Friday, June 21, 2013

MWANAFUNZI APIGWA RISASI TUMBONI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM USIKU WA KUAMKIA LEO



Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni hapo.
Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe kompyuta zao na pochi za fedha. 


Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa kompyuta hizo na pochi za fedha,  na majambazi kuanza safari yao ya kuondoka bila kuwadhuru.

Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.

Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa bila kupata majibu na ndipo walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi.


 Kwa sasa mwanafunzi huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka....

No comments:

Post a Comment