Thursday, October 11, 2012

RUDI yapata tuzo ya ubora kimataifa


Mkurugenzi Mtendaji wa RUDI, Abel Lyimo kulia akiwa na mwenyekiti wa bodi ya RUDI wakiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) tuzo hizo.

 Viongozi wa RUDI waliokuwa wakiongea na waandishi wa habari leo.

Na Carren-Flora Mgonja
TAASISI ya Maendeleo Mijini na Vijijini (RUDI) imepata tuzo ya ubora wa kazi za kuhamasisha
kilimo na mafanikio katika mapinduzi ya kijani kwa wakulima wadogo nchini.
RUDI ilipokea tuzo hiyo hivi karibuni kutoka kwa aliyekua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Koffi Annani mjini Arusha wakati wa mkutano wa kimataifa wa
Akizungumzia tuzo hiyo Mwenyekiti Mtendaji wa RUDI Abel Lyimo alisema tuzo hiyo imetolewa na
Shirika la Ubia wa Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA) na kutambuliwa kuwa taasisi binafsi
lililohamasisha mapinduzi ya kijani Tanzania .
 “Tinashughulika zaidi na wakulima wadogo tukiwahamasisha walime mazao ya nafaka hasa
mpunga… lengo ni kuwainua wakulima na kukifanya kilimo kiwe kweli uti wa mgongo wa uchumi wa
Tanzania .
“…Ilikua furaha kwetu kwa sababu ni RUDI pekee ndiyo iliyopokea tuzo hii kutoka Tanzania
mbele ya rais Jakaya Kikwete, tukaona kwamba mchango wetu unatambuliwa ndiyo maana leo
tumeamua kuzungumza na waandishi wa habari ili taifa litufahamu zaidi,” alisema Lyimo.
Alisema kazi kubwa inatofanywa na taasisi hiyo iliyoanza mwaka 2007 ni kuanzisha na
kuimarisha vikundi vya wakulima kisha kuviunganisha na asasi za fedha na masoko.
Kwa mujibu wa Lyimo tangu kuanzishwa kwa RUDI iliyowezeshwa na Asasi NORGES yenye maskani
yake nchini Norway wamewafikia wakulima zaidi ya 60,000 katika mikoa nane ya Tanzania Bara.
Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Mbeya, Morogoro, Iringa, Dodoma , Singida, Shinyanga, Geita na
Njombe huku akisisitiza kwamba kabla ya kuwafikia wakulima huzungumza na serikali ya wilaya
husika kufahamu vipaumbele vyao.
“Wakulima tunaofanyakazi nao tumewaunganisha na makampuni ya wauza pembejeo binfasi pia
wamefaidika na mfumo wa uhifadhi wa mazao kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani…zaidi ya sh
bilioni moja zimetumika,” alisema na kuongeza kwamba lengo ni kuwafikia wakuliam 100,000
baada ya miaka mitano.

No comments:

Post a Comment