Friday, June 21, 2013

MWANAFUNZI APIGWA RISASI TUMBONI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM USIKU WA KUAMKIA LEO



Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni hapo.
Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe kompyuta zao na pochi za fedha. 


Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa kompyuta hizo na pochi za fedha,  na majambazi kuanza safari yao ya kuondoka bila kuwadhuru.

Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.

Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa bila kupata majibu na ndipo walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi.


 Kwa sasa mwanafunzi huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka....

Miaka 13 ya kikosi cha mizinga leo.......usikoseee

MWENYEKITI wa Chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika onyesho la maadhimisho la miaka 13 ya Kikosi cha Mizinga zinazotarajiwa kufanyika leo kwenye ukumbi wa Msasani Club, jijini Dar es Salaam.

Kiongozi wa Kikosi, Karama Masoud 'Kalapina' alisema jana kuwa Prof Lipumba ndiye atakayekuwa mgeni rasmi baada ya mipango ya awali kumualika Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan kushindikana kumpaka kwa kuwaomba udhuru.
Kalapina alisema maandalizi ya onyesho hilo ambalo mashabiki watalazimika kulipa Buku 5 tu mlangoni, yamekamilika ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya wasanii na makundi yatakayowasindikiza katika onyesho hilo ambalo litaambatana na maonyesho mbalimbali yenye asili ya utamaduni wa Hip hop.
"Maandalizi ya onyesho la Kikosi cha Mizinga yamekamilika ikiwemo kutarajiwa Mwenyekiti wa Kitaifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgeni rasmi baada ya kumkosa Mhe. Idd Azan, pia burudani zimeongeza zaidi katika kunogesha miaka hiyo 13," alisema Kalapina. 
Mkali huyo ambaye pia ni mwanaharakati na mwanasiasa alisema baadhi ya wasanii watakaoshiriki kupigwa mizinga 21 ya Kikosi kesho ni Afande Sele, Young Killer, Manzese Crew, Stereo, Kala Jeremiah, LWP, Mansu-Lee, Gangwe Mob  wakiwa na Inspekta Harun na wengine wakiwamo Kikosi cha Mizinga chenyewe.
Shughuli nyingine zitakazoambatana na onyesho hilo ni maonyesho ya uchoraji na kupaka rangi, mitindi ya nguo na mavazi, kucheza break dance na utoaji wa tuzo kwa watu na asasi zilizosaidia Kikosi cha Mizinga kufika hapo ilipo ikiwa inatimiza miaka hiyo 13 tangu kuzaliwa kwake.