Wednesday, June 12, 2013

Hali ya Mandela ina 'utata'.....

Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa hospitalini kwa siku ya nne ambako anapokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu.
 
habari kutoka kwa ofisi ya rais Jacob Zuma, zinasema kuwa Mandela mwenye umri wa miaka 94, yuko katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa.
Jamaa zake pamoja na aliyekuwa mkewe Winnie Madikizela-Mandela, walimtembelea hospitalini Jumatatu
Serikali imekuwa ikisema kuwa hali ya Mandle inatia wasiwasi ingawa madaktari wameweza kuidhibiti.
Amekuwa katika chumba ya wagonjwa mahututi tangu kulazwa hospitalini Jumamosi kwa mara ya tatu mwaka huu.
Mwezi Desemba , bwana Mandela alilazwa hospitalini kwa siku 18 baada ya kupata maradhi ya mapafu,

No comments:

Post a Comment