Kala Jeremiah agawa tuzo yake kwa Marehemu Albert Mangweha....
Kala Jeremiah akitoa neno la shukranii baada ya kupokea tuzo zake.... |
Leo hii nimepita ukurasa wa mtandao wa kijamii wa facebook kwwenye akaunti ya msanii bora wa hiphop Tanzania, mtunzi bora na
msanii mwenye wimbo bora wa Mwaka....Kala Jeremiah, ambapo nilikutana na ujumbe huu....naomba niufikishe kama alivyoandika yeye mwenyewe.......
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA KWA UJUMLA.
MIMI KAMA MSANII BORA WA HIP HOP KWA MWAKA HUU NAPENDA KUCHUKUA MUDA
HUU KUWATANGAZIA WATU WOOTE KUWA. KATIKA TUZO TATU NILIZOCHUKUA MOJA
NAIKABIDHI KWA ALBERT MANGWEA.YANI NI TUZO YA MANGWEA NA NITAIPELEKA KWA
MAMA MZAZI WA MANGWEA MOROGORO.
NIMEAMUA HAYO KWA KUWA HAYATI
ALBERT MANGWEA ALIKUWA ANAFANYA MZIKI AMBAO UKO UPANDE AMBAO MIMI
NIMESHINDA TUZO TATU YANI HIP HOP.
TUZO NILIYOAMUA KUMPA MANGWEA NI TUZO YA MSANII BORA WA HIP HOP. KWA KUWA ALIKUWA ANASTAHILI PIA KUITWA HIVYO.
TUZO HII NAAMINI ITAKUWA UKUMBUSHO MHIMU SANA KWA FAMILIA YAKE.LAKINI
PIA ITAKUWA INAONYESHA MSHIKAMANO WETU KAMA WASANII WA HIP HOP.
POPOTE ULIPO KAMA WEWE NI SHABIKI WA HIP HOP TAFUTA NJIA YOYOTE YA KUENDELEA KUMUENZI NDUGU YETU
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI HIP HOP.
No comments:
Post a Comment