Wednesday, December 19, 2012

Amina Singo azikwa, wadau wamlilia

Marehemu Amina Singo
WAKATI mtangazaji na mwandishi wa michezo wa zamani wa Times FM, Amina Singo, akizikwa leo jioni, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko msiba huo uliotokea jana.
 
Msiba huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti kupitia taaluma ya uhandishi wa habari, Amina alifanya kazi na TFF, hivyo mchango wake katika mpira wa miguu tutaukumbuka daima.

Tutamkumbuka kama mtangazaji wa habari za mpira wa miguu na michezo kwa ujumla.  TFF tunatoa pole kwa familia za marehemu Amina Singo, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Marehemu enzi za uhai wake alifanya mambo mengi katika sekta ya utangazaji na muziki kwa ujumla, akishiriki katika kila jema linaloibua na kuendeleza maendeleo ya sanaa na michezo nchini.

Mungu aiweke roho ya marehemu Amina Singo mahali pema peponi. Amina

No comments:

Post a Comment