Friday, December 21, 2012

Waliofanya vizuri la Saba watajwa


OFISI ya Elimu Mkoa wa Dar es Salaam imetoa orodha ya majina ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2011 .

 Taarifa kutoka Ofisi ya Elimu ya Mkoa inaonesha kati ya wanafunzi hao, wanane wanatoka Shule ya Tusiime ambao na alama zao kwenye mabano ni Emmanuel Amos (233), Collins Hope (233), Esther Mayenga ( 232), Bertha Morgan (230), Joshua Richard (229), Kelvin Jackson ( 229), Gofrey Gervas (229) na Arafa Nyundo mwenye alama 228.
Wengine walio katika kumi bora ni Mateso Lutengwe wa Shule ya Manzese aliyepata alama 232, Latifa Kapiligi wa shule ya Chang’ombe mwenye alama 229 .
Aidha taarifa hiyo inaonesha wasichana walioongoza kwa ufaulu katika wilaya ya Ilala, saba wanatoka shule ya Tusiime na watatu wanatoka katika shule ya St Joseph.
Katika kumi bora kwa upande wa wavulana wilayani Ilala, wanane wanatoka shule ya Tusiime, wawili shule ya St Thereseofili na mwingine wa shule ya St Joseph.
Kwa upande wa Kinondoni kwa wavulana, wa kwanza anatoka shule ya msingi Manzese akifuatiwa na Mikocheni Hazina, Mirambo, Oysterbay, Msisiri, Gilman-Rutihinda, Kilimani, Magomeni na Bethel.
Wasichana wa wilaya ya Kinondoni ni wa shule za Ali Hassan Mwinyi, Kijitonyama, Mashujaa, Dk Omari A J, Mburahati, Mashujaa, Mirambo, Kawawa na Muhalitani.
Temeke kwa wavulana wa kwanza anatoka shule ya Uwanja wa Ndege akifuatiwa na wa shule za Maendeleo, Mbagala, Hamis Temeke, Kilimahewa, Nzasa, Kingugi, Montfort, Azimio na Montfort.
Wasichana kwa Temeke ni Chang’ombe wakifuatiwa wa shule za Sandali, Mgulani, St Mary’s, Mgulani, Mgulani, Chang’ombe, Mgulani, Jitihada na Mgulani.

Kwa hisani ya Habari Leo..

No comments:

Post a Comment