Monday, December 17, 2012

Watoto 20 wauwawa kikatili.........

Mtu aliyekuwa na silaha nzito amefanya mashambulizi katikashule ya awali iliyoko Newtown kwenye jimbo laConnecticut, nchini Marekani na kuwaua watu 26 wakiwemowatoto wadogo 20 wenye umri kati ya miaka 5 hadi10.

Mtu huyo anayekadiriwa kuwa katika umri wa miaka 20,alivamia darasa kwenye shule hiyo ambayo mama yakealikuwa mwalimu na kumfyatulia risasi mama yakepamoja na wanafunzi 18 darasani humo kabla ya kuwauwa watuwazima watano na kisha kujiua mwenyewe.

Wanafunzi wengine wawili walifariki wakiwa hospitalini kutokana na majeraha waliyopata. Polisi wamesema kuwa hilo ni moja kati ya matukio mabaya ya mauwaji ya raia katika historia ya Marekani. Polisi imesema kuwa mtu huyo alikutwa amekufa ndani ya shule hiyo.
Muuwaji anaripotiwa alikuwa na silaha nne za mkononi na alivalia mavazi ya kujikinga na risasi. Mtu mwingine alikutwa amekufa kwenye mji huo wa Newtown na kufikisha idadi kuwa 28.

Obama awalilia watoto waliouawa


Rais Barack Obama akizungumzia mauwaji ya Newtown, ametoa tamko akiwa katika hali ya majonzi makubwa kwenye Ikulu ya nchi hiyo White House na kuapa kupigania udhibiti wa silaha kwa kiwango kikubwa.
Obama alionekana akijifuta machozi mara kwa mara wakati anazungumza na waandishi wa habari kuhusu vifo vya watoto wadogo ambao aliwaita "watoto wazuri wenye umri wa miaka kati ya 5-10".
Alisema "leo mioyo yetu sote imevunjika. Wazazi, bibi na babu, dada na kaka wa watoto hawa wadogo na pia familia familia za watu wazima waliouawa kwenye kisa hiki" alisikika Obama katika sauti ya mtu anayelia.
Mara baada ya kuenea kwa tarifa hizo za mauwaji, wazazi waliokuwa na wasiwasi walikimblia shuleni hapo kuwatafuta watoto wao wakati wanafunzi waliokuwa wamelowa damu walipokuwa wanatolewa nje ya jengo. Mamia ya wakazi wa Newtown wamekusanyika katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Rose wa Lima lililopo umbali mdogo kutoka eneo la tukio kuwaombea waathirika.
Taarifa kuhusu mshukiwa
Taarifa kuhusu mshukiwa wa mauwaji hayo zinasema kuwa kijana huyo anatambulika kwa jina la Adam Lanza na mama yake aliitwa Nancy Lanza. Silaha zilizotumiwa na kijana huyo zilinunuliwa kisheria na mama yake mzazi. Jirani wa mama huyo amesema kuwa aliwahi kumweleza kwamba anapendelea mafunzo ya kufyatua risasi na wanawe.

Kikosi cha usalama kwenye eneo la tukio Kikosi cha usalama kwenye eneo la tukio.
 
Hapo awali vyombo vya habari viliripoti kuwa kijana ajulikanae kwa jina la Ryan Lanza mwenye umri wa miaka 24 ndiye mshukiwa wa mauwaji hayo. Baadae ikafahamika kuwa Ryan ni kaka mkubwa wa Adam.
Ryan alikuwa kazini New York City wakati muuwaji alipofyatua risasi katika shule ya awali ya Sunday Hook. Miongoni mwa watu wazima waliouawa ni pamoja na Mkuu shule hiyo ambaye ni mwanamke aliyefahamika kwa jina la Dawn Hochsprung.
Hochsprung alikuwa miongoni mwa watu watatu waliokimbilia kwenye madarasa ilikosikika milio ya risasi pamoja na msaidizi wake na mwalimu wa saikolojia shuleni hapo. Baada ya muda mkuu msaidizi alitoka nje ya eneo akiwa amejeruhiwa mguu na wawili hao hawakurejea na baadae kufahamika kuwa wameuawa.

No comments:

Post a Comment