukio hilo zikiwa zimetapakaa damu.
Kamishna Kova alisema kuwa mtuhumiwa alipohojiwa alidai kuwa marehemu alitoweka nyumbani tangu siku ya Ijumaa na baada ya kubanwa na polisi mtuhumiwa alikiri kuhusika  na tukio hilo.
Kova alisema mtuhumiwa huyo bado anahojiwa na polisi na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Mwili wa Pepetua ukiwa umefunikwa.


Mwili wa dada huyo ukitolewa shimoni.
Mwili wa Pepetua baada ya kutolewa shimoni.
Kamanda Wambura alisema kuwa, Pepetua alikuwa akifanya kazi kwa Jaji Engera Kileo kwa miaka mitatu mpaka siku ya kifo chake.

Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari.

No comments:

Post a Comment