Safari ya mwisho ya Abert Ngwea.....'cowbama'...
MAELFU ya watu walijazana leo katika Mkoa huu wa Morogoro kwa ajili ya mazishi ya msanii Albert Mangweha Ngwair, huku aliyepata naye matatizo nchini Afrika Kusini, Mgaza Pembe M to The P naye akiwa miongoni mwa waliohudhuria mazishi ya Ngwair.
MAELFU ya watu walijazana leo katika Mkoa huu wa Morogoro kwa ajili ya mazishi ya msanii Albert Mangweha Ngwair, huku aliyepata naye matatizo nchini Afrika Kusini, Mgaza Pembe M to The P naye akiwa miongoni mwa waliohudhuria mazishi ya Ngwair.
Hapa
jeneza la Ngwair linaingizwa karubini, ikiwa ni picha inayoonyesha kuwa
hatutaweza tena kukutana na msanii huyu hapa chini ya jua. R.I.P
Ngwair.....
Hapa
M to The P akilia baada ya kupita kwenye jeneza la Ngwair katika Uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika Kihonda
Kanisani jioni yake.
Mama
wa Ngwair akizungumza na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Joel Bendera, leo mjini
Morogoro, kabla ya mazishi ya msanii huyo wa Hip Hop Tanzania
Mwili wa Ngwair unaingizwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.Inaendelea hapo chini.....
Mbunge Sugu anamuaga Ngwair katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Hapa
watu wanakanyagana kwa ajili ya kujipanga mstari kwenda kumuaga
marehemu Ngwair, leo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro ulikuwa umejaa watu, sambamba na wale
waliojipanga barabarani kwa ajili ya kuangalia msafara wa Ngwair
uliofunika mji wote siku ya leo.
Tukio la kuzikwa lilitanguliwa
na shughuli ya uagaji iliyofanyika pia katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro,
baada ya kuona mkanyagano wa watu wengi nyumbani, usiku wa Jumatano, ambapo
taarifa za kuwasili kwa mwili wa Ngwair zilienea.
Makaburini
nako kulikuwa hakutoshi baada ya watu wengi kufurika, huku kila mmoja
akiwa na lake, wakiwapo wale waliokwenda kwa ajili ya kuangalia wasanii
wao.
No comments:
Post a Comment