MWENYEKITI wa Chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika onyesho la maadhimisho la miaka 13 ya Kikosi cha
Mizinga zinazotarajiwa kufanyika leo kwenye ukumbi wa Msasani Club,
jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa Kikosi, Karama Masoud 'Kalapina' alisema jana kuwa Prof Lipumba ndiye atakayekuwa mgeni rasmi baada ya mipango ya awali
kumualika Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan kushindikana kumpaka
kwa kuwaomba udhuru.
Kalapina alisema maandalizi ya onyesho hilo ambalo mashabiki
watalazimika kulipa Buku 5 tu mlangoni, yamekamilika ikiwemo kuongezeka
kwa idadi ya wasanii na makundi yatakayowasindikiza katika onyesho hilo
ambalo litaambatana na maonyesho mbalimbali yenye asili ya utamaduni wa
Hip hop.
"Maandalizi ya onyesho la Kikosi cha Mizinga yamekamilika ikiwemo
kutarajiwa Mwenyekiti wa Kitaifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa
mgeni rasmi baada ya kumkosa Mhe. Idd Azan, pia burudani zimeongeza
zaidi katika kunogesha miaka hiyo 13," alisema Kalapina.
Mkali huyo ambaye pia ni mwanaharakati na mwanasiasa alisema baadhi ya
wasanii watakaoshiriki kupigwa mizinga 21 ya Kikosi kesho ni Afande
Sele, Young Killer, Manzese Crew, Stereo, Kala Jeremiah, LWP, Mansu-Lee,
Gangwe Mob wakiwa na Inspekta Harun na wengine wakiwamo Kikosi cha
Mizinga chenyewe.
Shughuli nyingine zitakazoambatana na onyesho hilo ni maonyesho ya
uchoraji na kupaka rangi, mitindi ya nguo na mavazi, kucheza break dance
na utoaji wa tuzo kwa watu na asasi zilizosaidia Kikosi cha Mizinga
kufika hapo ilipo ikiwa inatimiza miaka hiyo 13 tangu kuzaliwa kwake.
No comments:
Post a Comment